Kisa kukosa license kunavyofanya nikose ajira kwenye taasisi

Kisa kukosa license kunavyofanya nikose ajira kwenye taasisi

Mirror 14

Member
Joined
Feb 18, 2023
Posts
11
Reaction score
10
Wakuu mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 nina elimu ya sekondari kidato cha nne

Nilihitimu 2017 lakini sikubahatika kuendelea na elimu ya advance, mimi ni mkubwa kwenye familia ya watoto wanne

Dhumni la kuja kwenu, ninaomba mwenye uwezo wa kunichangia japo chochote ili niweze jiendeleza na elimu ya veta ili nipate license

Kwani nimekua nikijishughulisha na ajira ambayo mwisho wa mwezi ninapata malipo ya 130,000

Ambayo yote hua inaishia kuhudumia wadogo zangu kwa chakula na nauli za kila siku za kwenda shule,

Na kushindwa na kubaki na chochote kwani familia yetu ipo na mama tu baba ameshaitelekeza familia mwaka wa nne sasa

Wakuu naombeni mnichangie japo nijiendeleze nipate license maana kuna taasisi iliniahidi nikipata license itaniajiri na kunilipa 450,000 kila mwezi

Nimejaribu kukopa sehemu mbalimbali lakini watu wanakosa kuniamini kutokana sina kipato cha kuwarejeshea pesa yao pia nimejaribu kwa baadhi ya ndugu waniendeleze lakini baadhi wananiahidi tu mwaka wa pili sasa bila kutimiza ahadi zao

Naombeni member wenzangu mwenye chochote aweze kunichangia ili namimi niweze kujiondoa kwenye hili dimbwi la umasikini,kwani ninaamini humu jf kuna watu wema tu watakaoweza kuguswa

Kiasi cha kusoma veta na kupata license ni shilingi 280,000, nichangieni ndugu zangu maana option niliobakiza ni hii tu maana mtu wa taasisi aliyeniahidi kazi ameniambia anataka aende kujiendeleza na masomo sasa ni muda mrefu sijapata license ambacho ndio kigezo cha kuajiliwa,hivyo akienda masomoni nitakosa tena tumaini la kupata kazi kwenye hiyo taasisi

Natanguliza shukrani kwa yeyote aliyeguswa kwa namna yeyote ile japo si kwa kunitumia pesa 🙏🙏

Namba ya kunichangia ni

0678265762
 
pole sana kwa majukumu ingali upo kijana mdogo, ndo ukubwa huo

Huwa sipendi sana ndugu ambao hua wanaahidi na kushindwa kutekeleza wanasahau wanajitengenezea mikosi maana unamuacha mtu anasonona moyoni
 
pole sana kwa majukumu ingali upo kijana mdogo, ndo ukubwa huo

Huwa sipendi sana ndugu ambao hua wanaahidi na kushindwa kutekeleza wanasahau wanajitengenezea mikosi maana unamuacha mtu anasonona moyoni
Asante mkuu
 
Ukitaka usaidiwe haraka weka account ya chuo-veta anaweza tokea mtu akakulipia then akakutumia Payslip (risiti) ukaipeleka chuo kuanza masomo. Ila kutoa pesa mkononi watu wagumu wanaogopa utapeli...
sawa mkuu nashukuru kwa mchango wako,,nimefanya hivo ili kama mtu anachochote aweze kunichangia maana nimeona itakua ngumu kwa mtu mmoja kuchangia yote kwa pamoja, ila nipende kukiri tu, hili swala sio utapeli kama yeyote atakavyozani.

Mawazo yako pia nimeyapokea.

Nifanye mchakato wa kupata account number ya veta niwaletee wanandugu
 
Mh sawa mkuu ila kuna kitu kama sijaelewa samahani lakini

Sijajua uko mkoa gani lakini sidhani kama kwa sasa VETA wanatoa leseni ya udereva ukimaliza masomo yao

Labda ufatilie vizuri ingawa sijajua kama uko mkoani na wanautaratibu huo.

Ila kama Dar es salaam kwa sasa unasoma ukimaliza unaanza tena process za leseni kwa gharama nyingine kabisa

Asante na niko tayari kusahihishwa.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom