Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Nilipewa Kipigo Na Wanafunzi Wenzangu (Nilikuwa Snich)[emoji21][emoji21]

.
.
Nikiwa uko o level 2013 Moro uko boding shule moja ivi (sitaki mnikimbuke kama mpo humu)

Kuna Maticha Waliniomba Niwe Mpelelezi (Snich) Napeleleza Mambo Ya Hostel ya Wanafunzi Hapo Nipo Kidato Cha Pili

Nilikuwa Naishi Vizuri Sana Maana Kupata Vibuku 3 Kutoka Kwa Maticha Ilikuawa Ni Uwakika Na Nilikuwa Snich mzuri Vijana Wakipanga Kitu Nikisikia Tyuu Wanakuta Walimu Wameisha Pata Taarifa

IKAFIKA SIKU YANGU [emoji24][emoji24]....

Wanafunzi Wakawa Wamepanga Kuleta Mgomo Wa Msosi Mgomo Huo Walita Wafanye Mida Ya Usiku Nyumban Kwa headmaster

Bhana Snich Nikapata Taarifa Chapu Nikaenda Kwa Kwa Maboss Nikatema Vyote Walimu Wakaita Kikaoo Cha Fasta Kwa Wanafunzi Wote Baati Nzuri Au Mbaya Hawakupata Ushaidi Wowote Kama Ni Kweli Walitaka Kuandamana

Sasa Mbaya Kuna Nigga Aliniona Natoka Ofisini Kwa Ticha Alie kiwa anaongea Sana Kwenye Icho Kikao... Jamaa Akawastua Maniggah Midaa Ya Saa Sita Usiku Nimelala Zangu Ivi ...

Nikajikuta Nimevutwa Vibaya Nikamulikwa Na Tochi Kama Mia ivi Nikawa Sio Vizuri Nikashambuliwa na Mataulo Mabichi Usoni Kama dakika 2 Ivi Yaan Sielewii [emoji24][emoji24]

Wakanituliza Wakaanza Kuhojii Kwa Zile Sura Nilivo Ziona Ikabidi Nifunguke Yote Yaan kila kitu Kuna Jana Mmoja alikuwa Anajiita Kopo Akawaambia Mm Ntamchapa Fimbo 20 Za mgongoni

Daah Yule Jamaa Nikatili Sana Jamaa Alinipiga Zile Fimboo Bila Huruma Tena Nikiwa Mgongo Wazi Daah [emoji24][emoji24]

Sitakuja Kusahau Kesho Yake Niriludi Nyumbani Na Kuhama Shule ..

Sema Usnich Mbaya Sana [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Na hujaacha kusnitch
 
Duh! Uzi mrefu kiasi

Mwishoni mwa mwa mwaka 2011 karibia na kipindi cha msimu wa sikukuu nikiwa nasubiri majibu ya mtihani wa kidato cha nne. Nilikuwa naishi na bibi yangu katika moja ya mikoa ya nyanda za juu kusini.

Nilikuwa napenda sana kujifanya msela na kuiga uhuni kampani yangu kubwa ilikuwa ni masela kwahiyo bangi, viroba na sigara vilikuwa vinahusika sana pale tunapokuwepo kijiweni

Siku moja tukiwa kijiweni tulikuwa raia wawili tu siku hio alikuja mama mmoja akatupa tenda ya kumsaidia kupakia chupa, vinywaji na mazaga mengine ,(huyo mama alifiwa na mmewe miezi kama miwili nyuma mmewe alikuwa anafanya biashara ya kuuza vinywaji vya kawaida na vileo baada ya kufariki mmewe huyo mama alimua kufunga biashara).

Baada ya kumaliza kupakia kuna vitu vingine aliviacha ambavyo hakua na uhitaji navyo. Katika vitu alivyoviacha kuna boksi moja lilikuwa limejaa viroba vilikuwa vinaitwa double punch (sio double kick) vilikuwa kwenye pakti ya nylon. Yule mama alivyomaliza kupakia vitu vyake na kuondoka mimi nilichukua lile boksi la viroba nikaenda nalo gheto nikalificha lengo la kuficha ilikuwa nikawauzie washkaji wangu jumapili tukienda club

Ilivyofika jumapili tayari nishakula viwalo kwa ajili ya kwenda disko shetani akanibadilisha akili badala ya kuchukua viroba nikawauzie wadau mimi nikachukua chupa ya maji ya lita moja nikachana viroba vyote nikavijaza kwenye chupa japo chupa haikujaa. Nikachukua chupa yangu yenye double punch nikatembea nayo kama nimeshika maji vile mpaka club.

Kuingia club huku nailambalamba ile double punch nikakutana na demu mmoja wa mtaani anaitwa Judy tumecheza ile ya kukaribiana zero distance, yule demu akaniuliza wewe umekunywa nini mbona mdomo wako unanukia kama nanasi.
Mimi bila wasiwasi nikamwambia kilichomo kwenye chupa. Kama masikhara yule demu akaniomba aonje akapiga pafu ndefu kama maji huku anajifanya analalamika kali.
Baada ya sekunde kadhaa akachangamka ile sio kama mwanzo huku anayumba kwa mbali mara anivute, anikalie full vibe.

Mda kidogo kupita Judy akiwa bado na vibe akainga'ng'ania ile chupa yenye vitu hapo ikiwa imebaki kama robo ( chupa ilikuwa ya lita moja) akainywa tena kwa fujo baada ya nusu saa zile mbwembwe zote zikaisha akatulia kimya kama kalala yupo kama hajielewi hivi sio yule wa saa moja nyuma. Baada ya mda kidogo tukiwa tumekaa wote kwenye kochi moja nikahisi tofauti kumcheki vizuri nakuta demu kajichafua kote.
Nikaona hapa ishakua soo nikapotea fasta yale maeneo, kumbe kuna wahuni huku nyuma sijui waliusoma mchezo walichomfanya kwenye vyoo vya club ni zaidi ya aibu....

Kesho yake asubuhi saa 3 kasoro nakuta polisi hawa hapa nikapokelewa na vibao na matusi mpaka kwenye difenda nilipigwa sana polisi.
Kumbe kule hospital demu ananitaja mimi tu huku analia vibaya mno

Ni kesi ya kipumbavu iliyosababisha familia irudi nyuma sana kimaisha na ndo mara yangu ya kwanza kulala lockup tena nikiwa na miaka 17 tu kwa siku 9 sitegemei kama itajirudia tena

Namshukuru sana mshua wangu kwa busara, weledi na ujasiri wake bila yeye sijui ingekuwaje!

I'm sorry Judy japo sijawahi kukuona tena

Judy wako yupo Moro nowadays analewa daily
 
Kipindi tupo form 6 mwanzo mwanzo kabisa kama wadau,washikaj tulioshibana tuliamua kutafuta chumba ambacho kitakuwa karibu na shule ili tusipate hadha ya kugombania daladala asubuh kila siku.

Kweli tukatafuta na hatimae tulipata chumba mita 500 kufika shule. Tukalipia maisha yakaanza.

Sasa tulikaa kama miezi 3 hivi na mitikasi ya shule mara umeingia hapa mara pale lazima uwe na mademu, Na sis advance tulikuwa tunawakula sana o level .

Basi tunachukua videmu vya shule tunaenda kuvikula geto, na vyenyewe vinanogewa vinazoea, vikifika shulen vinawahadithia wenzao. Kwahyo pale shuleni geto letu lilipata umaarufu mkubwa sana ikafikia hatua mpaka walimu wakajua ila tu hawakuamua kulivalia njuga.

Sasa miezi 2 kabla ya necta shule kunakuwa hakuna mpya kila mtu anasongoka kivyake kwa hiyo kwa sisi wa geto swala la kwenda shule lilikuwa ni kujiamulia tu unajikuta week nzima uko geto tu.

Sasa kilichofanya nijute kama muandishi "kuna mshikaji fulan pale shule alikuwa maarufu sana Coz alisoma pale since o level.

Huyu jamaa alikuja kutuomba aje akae geto kwa kwa miezi iliyobaki Baadhi tukamkubalia ila kuna mwana mmoja alitupinga kwa uamuzi tuliouchukua.

Basi siku 2 baada ya kumaliza pepa ya practical siku hyo tumelala mpaka saa 3 asubuhi tukaamua siku hiyo tusiende shule. Ila mim na jamaa yangu tukajadiliana tukasema tuende saa 4. Ilivyofika saa 4 haoo shule.

Tumefika shule ulizia mazingira jamaa wakasema hakukuwa na jipya ila kuna jamaa akatuambia walipewa pepa ya prac. Ah bas jama yang akaniashauri turudi geto nikawa nakaza kumbe machale yalikuwa yananicheza ila napotezea. Basi mwisho wa siku nikakubali tukarudi geto.

Sasa kumbe yule jamaa tuliyemkaribisha mama yake alikuja shule kwaajili ya kesi ya mdogo wake ambaye alikuwa ni kiongozi pale shule, sasa baadae akamuulizia yule mshikaj ikabid atoke MP mmoja ambaye alikuwa mnoko kinoma kwenda kumfata class.

Amefika madarasa ya form 5 karibu na vimbweta akakutana na karatasi ya mtihani wa jamaa inagaragara chini ikabidi auokote akawa anakuja nao darasani kwetu, kabla hajafika darasani kwetu akakutana na dogo fulan wa o level ambaye ni rafiki wa mdogo wake na mshikaji. Ikabidi amuulizie, yule dogo akamjibu yupo geto.

Yule MP hakuja tena darasani akarudi staff kuwapanga wenzake[emoji23][emoji23] wakamchukua yule dogo wakampandisha kwenye ndinga haooo mpaka get. Ila kabla hawajafika geto wakakutana na mshikaji mwenyewe ndo alikuwa anakuja skonga so wakamkamata kirahisi sana. Then wakamwambia awalete geto jamaa alivyokuwa boya akawaleta kweli[emoji23][emoji23]

Ile nyumba, tuliyokuwa tunakaa kulikuwa na geti kubwa na kigeti kidogo, sisi wengine tulikuwa geto jamaa yangu mmoja ni Artist mzuri tu yeye alikuwa anachora picha ya messi namim nakula ngoma taratiib[emoji16][emoji16] kuna jamaa yetu mmoja hivi mkurya yeye mda wote alikuwa kajichimbia maeneo anakula msuli. Na kuna jamaa mwingine alikuwa anadeki choo[emoji23][emoji23] basi hivyo ndo tulivyokamatwa.

Noo kuvaa sare ya shule ni kupakia ndinga na kwenda shule, tumefika kama mita 100 hivi kabla ya kufika shule kilianza kichurachura mpaka shule tumefika shule tulikula doso kali sana kiasi cha kujuta na kutosahau(kama mnavyojua wanajeshi wakisulubu)

Kutokea saa6 tumekuja kuachiwa saa 11 jioni wakati tunapewa vifaa vya kung'olea visiki na kuchimba shimo[emoji23][emoji23]

Nisiku ambayo nilijuta kupuuzia hisia zangu[emoji120][emoji120]
Hii sio jiteute kweli kwa akina afande mrocky na nziku?
 
kiukweli kuna mtu najuta mno kumfanya rafiki, sina wa kumsimulia kisa changu maana hii siri nitakufa nayo mwenyewe, lakini najuta mno kumfanya rafiki na sina namna ya kumuacha na kumuweka mbali lakini pia sina namna ya kumkimbia..

Mola wangu wa mbinguni nisamehe mimi siyapendi haya na yananigharimu mno kwenye maisha yangu..
HAKUNA lisilowezekana chini ya jua...

Akikushinda kwa nguvu ..wewe mtege kwa nyavu..hata Kama ita kuchukua miaka...

Unaishi maisha gani mkuu hayo?!
 
Miakankadhaa nyuma... mida ya jioni niko na wanangu tunazurul tu mtaani ghafla mwana anasema tupite home kwao kidogo kuna nshu kasahau then tuendelee misele kukagua mitaa...

Kwao geti kali wana walinzi wamasai na nini... tumekaa zetu ubarazani tunamsubiri mwana atoke ndani tusepe huku tunapiga story na masai mlinzi..

Story zikiendelea ghafla masai anatoa kichupa kina unga mweusi amaweka mdomoni tunamuukiza oya nini hiyo unaweka mdomoni Masai anasema chkua weka na ww rafiki utafurahi...

daaah sitakuja kisahau hii siku asee since that day i hv been addicted to snuff na inanikwamisha mambo kibao yani...

Hii mambo ya kujaribu jaribu kila kitu sio poa... unaweza haribu future yako yako yote kifala sana
 
Ukila single mother kesho yake akikupigia anakwambia msalimie mwanao.
True na huyu bibie alikuwa kila akinipigia simu anataka nisalimie wajukuu zake...alikuwa ananichosha sana kwa kulazimisha mapenzi yasiyokuwepo
 
Miakankadhaa nyuma... mida ya jioni niko na wanangu tunazurul tu mtaani ghafla mwana anasema tupite home kwao kidogo kuna nshu kasahau then tuendelee misele kukagua mitaa...

Kwao geti kali wana walinzi wamasai na nini... tumekaa zetu ubarazani tunamsubiri mwana atoke ndani tusepe huku tunapiga story na masai mlinzi..

Story zikiendelea ghafla masai anatoa kichupa kina unga mweusi amaweka mdomoni tunamuukiza oya nini hiyo unaweka mdomoni Masai anasema chkua weka na ww rafiki utafurahi...

daaah sitakuja kisahau hii siku asee since that day i hv been addicted to snuff na inanikwamisha mambo kibao yani...

Hii mambo ya kujaribu jaribu kila kitu sio poa... unaweza haribu future yako yako yote kifala sana
Ngada,Ugolo na sigara wanasema ukijaribu huachi,kaa mbali navyo
 
NAIROBI

Kipindi fulani nimepata mchongo Nairobi, Kenya.

Kwenye kampuni moja hivi inajihusisha na mauzo ya mfumo fulani wa Computer [Sitasema ni System gani].

Mfumo ulikua umekamilika kisawasawa kulingana na namna ulivyokua unafanya kazi katika kutimiza mahitaji ya wateja. Kwaiyo bei yake ilikua imechangamka kidogo lakini makampuni yalilipia bila shida kwa sababu ya namna ambavyo mfumo uliwarahisishia kazi.

Sasa huo mfumo ulikua una ada zake za kila mwaka (annual subscriptions fees) ambazo nazo ni kubwa kidgo kwa wale wateja ambao bado wanaendelea kutumia huo mfumo. Ila kwa wale ambao wameshindwa kulipia, mfumo unafungwa (license ina expire) hadi watakapolipia tena.

Mimi na Jamaa yangu mmoja tukaona fursa kwa wale ambao wanashindwa kuendelea kutumia mfumo kwa sababu ya gharama zake kuwa kubwa. Tukaingia mzigoni kucheza na lile file la license (lilikua limesukwa na lugha ya Delphi) mpaka tukafanikiwa kujua namna ya kulichezesha ili mfumo uendelee kufanya kazi. NB: Hiki sio kitu kizuri, Usijaribu utafungwa!

Kampuni ilikua ina milikiwa na wazungu, kwaiyo sisi tunatumwa kufanya marketing, installations na trainings kwa wateja. Pia tulikua tunafanya support kwa wale wanaokutana na changamoto za mfumo hata baada ya kuanza kuutumia. Kwaiyo tulikua tunajua A2Z ya wateja wote ambao tulikua tunafanya nao kazi vizuri.

Sasa basi, baaada ya kufanikiwa kucheza (crack) na license file, tukaanza kuwa approach kimya kimya wateja waliokua wanatumia mfumo halafu wakashindwa kuendelea nao na kuwapa offer ya punguzo la bei na namna wanavyotakiwa kufanya malipo (tukabadilisha hadi zile payments methods, mpunga uwe unaingia kwetu). Duh, ujanja ujanja sio kitu kizuri ila anyway I have learnt my lessons!

Sio siri jamaa walikua wanatulipa vizuri sana plus allowance za kukidhi mahitaji ila ndoivo tamaa haina aibu. Tukaanza kupiga hela, chezea discount wewe! Wateja wote waliokua wamekufa wakafufuka na mtonyo tukawa tunapokea sisi. Si tukajisahau...asalaaaaleee. Siku moja mteja mmoja akawa amekwama kufanya kitu kwenye mfumo sasa ile kututafuta mimi sikua online, jamaa yangu naye alikua anakula bata kama kawaida yake maana illikua ni siku ya jumapili kama leo. Heheee

Saa ngapi yule mteja asitafute contacts za mzungu aanze kuwasiliana naye na wakati sisi tulisha update taarifa zake kwenye mfumo wa CRM kuwa ni Dead Customer. Si akafunguka kuwa alikua anatumia mfumo toka kitambo tu na alikua anawasiliana na sisi...duuuh

Wazungu wakatusubiri Juma3 Ofisini. Hatuna hili wala lile. Tuko na hangover zetu. Kwa namna salamu zilivyokua zinapokelewa ofisini na namna tulivyokua tunapewa zile weird looks nikajua kuna kitu hakiko sawa hapa. Machale yakanicheza kidgo lakini haikusaidia.

Nikashangaa mimi na jamaa tu ndio tunaitwa kwenye kikao cha dharura. Duuuh tukavuliwa nguo vibaya sana. Heshima yote tuliyokua tumejijengea ofisini pale ikayeyuka yooote! Kumbe hadi emails zimeshatumwa kwa wateja wote kuwa sisi sio wafanyakazi wa pale tena, sisi hata hatujui. Kumbe tumeshatolewa kila mahali wafanyakazi wote wanajua hata hatuelewi.

Tukanyang'anywa kila kitu cha ofisi. Kazi hakuna. Nikapewa siku mbili tu za kubaki kwa kenyatta zaidi ya hapo nikionekana nadhurura ni ndani. Na hiyo pia ni kama favor tu nilipewa maana wangeamua kwenda mahakamani ilikua ni ndani moja kwa moja.

Dah niliteseka sana baada ya hapo. Kwa sababu connections zote nilizokua nazo zilikua zinatokana na kazi za hao jamaa na wameshachafua hali ya hewa kila mahali. Nilisota sana kupata kazi nyingine.

Kuna kipindi nikaanza kukumbuka maisha niliyokua naishi pale Ruaka Dah.. Nikawa najuta sana. Nikaweka nadhiri rasmi sitakaa nijihusishe na illegals tena!

Na hilo likawa funzo langu!
Mkuu unaonekana una vielement vya kutaka upate kiurahisi au utapeli kabisa maana ukianzia na payslip za kufoji ukiwa chuo na ukajuta hutakuja kufanya mishe nyeusi na ukarudia tena, wewe sio wa mazoea Kwa pesa unabadirika muda wowote
 
Part 2

Siku ile baada ya kudhurumiwa niliumia saana sana hasa kwa kuwa hela haikuwa yangu pia hali ya uchumi mtaani kugumu. Basi bwana, kufika jioni dogo akanichek kupata mrejesho wa betri lake, ikabidi nimwambie yule jamaa kafunga kaenda msibani so atarud after siku tatu na kununua sehemu nyingine ni bei sana. Nashukuru dogo alinielewa japo kishingo upande.

Ishu ya kudhurumiwa iliniima saana sanaa sana ilifika kipindi nipo busy na mambo mengine lakini moyoni unakuwa kama kuna kitu hvi hakiko sawa ukikumbuka unagundua hela yako imeenda kiboya. Hivo nkapanga mikakati narudishaje pesa yangu niliyodhurumiwa hadi kwa wakati ule usiku sikujua nn ntafanya.

Kesho yake mchana nkapada gari hadi pale pale kwa wachezesha bahati nasibu, lengo lilikuwa niende nisome mazingira tena nimezurumiwaje kiboya vile tena laki. Laki yangu ilikuwa inaniuma kinoma na isitoshe nimemdanganya dogo so baada ya siku tatu anategemea nimtumie betri lake na isitoshe dogo ananiamini kinoma.nilishukia kituo kinaitwa pamba road sheli. Mdogo mdogo hadi pale kufika tu pale nkasimama kuchek wahusika nkakuta yule mdada aliyeshinda begi ndo anagawa tiket yule niliyechanga nae hela ni msaidizi ndo nkagundua huu ni mchezo hakuna bahati nasibu wala nini hapa, kuwaona pale kichwa kikazidi kujaa sumu. Wale watu bhana kumbe wana mabaunsa nkaona hapa nkileta fujo ntajikuta nipo polisi so nikawa mpole. Sasa kumbe yule mdada tuliyechanga nae hela alinijua akasema kwa nguvu "kuna wengine wamerudi kufanya fujo baada ya kuliwa jana" basi mabaunsa wakaja wakanifukuza baada ya kuoneshwa kuwa ni mimi na isitoshe ni kweli jana nilitaka kufanya fujo baada ya kudhurumiwa. Nkajua hapa kitumbua kishaingia mchanga, wakanifukuza pale nkatoka lakini nikawa najua mchawi wangu ni yupi ni yule dada aliyenichongea kwa mabaunsa.

Nkatoka pale nmejaa sumu kinoma, nkaenda zangu kamanga "Bismark rock" kuna kabustani pale kwa wenyeji wa mwanza washapafahamu, nkalipia jero nkakakaa kwenye nyasi napunga upepo wa ziwa huku natafakari nini cha kufanya.

Kichwani likaja wazo nilisema nipambane nao siwawezi kwanza wana mabaunsa, niende polisi siwezi, inamaana polisi hawajui kuwa hawa jamaa ni matapeli? Nkajisemea hapa nadeal na huyu mdada aliyenichongea anajifanya mwema kumbe ni snichi. Sasa ikawa muda wa kupanga mikakati namna ya kurudisha pesa yangu.

Njia ya kwanza nkawaza nimvamie nimnyang'anye simu na hela nkaona ntaitiwa mwizi nkasema hapa lazima nijue anakaa wapi kwanza ndipo mambo mengine yaendelee.

Sasa baada ya kurudi home ilikuwa mwanzo wa mwezi na mimi ndo nakusanya hela ya maji, tunapokaa tupo wapangaji wengi kidogo, nkakusanya hela ya maji kama laki na 30 hvi nkaenda kulipa 60 na 70 nkanunua betri la dogo nkamtumia. Nkachonga na jamaa anaekujaga kukata maji kama hujamaliza deni coz tulikuwa tunafahamiana nae kiasi na namba zake nilikua nazo coz kuna msala ashawahi nisaidia, nkamuahidi baada ya wiki mbili hvi ntakuwa nshamaliza deni so likitokea lolote anisitiri coz wapangaji wenzangu wanajua bill ishalipwa yote.

Nkapanga mikakati, mkakati wa kwaza ni kubadili mwonekano ili nikirudi pale nisijulikane kirahisi, hivo nilienda kunyoa nyele zoote na ndevu yaani full para coz nilikua na nyele ndefu na madevu mengi. Kiukweli nilibadilika saana hadi demu wangu alisema hajazoea kuniona vile, pia washkaji wengine walinisahau kabisa, nilifanya hvi ili nisigundulike hata nikimfatilia yule dada anapokaa hata tukipanda daladala moja asihisi chochote.

Katika maisha mimi huwa naamini kuwa tunaishi mara moja tu so ninachoamini, jambo likiumiza kama umeamua kusamehe basi samehe kama kulipiza kisasi, lipiza coz maisha ni kma maji yanayo toka mlimani kwenda bondeni yakipita hayarudi tena kwa kifupi tunaishi mara moja tu, punguza majuto katika maisha. falsafa hii ndio chanzo cha kujiita "MTAMAUSHI" kwa waliosoma somo la kiswahili vizuri levo ya chuo na advance wanaelewa nini maana ya falsaha hii ya ndugu E kezilahabi kma sijakosea.

Tuachane na falsafa, baada ya kubadili mwonekano nkarudi tena pale pale kwa wanapochezesha bahati nasibu lakini awamu hii nilirudi jioni saa 10:30. Nilikaa pembeni kidogo walikua wanakaanga chipsi, nkaagiza chipsi na soda nikawa nakula taratibu nkivizia wafunge. Baada ya kumaliza kula nkaagiza soda nyingine nkaanza kunywa taratibu, kweli bhana saa 11: 30 hvi wakawa wamefunga wanakusanya kila kitu pale wakakutana pembeni kama kimduala hvi wakagawana hela ndo nilipojua kumbe wanapiga mkwanja mrefu. Hela alikuwa anagawa kiongozi wao, baada ya kugawana wakaanza kusepa wengine kwenye gari lililobeba vyombo wengine kwa miguu, target yangu ilikua ni yuje mdada tu. Akatoka pale mdogo mdogo akaingia sokoni mimi nyuma yake ila kwa mbali na umakini mkubwa sana asijue lolote. Yule dada alinunua vitu vichache pele akaenda kupanda gari. Baada ya kufika kwenye gari alikaa siti ya mbele kwa dereva nilichofurahi ni kwamba alikuwa kumbe anakaa njia ambayo namimi naishi huko hvo alinipunguzia garama ya usafiri coz niliapa kokote anakokaa nitamfata tu. Basi bhana baada ya abiria kujaa nkajisogeza pale nikakaa ndani ya daladala gari likaondoka likapita kituo ninachoshukiaga mimi hadi kama vituo 5 mbele yule dada akashuka. mimi sikushuka, gari lilipoanza kuondoka limetembea mita chache nkamwambia konda anishushe nilikua nimejisahau kweli nilishushwa ila kwa matusi na misonyo kibao ya konda kwamba sipo makini kumbe nilipanga iwe hvo. Baada ya kushuka tu nilianza kwenda kituoni kumchek yule dada, nikamwona kwa mbali anatembea. Nilikua nmevaa sweta jeusi nikavua nkabaki na shati tu nilifanya hvo asikumbuke kama tumepanda wote daladala kama aliniona. nilimfatilia hadi anapokaa nkapajua uzuri nyumba ilikua imejitenda kidogo na njia ina kichaka na uchochoro kidogo.

Baada ya kujua anapokaa nilirudi zangu geto kusubiri nifanye revange yangu, baada ya siku kadhaa saa 12:00 nipo kituoni namsubiri mfukoni nina bonge la panga. Saa moja na dk kadhaa nkamwona kashuka nikatangulia mbele coz yeye alipita kununua mhindi choma pale standi. Kwa wakati ule nilikua nakumbuka ile kauli yake ya "kuna wengine wamerudi kufanya fujo baada ya kuliwa" hii kauli iliniuma sana. Sikuwa na lengo la kumdhuru ila tu nirudishe hela yangu tu.

Baada ya kutangulia mbele nnkaanza kutudi nilikotoka tukakutana jiani nkachomoa panga. Nkamwambia naomba hela zangu, akauliza hela ipi? nilimpa ubapa wa mgongoni nkamwambia ukipiga kelele umekwisha, alitetemeka yule dada sijapata ona. nkamwambia leo nimekufata na huku mnapenda kudhurumu watu mbwa nyie. lete mkoba akawa anabisha nkampa bapa la pili akaachia nkazama kwenye mkona nkatoa simu na hela nkasepa zangu mbio uchochoroni nkamwacha anali na isitoshe watu hawakuwepo .Njiani nkadaka boda hadi karibu na geto nkashuka. Nilipofika home kuhesabu nkakuta hela kma 70 hvi simu, nkawafata wahuni kesho yake nkawauzia kama 50 ilikua smartphone. Nkalipa deni la maji na usumbufu.

Inayofuata:
Fema club walisababisha nikamatwe na bro nikiwa napiga punyeto kisa ile kauli yao ya punyeto ni njia salama, ntawalete kisa soon
Sasa broo si ungeendeleza tu hicho kipaji maana sio kazi rahisi kumtembezea bapa za panga binadamu hata kama unalipa kisasi inatakiwa ujasiri wa hali ya juu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Inavyoonekana una hako kakipaji ulipaswa uanzishe kijiwe cha kukaba ungetoboa fasta tu
 
Mkuu unaonekana una vielement vya kutaka upate kiurahisi au utapeli kabisa maana ukianzia na payslip za kufoji ukiwa chuo na ukajuta hutakuja kufanya mishe nyeusi na ukarudia tena, wewe sio wa mazoea Kwa pesa unabadirika muda wowote
Na ndio mwanaume unapaswa kuwa hvo mkuu.
 
Mkuu unaonekana una vielement vya kutaka upate kiurahisi au utapeli kabisa maana ukianzia na payslip za kufoji ukiwa chuo na ukajuta hutakuja kufanya mishe nyeusi na ukarudia tena, wewe sio wa mazoea Kwa pesa unabadirika muda wowote
Kila anayeishi anapenda urahisi. Unadhani ungepewa uwezo wa kubadilisha maisha yako kwa ku.click vidole vyako viwili usingefanya hivyo?

Unajua kwanini vijana wengi wanaingia ki rahisi kwenye Betting? Forex? Au kwanini watu wengi walizama kirahisi kwenye Forever Living? Four Corners? Global Alliance? DU? ... Ni for obvious reason, kupata mafanikio kirahisi!

Je ni wapumbavu kwa kufanya hivyo hadi wengine wakaishia kutapeliwa na kupoteza pesa zao huko? Hapana, sio wapumbavu, bali ni Binadamu, na akili zetu zimesukwa ili kutulinda sisi tusiteseke. Kwaiyo inapotokea njia mbili mbele na moja ikaonekana ni ngumu, automatically lazima tupite ile rahisi (shortcuts).

So yes, anyday kwenye haya maisha nitachagua an easy way out ikiji present mbele yangu. But saivi nitachagua kwa umakini zaidi kwa kuzingatia mambo mengi ya ki usalama (kisheria). Kama wewe unadhani you can make it in this life by playing too safe, good luck with that.
 
Ila ndio wanaume inapaswa tuwe hivo, unacheza na fursa tu.
 
BETTING

Waliotutangulia huku duniani waliandika kuwa betting au uwekezaji kwa lugha ya kibiashara dunia ya leo sio kitu cha kutegemea ki uchumi kwa sababu hakitabiriki na huwezi kuwa master katika career hii. Hivyo basi ni muhimu kutafuta kazi inayotumia skills ambayo unaweza kui master kwenye kutafuta pesa kuliko kutegemea mambo ya kubahatisha.

Looh, sikuwahi kuelewa walimaanisha nini kwa kipindi kile. Japo nilikuja kuelewa in a hard way!

Miaka kadhaa nyuma, wakati mambo ya kubet yameanza kutaradadi nakumbuka kulikua na vi ofisi flan town ukipita unakuta watu wamejazana huko hadi wameunga foleni ukichungulia kwa ndani unaona maandishi yanayo wakawaka yanapita kwa juu hata huelewi ni nini. Una amua kuuliza unaambiwa watu wanacheza kamari. Duh, kusikia kamari unachanja mbuga maana kwa wakati ule neno "kamari" lilikua linaogopesha sana sio kama saivi.

