Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Nilipewa Kipigo Na Wanafunzi Wenzangu (Nilikuwa Snich)[emoji21][emoji21]

.
.
Nikiwa uko o level 2013 Moro uko boding shule moja ivi (sitaki mnikimbuke kama mpo humu)

Kuna Maticha Waliniomba Niwe Mpelelezi (Snich) Napeleleza Mambo Ya Hostel ya Wanafunzi Hapo Nipo Kidato Cha Pili


Nilikuwa Naishi Vizuri Sana Maana Kupata Vibuku 3 Kutoka Kwa Maticha Ilikuawa Ni Uwakika Na Nilikuwa Snich mzuri Vijana Wakipanga Kitu Nikisikia Tyuu Wanakuta Walimu Wameisha Pata Taarifa

IKAFIKA SIKU YANGU [emoji24][emoji24]....

Wanafunzi Wakawa Wamepanga Kuleta Mgomo Wa Msosi Mgomo Huo Walita Wafanye Mida Ya Usiku Nyumban Kwa headmaster

Bhana Snich Nikapata Taarifa Chapu Nikaenda Kwa Kwa Maboss Nikatema Vyote Walimu Wakaita Kikaoo Cha Fasta Kwa Wanafunzi Wote Baati Nzuri Au Mbaya Hawakupata Ushaidi Wowote Kama Ni Kweli Walitaka Kuandamana

Sasa Mbaya Kuna Nigga Aliniona Natoka Ofisini Kwa Ticha Alie kiwa anaongea Sana Kwenye Icho Kikao... Jamaa Akawastua Maniggah Midaa Ya Saa Sita Usiku Nimelala Zangu Ivi ...

Nikajikuta Nimevutwa Vibaya Nikamulikwa Na Tochi Kama Mia ivi Nikawa Sio Vizuri Nikashambuliwa na Mataulo Mabichi Usoni Kama dakika 2 Ivi Yaan Sielewii [emoji24][emoji24]

Wakanituliza Wakaanza Kuhojii Kwa Zile Sura Nilivo Ziona Ikabidi Nifunguke Yote Yaan kila kitu Kuna Jana Mmoja alikuwa Anajiita Kopo Akawaambia Mm Ntamchapa Fimbo 20 Za mgongoni

Daah Yule Jamaa Nikatili Sana Jamaa Alinipiga Zile Fimboo Bila Huruma Tena Nikiwa Mgongo Wazi Daah [emoji24][emoji24]

Sitakuja Kusahau Kesho Yake Niriludi Nyumbani Na Kuhama Shule ..

Sema Usnich Mbaya Sana [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hiyo ndo dawa ya mnoko,unasaliti wahuni kwa vipande vya fedha.
 
Siku niliyokamatwa napiga punyeto na bro:

Wakati nipo shule o-kevel hakuna kitu nilikua nakichukia kama club za masomo. Nakumbuka ilikua kila alhamisi, kilichokuwa kinanifanya nisipende ni maswali mengi kutoka kwa walimu na viongozi wa club husika yaani unapigwa maswali mbele ya madogo na ukikosea kujibu full aibu.
Basi wakulungwa wengi tulikua tunajazana kwenye club za michezo na fema. Mimi nilikua napenda fema coz ya mada nyingi ni za ujana. kule ndo nilipopata ujuzi wa kupiga punyeto. Wale jamaa walikuwa wanagawa na magazeti yao ambayo ndani wanasema njia mojawapo ya kujikinga na ukimwi ni ngono salama mojawapo ni punyeto a.k.a. selfee.

Basi bwana nilikua na mshkaji wangu anaitwa yaseen, huyu bwana anajua stye zote za punyeto na utamu wake, mara akwambie nyingine unapita mkao wa kukata gogo, nyingine unapiga umelala chali na ukikaribia kumwaga unapanua miguu unaanza upya. Hizi style zake zilinikosha kinoma. Huyu bwana alitoa ahadi siku akija kununua pc kitu cha kwanza atajaza video za x mtupu coz ndo starehe yake. Sitasahau kuna siku alikuja geto kuchek x kwenye pc ya bro mvua ikaanza kunyesha akalazimika kutoka hvohvo na mvua kisa anawahi kudowload ( kukumbuka) kabla muda haujapita ili asisahau akadai ili punyeto iwe tamu.

Kupitia huyu jamaa ndio nilikuja kujua kuwa kuna mshkaji wetu alikua mtu wa dini kinoma tena kiongozi alipiga punyeto getoni kwake akazimia akakutwa na bro ake hajitambui, nilicheka kinoma, huyu jamaa tulizoea kumwita kakoba coz alifanana sana na mshkaji mmoja kwenye maigizo ya ITV ya kila jmoc usiku alikuwa anaitwa mjomba kakoba.

Pole pole na mimi nikaanza huu mchezo wa punyeto na full kuapply style za mskaji wangu yaseen the master. Siku zote nilizoea kupigia bafuni, nilikua na mtindo wa kuoga maji ya moto hata kama ni mchana, nyumbani walinishangaa kinoma, kumbe mimi nilikua na lengo langu. Maji ya moto nilikua nayamwagilizia pale nnapokaribia kupiga bao + na lile joto la maji raha yake sio ya nchi hii. Hii style alinipa master wangu yaseen.

Basi bhwana chumbani nilikua nalala na bro sasa kuna siku bro alisema anaenda town nkakumbuka ndo mida sahihi ya kupiga puli coz pc ameiacha. Nkachukua cd yagu ya pilau nkaiweka nkaanza kuangalia baada ya mzuka kupanda nkachukua mafuta nkapaka kwenye mashine nkaanza taratibu kupiga punyeto, nilipata ujasiri wa punyeto ni salama hasa baada ya kushauriwa na fema club shuleni. Sasa ile utamu umekolea mara bro huyu hapa karud gafla na isitoshe mlango sikuufuga, aisee nilistuka balaa nachanganyikiwa nishike kipo nivae nguo coz nilivua zote au nizime pic, so nkabaki tu nimeduwaa sijui la kufanya. Daaah bro alimaind kinoma na isitoshe alikua ananiamini kinoma kila siku ananiona sio mtu wa mambo hayo . Bro ikabid aanze kunishauri kila siku kuwa mchezo huo sio mzuri. Moyoni nilimlaumu sana jamaa yangu yaseen coz alichangia pakubwa kwa mimi kuwa mpiga punyeto maarufu.

Kisa kinachofuata:
nilinusurika kufumaniwa na baba wakati nafanya mapenzi na beki tatu jikoni. Kalituona kadogo kamoja kakaja kusema sebuleni.
Unapiga nyeto huku umevua nguo zote, du we ni konki.
 
Nilidate na mtoto wa polisi enzi hizo yeye alikuwa form 4 nadhani lile funzo nililopata hadi Leo nikiona sketi za shule moyo unaliaa Paaaaa...!! Bila dada yake i was gone for good jela ingenihusu aiseee..
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ilikuwa Kimasihara?
 
FUJO ZA WANAFUNZI NA WANAKIJIJI


Dah miaka hiyooo. Nipo sekondari O-level mkoa fulani hiviii waliosoma hapo wataikumbuka hii story maana nilikua aina ya wale wanafunzi ambao anafahamika shule mzima na nilikua nataniwa na kila mtu.

Kulikua na shida kubwa sana ya maji katika mji huo hivyo kulazimika wanafunzi wa shule za boarding za hapo kuwa na kawaida ya kutoka nje ya shule kutafuta maji huko mitaani yaani ilikua ni ubabe na vurugu maana kilichokua kinahitajika ni maji yawe ya kisima salama, kisima cha wazi/shimo ama hata ya mfereji lakini maji yafike shule kwa matumizi binafsi na matumizi ya jikoni endapo darasa lako litakua na zamu na kipindi hiki hata ratiba za darasani hazikua sawa maana wenye zamu ya jikoni wakizingua basi uji mnakunywa saa sita mchana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] au kula wali saa sita usiku kosa maji yamechelewa ilikua kawaida.

Kipindi hicho ilikua inafika hatua mtu ukimaliza kula inabidi uilambe sahani yako kwani hakukua na maji ya kuoshea, tulikunywa maji machafu yaani machafu unayoyajua wewe yaani ile ndoo mnayoingia nayo bafuni(nadhani mnajua hali ya maliwato za shule za bweni za serikali) ndio hiyo mnaitumbukiza kisimani mnachota maji kwa matumizi yooote kuanzia kunywa, kuoshea, kufulia, kupikia,nk hapo kutumia maji chooni ilikua anasa zaidi ya makaratasi na magodoro[emoji2955][emoji2955][emoji2955].

Basi nilikua na kakundi kangu tunajikuta manundaaa hatuogopi mbuzi yeyote baada ya chakula cha jioni tumeenda kunyanyua vyuma ikabidi tushuke kitaa kusaka maji na kuoga hukohuko ilikua mida ya saa mbili usiku no body caring about the so called night prepo.
Sasa kufika kwenye kisima cha wazi kikubwa zaidi hatukukuta foleni tukajichotea maji na kuoga. Wakati tunaoga kuna majamaa wawili ambao ofcourse tulikua tunafahamiana nao (kutokana na harakati zetu chafu na uhuni za mtaani) walikua wanaishi jirani kabisa na kisima na walikua wamelewa, sasa wakaanza kututolea maneno machafu sana na ninaamini hawakututambua kutokana na kulewa.

Kikatuuma sana wana tulikua 6 tukaamua tukiwashe, ukumbuke ni usiku sasa hiyo inaenda saa nne basi tukawachezeshea kichapo na walipiga kelele kinoma nadhani hadi wanakijiji wengine wakasikia. Ili kuonesha sisi ni wababe zaidi tukaanza kurusha mawe mazito kwenye paa la nyumba ya washkaji ASALALEEEEH kumbe wanakijiji wamejikusanya waje kutoa msaada.

Sasa kutokana na jeuri ya wanafunzi wanapokua wanafuata maji kijijini kulikua na chuki imejengeka kwa wanakijiji juu ya wanafunzi ni vile tu walikua wanakosa namna ya kulipiza sasa na sisi ndio tukawa tumeingia king wenyeweee. Ebwanaee, baada ya kumaliza hilo timbwili letu kuwapiga majamaa na kufanya vurugu tukaamua tusepe sasa njia ilikua ni ile ya imesongwa na nyasi so mnavyopita mnakaa kama msululu kama bata na wanae mimi nikiwa wa mwisho kabisa nikiwa nimebeba maji nusu ndoo na tochi mkononi.

Ghafla tunakutana na nyomi la wananzengo mzee mwenye jiwe, fimbo na silaha nyingine za jadi kumbe wanatulia timing basii nilichosikia ni WEZI WENYEWE HAWA HAPAAA KAMATAAA.

Ilikua ni nyuma geuka, mimi nikawa wa kwanza nilikimbia nikapaa kile kisima ambapo hadi leo sijui niliwezaje mbele kulikua na matuta yale ya majaruba nikajikwa nikaanguka, hapo ujue wanakijiji wametuungia na kelele za weziiii weziiiiii[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91].
Ile nataka kuinuka nikasukumwaa na mwenzangu nikarudi chiniiii wanakijiji hawa hapaaa, usiombe babaangu, ndani ya sekunde kadhaa nilikua nakiona kifo hiki hapa nilipiga kelele ambazo sijawahi kupiga maishani mwangu nikijitetea kuwa mimi sio mwizi bali ni mwanafunzi wa hiyo shule.

Nashkuru kuna mzee mmoja pale wenye hekima akaingilia kati nisiendelee kupigwa japo wanakijiji kila mmoja alikua na hasira na tabia chafu za wanafunzi mfano kuchota maji kibabe wakikuta foleni( yaani unaweza kuwa na kisima kwako ila tukifika tunakusubirisha kuchota hata ya kupikia), kuiba mazao ya bustani kama miwa na matunda, kuiba mademu zao, nk ambazo nyingine hata mimi nilikua nazo basi nikawa nimepelekwa sehemu kuna taa nahojiwa pale ratiba inayofuatia ni kupelekwa polisi kwa uharibifu tulioufanya na wakati huohuo kuna baadhi ya raia wenye hasira wananipa ngumi au makofi ya kuvizia, sisahau mshkaji mmoja yuliwahi kula demu wake namkumbuka vizuri kabisa alinipa kichwa cha pua aisee nikaishia kuona nyotanyota.

Lakini akatokea mwana ambaye alikua tunafanya nae michongo flani haramu akateteaa pale uwongo na ukweli nikaachiwa kwa mkwara mzito, hapo nahisi maumivu kila sehemu.
***********
Sasa wale wenzangu wengine walifanikiwa kufika shule na kugonga kengele ya dharula(ile shule ni moja ya shule inayoheshimu lengele za dharula yaani mtu anaweza asikimbilie kengela ya chakula ila ya dharula usiku ni dk chache tu wapo assembly. Basi jamaa mmoja fala sana akatangaza kuwa nimedakwa na wanakijiji huko wananibaka na tunavyozidi kuchelewa watakuta nimekufa hivyo washuke fasta kuniokoa.

Mwanaaa usiombeeee, ofisi ya vifaa ikavamiwa wa kutoka na fyekeo, jembe, fito za mafagio, mwenye jiwe, na silaha yoyote alibeba shule nzima yenye 800+ students ikashuka village na hasira maana ujue hapo wanafunzi na wanakijiji hawapatani.

Aisee mimi nimeachiwa pale hata wanakijiji hawajatawanyika, nakatisha kona ya kwanza kusepa nachechemea taratibu nipo na mwana aliyenitoa kwenye msala nakutana na wale vimbelembele wa skaut aisee wataka waanze na yule mshkaji nikawapooza nikamwambia mshkaji potea jeshi la kazi limefika hapo ukumbuke wanakijiji bado hawajatawanyika pale walipokua wakinihoji na wanafunzi wanazidi kuja wananiuliza hali yangu palee nikawaambia wabaya wote wapo hapo nyuma kama vipi tuwaibukie.

Kilichotokea huwa sipendi kukumbuka kilitembea kichapo hapo yaani palichafuka, yule mshkaji aliyenipiga kichwa cha pua aisee sikumuacha tulilipana palepaleee nadhani ndie aliyejeruhiwa zaidi maana wana walikua wananiuliza nioneshe aliyenipiga wote wamewekwa mtu kati alitia huruma sana maana alipasuliwa kweli kuna jamaa alimkata na jembe kichwani ameloa damu kichwa choteee. Basi mida ya saa saba operation ya kuniokoa ikaisha tukakusanyana wale wote tuliokua kwenye kisanga tukatunga story moja na kama tulijua, polisi hawa hapa shule tukabebwa hadi kituoni tukahujiwa kila mmoja peke yake na tukatoa story inayofanana.

Pamoja hayo yote ila ni shule ninayojivunia kwa shule zote na levels zote za kielimu nilizopitia ma huwa naimiss sana.
Duuuh mlitisha sana
 
Kipindi tupo form 6 mwanzo mwanzo kabisa kama wadau,washikaj tulioshibana tuliamua kutafuta chumba ambacho kitakuwa karibu na shule ili tusipate hadha ya kugombania daladala asubuh kila siku.

Kweli tukatafuta na hatimae tulipata chumba mita 500 kufika shule. Tukalipia maisha yakaanza.

Sasa tulikaa kama miezi 3 hivi na mitikasi ya shule mara umeingia hapa mara pale lazima uwe na mademu, Na sis advance tulikuwa tunawakula sana o level .

Basi tunachukua videmu vya shule tunaenda kuvikula geto, na vyenyewe vinanogewa vinazoea, vikifika shulen vinawahadithia wenzao. Kwahyo pale shuleni geto letu lilipata umaarufu mkubwa sana ikafikia hatua mpaka walimu wakajua ila tu hawakuamua kulivalia njuga.

Sasa miezi 2 kabla ya necta shule kunakuwa hakuna mpya kila mtu anasongoka kivyake kwa hiyo kwa sisi wa geto swala la kwenda shule lilikuwa ni kujiamulia tu unajikuta week nzima uko geto tu.

Sasa kilichofanya nijute kama muandishi "kuna mshikaji fulan pale shule alikuwa maarufu sana Coz alisoma pale since o level.

Huyu jamaa alikuja kutuomba aje akae geto kwa kwa miezi iliyobaki Baadhi tukamkubalia ila kuna mwana mmoja alitupinga kwa uamuzi tuliouchukua.

Basi siku 2 baada ya kumaliza pepa ya practical siku hyo tumelala mpaka saa 3 asubuhi tukaamua siku hiyo tusiende shule. Ila mim na jamaa yangu tukajadiliana tukasema tuende saa 4. Ilivyofika saa 4 haoo shule.

Tumefika shule ulizia mazingira jamaa wakasema hakukuwa na jipya ila kuna jamaa akatuambia walipewa pepa ya prac. Ah bas jama yang akaniashauri turudi geto nikawa nakaza kumbe machale yalikuwa yananicheza ila napotezea. Basi mwisho wa siku nikakubali tukarudi geto.

Sasa kumbe yule jamaa tuliyemkaribisha mama yake alikuja shule kwaajili ya kesi ya mdogo wake ambaye alikuwa ni kiongozi pale shule, sasa baadae akamuulizia yule mshikaj ikabid atoke MP mmoja ambaye alikuwa mnoko kinoma kwenda kumfata class.

Amefika madarasa ya form 5 karibu na vimbweta akakutana na karatasi ya mtihani wa jamaa inagaragara chini ikabidi auokote akawa anakuja nao darasani kwetu, kabla hajafika darasani kwetu akakutana na dogo fulan wa o level ambaye ni rafiki wa mdogo wake na mshikaji. Ikabidi amuulizie, yule dogo akamjibu yupo geto.

Yule MP hakuja tena darasani akarudi staff kuwapanga wenzake[emoji23][emoji23] wakamchukua yule dogo wakampandisha kwenye ndinga haooo mpaka get. Ila kabla hawajafika geto wakakutana na mshikaji mwenyewe ndo alikuwa anakuja skonga so wakamkamata kirahisi sana. Then wakamwambia awalete geto jamaa alivyokuwa boya akawaleta kweli[emoji23][emoji23]

Ile nyumba, tuliyokuwa tunakaa kulikuwa na geti kubwa na kigeti kidogo, sisi wengine tulikuwa geto jamaa yangu mmoja ni Artist mzuri tu yeye alikuwa anachora picha ya messi namim nakula ngoma taratiib[emoji16][emoji16] kuna jamaa yetu mmoja hivi mkurya yeye mda wote alikuwa kajichimbia maeneo anakula msuli. Na kuna jamaa mwingine alikuwa anadeki choo[emoji23][emoji23] basi hivyo ndo tulivyokamatwa.

Noo kuvaa sare ya shule ni kupakia ndinga na kwenda shule, tumefika kama mita 100 hivi kabla ya kufika shule kilianza kichurachura mpaka shule tumefika shule tulikula doso kali sana kiasi cha kujuta na kutosahau(kama mnavyojua wanajeshi wakisulubu)

Kutokea saa6 tumekuja kuachiwa saa 11 jioni wakati tunapewa vifaa vya kung'olea visiki na kuchimba shimo[emoji23][emoji23]

Nisiku ambayo nilijuta kupuuzia hisia zangu[emoji120][emoji120]
 
Kwenye Maisha tunajifunza kutokana na makosa na makosa yanaleta majuto kabla ya funzo.

Aidha ufanye kosa kwa siri au hadharani, ni lazima likugharimu kwa namna moja au nyingine na hivyo kupelekea majuto.

Kuna vitu huwezi kuzungumza na watu wanaokufahamu vizuri, kuna vitu vinabaki mioyoni mwetu kwa muda mrefu sana.

