Kisa nilicho kutana nacho huu mwaka katika kutafuta ajira

cold water

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2021
Posts
238
Reaction score
954
Jamani, jamani, ofisi zimetulia, majengo ni mazuri yanapendeza na kuvutia, na watu wake wanapendeza ukiwaangalia kwa nje lakini?! Lets go to the point,

Mwezi fulani hapa kati kati katika kutafuta sehemu za kujitolea nikaenda ofisi moja hivi sehemu fulani, jamani nilikutana na kaka mmoja alinipokea vizuri tu, nikampa barua yangu na CV zangu lakini alionesha kutokuridhika na nilichokiandika, ilibidi afanye kazi upya kuanzia kuandika barua hadi CV.

Tukiwa pale ofisini huku ananifanyia ile kazi huku ananilazimisha niende nyumbani kwake, na kunilazimisha kupima HIV ili niweze kumpa mzigo! Nikamkatalia, nikamwambia kaka kama hautaki kunisaidia basi naomba barua zangu niondoke watanisaidia wengine!

Akaniambia nina mda mrefu sijafanya mapenzi, mke wangu yuko mbali naomba nipunguze kidogo zimejaa! Nikamwambia mimi sihitaji, naomba barua zangu. Akaniambia kwahiyo wewe unataka mimi nikusaidie lakini wewe kunisaidia mmi hutaki?

Nikamwambia nitafanya huu mchezo kwa watu wangapi katika maofisi wakati mimi bado naendelea kutafuta kazi? Hivi ninavyowaambia barua niliziacha na sijapata hiyo nafasi ya kujitolea hadi leo.

Ofisini kwake nilienda karibu mara tatu akidai vitu havijakamilika na siku hizo zote alinidai ngono. Nilikosa furaha kila nilipokuwa nikirudi nyumbani. Basi nilivyoona miezi inakatika nikaenda sehemu nyingine, nako nilisaidiwa na kupewa hela juu, lakini nikaendelea kuombwa ngono kama kawaida.

Mtu ananiambia njoo nyumbani nifulie nguo, mara kuna kitu inabidi unitimizie, nikakataa pia. Nikaenda tena ofisi nyingine hivyo hivyo, oh dada naomba unipe nafasi, nimekuelewa sana, nakupenda, hii barua yako leo hii hii napeleka sehemu husika. Nikaipotezea tena hiyo sehemu hadi leo sijafatilia.

Nikaenda tena sehemu nyingine huyo sasa alikuwa Meneja, akaniambia njoo uripoti lakini naomba uwe na mimi, nitakufungulia na biashara pia! Ikabidi nimwambie basi nimegairi nitatafuta sehemu nyingine.

Siwachafui watu jamani huu mwaka nimepitia mikasa tu. Nimekata hadi tamaa ya kuomba kujitolea, hapo tu kujitolea vipi nikiwaambia waniajiri? Yani nimechoka kuzunguka. Namba za hawa watu zote nimezifuta, yaani ni kuniomba ngono tu hamna msaada wowote.

Nasemaje, ofisini kuna mambo! Ilishanitokea hadi kipindi cha field wababa wanaomba sana ngono maofisini, acha kabisa.
 
Huyo Dawa yake mchomeshe kwa Takukukuru, hiyo ni rushwa ya ngono anataka.

Hongera pia kwa kujitambuwa utu wako.
 
Na kwa Nn hutaki?
 
K
Kuzaliwa mrembo napo shida tupu.
 
Wadada bwana!!!! Kama una boyfriend na hamjaoana, na unamtegeshea kichupa anajisaidia, kwa Mungu hiyo ni dhambi (kama ndicho unachoogopa). So kumpa huyo jamaa wa kibaruani ni extension tu ya dhambi unayofanya na your boyfriend. Kama unaogopa magonjwa, ndo keshakwambia ukapime. Kuliko kuendelea kumpa bure boyfriend wako, achia for the first time kikulipe. Ila hakikisha kinakulipa kweli.

NB: KAMA KAWAIDA YA SIKU ZOTE, USHAURI UNAWEZA KUCHUKULIWA AU KUACHWA. HUU USHAURI NISINGEUTOA KWA MY WIFE MPENDWA
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…