Basi bhana, nikawa naishia tu kuangalia kwa mbali. Miaka ikasonga, betting ikazidi kukuwa, makampuni yakaanza kuongezeka, mpaka ikafika mahali karibu kila siku nikiwa kwenye mgahawa nakunywa chai siachi kuona washkaji wana vikaratasi vyeupe virefu (nilikuja kujua baadae sana vinaitwa mikeka).

Punde si punde nikaanza kusikia story za fulani kavunja Milioni kadhaa, fulani kavunja laki kadhaa, Daah. Katamaa kakaanza ku beep kwa mbali. Nikasema kwani nini mbaya kujua hii michezo inachezwaje acha niulize kidogo.

Mwana akanielewesha kuhusu hiyo michezo sema binafsi nikawa interested zaidi na betting ya soccer. Kwa sababu niliona ina uwazi. Mpira hauna longolongo, timu ikishinda kila mtu anajua kwa hiyo si rahisi kutapeliwa.

Muda ukaenda, story za watu kuvunja hela zikawa zinazidi kuwa nyingi. Ikafika mahali nikawa kama naanza kujiskia vibaya. Naona kama ni mimi peke yangu tu ndio nimebaki sina hela. Walivyokuja Meridian na system yao ya online betting, dah nikajikuta na mimi nimo ndani.

Duuh, kumbe nilikua natamani kubet sema nilikua naona aibu kuonekana hadharani. Sasa hii ya online najua hakuna mtu anaweza kunisanukia kama nacheza hata nikishinda ni siri yangu. Heheee! Sijawahi kushinda kitu! Hata mia! Kwaiyo maumivu yakawa ni ndani kwa ndani.

Betting ina addiction mbaya sana. Unaanza kujua umesha athirika na Betting pale tu unapoanza ku chase loss. Yani unapoanza kuweka hela haraka haraka ili kurudisha pesa uliyopoteza. Nakumbuka kuna kipindi nilikua hadi nakopa pesa nabetia na inaliwa yote. Pesa ya kodi nabetia inaondoka yote. Kila mahali ni madeni. Halafu kibaya zaidi hata nikipokea hela kidogo kazini naona uzito kwenye kulipa yale madeni napata wazo la kuweka mkeka hata wenye odds 4 tu ili pesa ijae nimalize madeni yote kwa mara moja lakini wapi. Yote imeenda na maji. Nikawa depressed!

Walioniamini na kunikopesha wakaanza kuniona mtu wa ajabu sana, nafanya kazi napokea hela, silipi madeni ya watu kwa makusudi. Kumbe hela yenyewe ya kazi inaishia kwenye mikeka. Baadhi ya wadeni wangu wakachoshwa na sound zangu, wakaji organize wakaja ghetto wakabeba vitu hadi simu yangu wakapita nayo na bado wakanipa tarehe ya kumalizia madeni yaliyobaki la sivyo watanishtaki hadi kazini. Dah mambo ya aibu!

Nikaapa naacha kubet rasmi. Of course bado nilikua nataka kuendelea sema hata simu ya kubetia nilishanyang'anywa, na kwenda vibandani siwezi maana nafanya kwa siri. Nikapiga kazi mpaka nikamaliza madeni yote kwa kipindi kirefu sana. Na ki ukweli hakuna kitu kilikua kinaniumiza kama kulipia madeni ambayo sijafanyia kitu. Bora hata zile hela nilizokopa ningekua nimekula. Zote zilipotelea huko kwenye mikeka!

Muda ukaenda mpaka nikafanikiwa kununua simu nyingine ya smartphone. Siku moja napitapita huko Instagram, mara pap nakutana na mtu kashika bango la milioni 30 za Sportpesa, Daah vinyweleo vikasimama tena!

Nikasoma soma comments nikaona kama kila mtu anampa hongera nikaona hawa jamaa watakua legits, nikasahau yaliyonikuta huko nyuma nikaona nijiunge nao chap. Walikua na mchezo wao mmoja wanaita Jackpot, ukikosea mechi kidgo katika zote 13 wanakupa hela. Sa ngapi nisijaribu niotee 12. Duh Milion 10 na ushee hizi hapa. Nikaona kama ni utani.

Mara jamaa wakanipigia simu wakaniambia niende ofisini kwao wakahakiki taarifa zangu wanipe mpunga. Kweli nikafika nikamalizana nao, mpunga ukaingia kwenye account. Nikasema dah, elf mbili tu imenipa Mita 10. Maisha si ndio haya. Heheee.

Kilichonikuta na hizo Mil 10 ni story for another day!
 
BETTING

Waliotutangulia huku duniani waliandika kuwa betting au uwekezaji kwa lugha ya kibiashara dunia ya leo sio kitu cha kutegemea ki uchumi kwa sababu hakitabiriki na huwezi kuwa master katika career hii. Hivyo basi ni muhimu kutafuta kazi inayotumia skills ambayo unaweza kui master kwenye kutafuta pesa kuliko kutegemea mambo ya kubahatisha.

Looh, sikuwahi kuelewa walimaanisha nini kwa kipindi kile. Japo nilikuja kuelewa in a hard way!