Lakini sehemu kama JamiiForums ambapo kila mtu ni kama mgeni tusiyemfahamu panafaa kabisa kutoa yale ambayo tunayabeba mioyoni mwetu kama majuto labda huenda yakamsaidia mtu mwingine kwa namna yake.

Unajutia vitu gani kwenye maisha yako?

Binafsi nina vitu fulani ambavyo niliwahi kujutia sana. Nitakuwa nashare kimoja kimoja kadiri navyopata muda.


FAKE BANK SLIPS

Kipindi fulani miaka kadhaa nyuma, wakati nasoma Chuo niliwahi kuingia katika harakati haramu za kuforge receipt za Malipo ya Ada. Ilinigharimu Sana!

Wakati huo maisha ya Chuo yamekuwa magumu sana, mambo ya ujana ni mengi halafu mpunga naotumiwa kutoka nyumbani hautoshi kabisa kumudu gharama zisizo rasmi.

Basi bhana, ilivyotokea hiyo story ya kuwa kuna namna unaweza kutoa pesa kidogo kama robo tu ya Ada unayolipa kisha ukapokea receipt halali ya Bank yenye malipo ya Ada kamili nikajikuta nimeingia mkenge kirahisi.

Tafuta connection mpaka nikakutana na jamaa mmoja ambaye ndio anaratibu huo mchongo. Kazi ikaanza. Wakati huo nipo mwaka wa mwisho ila Sem ya kwanza.

Nikaona maisha si ndio haya. Nakumbuka nilikua nalipa kama Mil 2 kasoro hivi ya Ada ya mwaka mzima. Kwahiyo nikawa nikitumiwa pesa ya Ada natoa kama jiwe 5 tu, receipt ya ada kamili hii hapa. Nikienda kwa mhasibu ni mhuri Twacha! Nishaingia kwenye kundi la walipa Ada naanza kupambana na Modules. Alikuwa wapi huyu Jamaa miaka yote hiyo nasota bure, Dah!

Sem ya kwanza ikaisha ki ulaini sana, Sem ya II ikaanza kama kawaida nikamcheck mzee wa michongo akanifanyia utaratibu chap maisha yakaendelea.

Kipindi hicho mpaka washkaji zangu wakawa kama hawanielewi elewi, si unajua tena zile umetoka na mwana kitaa kimoja anajua uchumi wenu vizuri halafu anashangaa mwana ghafla tu kila kitu huulizi bei na hukaukiwi Mchuzi! Duh, wangejua nilipojiingiza hata wasingekubali kupokea mia yangu.

Muda ukaenda, wiki zikakatika. UEs zikaanza. Kizaazaa kikaja!

Nakumbuka zilikua zimebaki kama paper 2 tu nimalize Chuo, katikati ya mtihani anaingia Dean of Student na maafande.

Heh! Moyo ukafanya Paah, Mkono ukaanza kutetemeka mpaka kalamu ikaanguka chini. Sijamalizia kuokota kalamu nasikia jina langu linaitwa, Mama yangu! Nimekwisha!

Nikasimama nikatoka nje wajomba wakaniambia kijana uko chini ya ulinzi. Kila mtu hapo ndani ya chumba cha mtihani wanashangaa. Laskaboza kafanya nini tena jamani? Mbona hanaga shida na mtu.

Unajua kuna kitu watu huwa hawajui kuhusu kukamatwa na mapolisi. Siku wanakuchukua huwa wanakuchukua kama utani vile, kama vile wanaenda kukuhoji tu kidogo kesho yake unatoka.

Aaah thubutu, nilikaa Central karibu wiki mbili, mpaka nikahamishiwa Magereza Bulalifuu. Naona kama ni Movie ya kihindi inanitokea lakini ni painful reality. Nimeshakuwa Mfungwa!

Wazee wakafunga safari kutoka mkoani wakaja Chuoni kujua kulikoni. Sitasahau aibu niliyoipata wakati namuona mzee wangu. Laskaboza? Imekuaje Mwanangu? Uliomba nini hukupewa? Pesa zote ulikuwa unapeleka wapi? Uchungu niliokuwa nao jumlisha na uchungu wa mzee, hali ikazidi kuwa Mbaya.

