Mafian cartel
JF-Expert Member
- Nov 19, 2021
- 3,876
- 7,118
[emoji23][emoji23][emoji23]Nilifaulu A Level moja ya shule bora Mkoani kilimanjaro, Kipindi hicho ndo nipo maskani nafanya maandalizi ya kununua baadhi ya vitu ili niweze kusafiri siku inayofuata, Nakumbuka nilikuwa nimepiga mishe mishe nyingi sana kitaa tangu nilivyomaliza form 4 nikajichanga kununua simu ya elfu 40 ya button , kipindi hicho ni simu nzuri sana yenye display ya visamaki vikiwa vinatambaa, pia nikanunua baadhi ya vitu vya muhimu vya shule kama sabuni, viatu, sare nk. na hela ikawa imeshakata, nikabaki na hela ya ada nikaamua kuiweka kwenye simu ili nikifika Moshi niweze kuitoa nikalipie shuleni.
Sikuwahi kufika Moshi kabla, na Mzee hakunipeleka kwani alikuwa anasumbuliwa sana na miguu kipindi hicho, Ikabidi nikomae mwenyewe nianze safari, bahati nzuri nikawa nimepata connection ya mawasiliano na bro mmoja aliyemaliza shule kabla yetu hivyo alipangiwa shule ninayoenda mimi , yeye alikuwa form 6. Akaanza kunielekeza baadhi ya vitu na kipi nifanye nikifika moshi. Haya Safari ikaanza, nilikuwa natokea Dodoma, Kipindi hicho unapitia kwanza Singida kabla ya kujengwa hii barabara ya shortcut ya babati. Safari imeanza vizuri tu tukafika Singida fresh, tukapiga tea dakika 10 tukaingia tena kwenye basi hadi babati, nafika babati tukaambiwa tuna dakika 10 za kula msosi, Nimekula fresh nikaingia kwenye basi nikae, kujisachi sion simu, nikakumbuka niliiweka mfuko wa shati, akili ikanijia na nikajua hapa nimeshapigwa. Kumwambia konda sioni simu akazidi kukazia ,dogo hapa ushaibiwa, Sio sehemu nzuri sana, pole sana...Daaah nikakumbuka laini ilikuwa ni mpya na namba sikuikariri, na nilishaweka hela ya ada, kichwa kikaanza kuniuma. Isitoshe namba ya yule jamaa nikawa nimeipoteza na sikuwa nimeikariri. Nilisafiri kwa mawazo sana siku ile. Nikafika Moshi usika kama saa 2 hivi, mfukoni nina elfu 4, nikaulizia magari yanayoenda shuleni, nikaambiwa huwa yanaenda mwisho saa 2 usiku kwahiyo nilishachelewa, ni nje ya mji kidogo. Dah, ikabidi niombe hifadhi kwenye basi nilale ili kesho niondoke, hapo nishaazima simu sana kumpigia mzee tangu mchana simu yake haipatikani, nikawa chakula cha mbu usiku ule.
Asubuhi nikaelekezwa magari ya shuleni na nikafanikiwa kufika shuleni kwa kulia sana na konda maana nauli ilipelea, sasa shuleni walimu wakawa wanagoma kunipokea sina ada sina godoro, kila napojaribu kuwaelezea mkasa ulionikuta wakawa wanahisi ninatunga, baada ya kuhangaika nao sana wakaniruhusu. Nakumbuka niliishi maisha magumu sana, mahitaji mengi yaliisha mixer madeni ya shuleni nikawa sina amani kabisa. Likizo time sikutaka kwenda home kabisa nilikosa hata nauli, tukabaki mimi na wenzangu (hasa wanafunzi waliokuwa wakiishi mikoa ya mbali kama kigoma na mwanza,) tukawa tunamsaidia mwalimu wa economics kulima shamba lake na kupanda, namshukuru sana likizo yote tulitumia shambani, alikuwa anatulipa vizuri sana na alikuwa mkarimu sana yule mwalimu (RIP), tulivyofungua Shule shida zote zikawa zimeisha nikafanikiwa kupunguza madeni na pia ile hela iliyokuwa kwenye laini voda waliirudisha kwani nilienda kurenew laini, kuna bro yule wa shulen alikuwa na namba yangu, hivyo kurenew ikawa simple sana, nikawa don sasa shulen hadi wanafunzi wakashangaa.
Ila nilijutia sana kuipoteza simu yangu, niliitumia siku moja tu, na niliitafuta kwa hela ya jasho langu[emoji20]
We mwizi uliyeniibia simu babati kama upo humu Mataccor yako
YNWA
Sent using Jamii Forums mobile app