Miaka kadhaa nyuma, wakati mambo ya kubet yameanza kutaradadi nakumbuka kulikua na vi ofisi flan town ukipita unakuta watu wamejazana huko hadi wameunga foleni ukichungulia kwa ndani unaona maandishi yanayo wakawaka yanapita kwa juu hata huelewi ni nini. Una amua kuuliza unaambiwa watu wanacheza kamari. Duh, kusikia kamari unachanja mbuga maana kwa wakati ule neno "kamari" lilikua linaogopesha sana sio kama saivi.

Basi bhana, nikawa naishia tu kuangalia kwa mbali. Miaka ikasonga, betting ikazidi kukuwa, makampuni yakaanza kuongezeka, mpaka ikafika mahali karibu kila siku nikiwa kwenye mgahawa nakunywa chai siachi kuona washkaji wana vikaratasi vyeupe virefu (nilikuja kujua baadae sana vinaitwa mikeka).

Punde si punde nikaanza kusikia story za fulani kavunja Milioni kadhaa, fulani kavunja laki kadhaa, Daah. Katamaa kakaanza ku beep kwa mbali. Nikasema kwani nini mbaya kujua hii michezo inachezwaje acha niulize kidogo.

Mwana akanielewesha kuhusu hiyo michezo sema binafsi nikawa interested zaidi na betting ya soccer. Kwa sababu niliona ina uwazi. Mpira hauna longolongo, timu ikishinda kila mtu anajua kwa hiyo si rahisi kutapeliwa.

Muda ukaenda, story za watu kuvunja hela zikawa zinazidi kuwa nyingi. Ikafika mahali nikawa kama naanza kujiskia vibaya. Naona kama ni mimi peke yangu tu ndio nimebaki sina hela. Walivyokuja Meridian na system yao ya online betting, dah nikajikuta na mimi nimo ndani.

Duuh, kumbe nilikua natamani kubet sema nilikua naona aibu kuonekana hadharani. Sasa hii ya online najua hakuna mtu anaweza kunisanukia kama nacheza hata nikishinda ni siri yangu. Heheee! Sijawahi kushinda kitu! Hata mia! Kwaiyo maumivu yakawa ni ndani kwa ndani.

Betting ina addiction mbaya sana. Kwenye Bettng unajua umeanza kuwa addicted pale tu unapoanza ku chase loss. Yani pale unapoanza kuweka hela haraka haraka ili kurudisha pesa uliyopoteza. Nakumbuka kuna kipindi nilikua hadi nakopa pesa nabetia na inaliwa yote. Pesa ya kodi nabetia inaondoka yote. Kila mahali ni madeni. Halafu kibaya zaidi hata nikipokea hela kidogo kazini naona uzito kwenye kulipa yale madeni napata wazo la kuweka mkeka hata wenye odds 4 tu ili pesa ijae nimalize madeni yote kwa mara moja lakini wapi. Yote imeenda na maji. Nikawa depressed!

Walioniamini na kunikopesha wakaanza kuniona mtu wa ajabu sana, nafanya kazi napokea hela, silipi madeni ya watu kwa makusudi. Kumbe hela yenyewe ya kazi inaishia kwenye mikeka. Baadhi ya wadeni wangu wakachoshwa na sound zangu, wakaji organize wakaja ghetto wakabeba vitu hadi simu yangu wakapita nayo na bado wakanipa tarehe ya kumalizia madeni yaliyobaki la sivyo watanishtaki hadi kazini. Dah mambo ya aibu!

Nikaapa naacha kubet rasmi. Of course bado nilikua nataka kuendelea sema hata simu ya kubetia nilishanyang'anywa, na kwenda vibandani siwezi maana nafanya kwa siri. Nikapiga kazi mpaka nikamaliza madeni yote kwa kipindi kirefu sana. Na ki ukweli hakuna kitu kilikua kinaniumiza kama kulipia madeni ambayo sijafanyia kitu. Bora hata zile hela nilizokopa ningekua nimekula. Zote zilipotelea huko kwenye mikeka!

Muda ukaenda mpaka nikafanikiwa kununua simu nyingine ya smartphone. Siku moja napitapita huko Instagram, mara pap nakutana na mtu kashika bango la milioni 30 za Sportpesa, Daah vinyweleo vikasimama tena!

Nikasoma soma comments nikaona kama kila mtu anampa hongera nikaona hawa jamaa watakua legits, nikasahau yaliyonikuta huko nyuma nikaona nijiunge nao chap. Walikua na mchezo wao mmoja wanaita Jackpot, ukikosea mechi kidgo katika zote 13 wanakupa hela. Sa ngapi nisijaribu niotee 12. Duh Milion 10 na ushee hizi hapa. Nikaona kama ni utani. Mara jamaa wakanipigia simu wakaniambia niende ofisini kwao wakahakiki taarifa zangu wanipe mpunga. Kweli nikafika nikamalozana nao, mpunga ukaingia kwenye account. Nikasema dah, elf mbili tu imenipa Mita 10. Maisha s ndio haya. Heheee

Kilichonikuta na hizo Mil 10 ni story for another day!

Mkuu malizia[emoji23]visa vyako vinakuaga noma sana
 
Back
Top Bottom