Story zikasambaa Chuo kizima, Laskaboza ni tapeli, ametapeli Chuo. Ubaya wa haya mambo, akikamatwa mwingine anasema wewe ndio ulimwambia kwahiyo mimi ndio nabanwa niseme mashine za kufyatulia Receipt ziko wapi. Niliteseka sana.

Kwa sababu hata yule jamaa aliyeniingiza huko alishamaliza Chuo mwaka mmoja kabla yangu. Kwaiyo alikua mtaani tayari. Alivyosikia nimedakwa, akapotea. Akawa hapatikani tena.

Aisee, hakuna rangi niliacha kuona. Hii story ni ndefu sana, ila ki ufupi nilikuja kuachiwa baada ya miezi 4.. walikuja kugundua hata mimi sijui mahali hizo receipt zinafyatuliwa.

Waliofanya mpango uvuje ni Auditors. Maana Chuo kilikuja kugundua pesa hazionekani Bank lakini zipo kwenye makaratasi.

Kwaiyo wakaguzi wa mahesabu wakishirikiana na Bank ndio wakagundua huo mchongo. Ki ukweli ulinigharimu sana. Nilijuta sana. Watu wa nyumbani kwetu walihisi nimelogwa ili nisimalize Chuo, Duh

Nilikuja kumaliza masomo yangu miaka miwili mbele, maana hapa katikati habari zangu zilikua zimeshasambaa sana.

Kwaiyo hata kurudi ikawa ngumu mnoo. Nilikuja kukubaliwa miaka miwili mbeleni baada ya mabadiliko katika uongozi wa Chuo kufanyika.

Hakika nilijutia sana

Kamwe usije ukaingia kwenye michongo meusi. Maana ina tabia ya kukolea kama sukari halafu ikishakolea unajisahau. Unajikuta umeharibu, maisha yanaanza kuwa Machungu!

Kisa kipi kilikufanya na wewe ujute sana?
Huruma uliniponza kulala na mwanamke nisiyempenda hata kidogo. Nililala na huyu mwanamama huku nikisikitika moyoni na kujuta kwanini nafanya vile, baada ya shoo kuisha yule mwanamama akawa ananichukulia mimi kama mumewe. Alikuwa hachoki kunipigia simu kila mara na kuniambia wajukuu wako wanakuulizia watakuona lini. Kwa kweli nilichoka maana hao wajukuu zake wenyewe hata kuwajuwa nilikuwa siwajuwi. Huruma "shikamoo" huko ulipo, sina hamu.🙌
 
Huruma uliniponza kulala na mwanamke nisiyempenda hata kidogo. Nililala na huyu mwanamama huku nikisikitika moyoni na kujuta kwanini nafanya vile, baada ya shoo kuisha yule mwanamama akawa ananichukulia mimi kama mumewe. Alikuwa hachoki kunipigia simu kila mara na kuniambia wajukuu wako wanakuulizia watakuona lini. Kwa kweli nilichoka maana hao wajukuu zake wenyewe hata kuwajuwa nilikuwa siwajuwi. Huruma "shikamoo" huko ulipo, sina hamu.🙌
We ulikula mbibi wewe
 
JKT

Katika harakati za kutafuta Ugali nilijikuta nimeomba kujiunga na jeshi la JKT. Nikatupiwa Kigoma, kule Bulombora 821KJ.

Nikapigishwa jaramba na kulishwa vumbi huku nikitazama ziwa Tanganyika kwa ukaribu kabisa lililozungukwa na mawese ya kutosha. Ruka Juu, Kanyaga Chini kwa nguvu mpaka mguu utoke nje ya kiatu.


Mikesha ilivyozidi nikaona hapa nitakufa. Nikaanza harakati za kutafuta nafasi ya kulala vizuri maana zile Dakika 5 unazopewa za kulala hazitoshi kabisa. Nikaanza kutafuta machimbo. Wenzangu wakienda mkesha, mimi najipeleka porini. Siku nyingine nakutana na ma afande na wao wamedoji kwenda lindo wananitimua najikuta nimerudi kulala uvunguni.

Tabia yangu ya kujizoesha kulala ikaanza kunigharimu. Ikafika mahali nikawa siwezi kabisa kwenda kukesha hata siku moja. Nikaanza kuona hadi uvivu wa kwenda kulala mbali na anga letu. Nakumbuka nilikua Eagle Coy.

Siku hiyo nimelala uvunguni nakoroma kabisa, saa ngapi afande asiingie ndani kutafuta watoro. Si akaniskia navyokoroma kule chini ya kitanda. Dah sitasahau hiyo kipigo niliyopewa. Nakumbuka al manusura nipoteze jicho. Maana vile vitanda vimechomelewa kwaiyo kuna kama vichuma flani hivi kama nondo vimejitokeza kwa juu, alinibamiza kichwa kwenye kile kitanda ile nondo ikachubua kidogo pembeni ya jicho.

Sijui nilipata wapi ujasiri nikamsukuma pembeni nikasogeza kioo cha dirisha nikarukia nje nikaanza kukimbia huku nachechemea machozi yananitoka ya kutosha. Jamaa nadhani aliniangalia navyokimbia kwa tabu akanionea huruma akaamua kuachana na mimi huku akisema "Nitakuua Mbwa Wewe".

Nilivyofika walipo wenzangu kwenye mkesha nikapokelewa tena na adhabu za kubiringita na kukwepa ndege za kivita. Dah.. nilihisi mwisho wangu umefika, nikasema kwa sauti "Nakufa" huku machozi yanatoka ili hata jamaa anionee huruma lakini wapi. Yeye kakazana kunioshea na kunifanya mfano kwa wengine. Saiyo pumzi imekata, maumivu kila mahali, machozi yameshatoka mpaka yamekauka, siwezi kuongea tena. Ni kwa Neema za Allah pekee nilifanikiwa kuona tena Jua siku iliyofuata maana nilikua nahisi kabisa nakufa. Hali yangu ilikua mbaya sana!

Sikuwahi kujuta kwenye maisha yangu kama hiyo siku. Nililaani uamuzi wangu wa kwenda huko. Kile kitu kilinikaa sana moyoni kwa muda mrefu. Niliona kabisa huku sio kwangu. Course ilivyoisha, wakati wengine wanasikilizia kwenda JWTZ na Polisi, mimi nikaandaa nauli yangu, nikavizia ule muda tunaotumwa kwenda town...nikatorokea huko mazima na nikaapa sitarudi tena. Ikawa imeisha hiyo!

Kwa kweli mambo ya Jeshi yana watu wake. I was not one of them!
aisee pole sana mkuu, hivi wengine hawafi huko kweli?
 
Huruma uliniponza kulala na mwanamke nisiyempenda hata kidogo. Nililala na huyu mwanamama huku nikisikitika moyoni na kujuta kwanini nafanya vile, baada ya shoo kuisha yule mwanamama akawa ananichukulia mimi kama mumewe. Alikuwa hachoki kunipigia simu kila mara na kuniambia wajukuu wako wanakuulizia watakuona lini. Kwa kweli nilichoka maana hao wajukuu zake wenyewe hata kuwajuwa nilikuwa siwajuwi. Huruma "shikamoo" huko ulipo, sina hamu.[emoji119]
Kila mbibii ndo akaanza kukuita babu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huruma uliniponza kulala na mwanamke nisiyempenda hata kidogo. Nililala na huyu mwanamama huku nikisikitika moyoni na kujuta kwanini nafanya vile, baada ya shoo kuisha yule mwanamama akawa ananichukulia mimi kama mumewe. Alikuwa hachoki kunipigia simu kila mara na kuniambia wajukuu wako wanakuulizia watakuona lini. Kwa kweli nilichoka maana hao wajukuu zake wenyewe hata kuwajuwa nilikuwa siwajuwi. Huruma "shikamoo" huko ulipo, sina hamu.[emoji119]
Ukila single mother kesho yake akikupigia anakwambia msalimie mwanao.
 
Back
Top Bottom