Kisa wivu wa mapenzi, mume adaiwa kumuua mke kisha kumtenganisha kichwa, kiwiliwili na viungo vingine

Kanda ya Ziwa mnapokezana siku tu,Roho iliyowaingia huko sijui mmeitoa wapi?
 
duh haya matukio isije ikawa ni matokeo ya chanjo zile 😎 nawaza tu lakini
 
kama huyu ndio mzazi wangu bora nikawe omba omba kuliko kuwa ndani ya hiyo nyumba.

huwezi charanga binadamu kama kuku kiasi hicho.
 
Mtuhumiwa anajua alichopanga na mganga wake,si wivu huo. Sukuma land mnatisha kwa hizi Imani. Niko huku najua.
 
... ndugu zangu wasukuma tunatia aibu kwa mambo haya kipumbavu!
Wivu wa mapenzi hauna kabila na wasukuma tu wauao kwa wivu wa mapenzi.

Cha msingi watz tuamke mkishindwa mnaachana kwa amani.
 
hii vita hatuimalizi mpaka wanawake wabaki kwenye mstari ulionyooka
 
Attachments

  • 64A39536-FF70-4BC9-B230-7A6E0A9368F5.jpeg
    64A39536-FF70-4BC9-B230-7A6E0A9368F5.jpeg
    77.3 KB · Views: 12
Mwanaume mmoja Mkazi wa Kitongoji cha Lubela, Mtaa wa Nyashimbi, Kata ya Mhongolo wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga, Bundala Mathew anashikiliwa na Polisi, kwa tuhuma ya kumuua mkewe, Rehema Nyamgila kwa kumcharanga mapanga.

Imedaiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo, alitenganisha viungo vya mwili wa mkewe na kuchukua baiskeli na kuvisafirisha mpaka mbugani usiku wa manane na kuvitawanya ili kupoteza ushahidi.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Magdalena Katambi ambaye ni mtu wa karibu na familia hiyo, alidai kuwa tukio hilo liligunduliwa na mtoto wa marehemu, Ezekiel Bundala tarehe 27 Mei 2022.

"Nilienda kumjulia hali mtoto aliyekuwa anaumwa, ndipo Ezekia akanijulisha kuwa mama yake hayupo funiani.

“Ameniambia aligombana na baba yake kwa kuwa aliona beseni likiwa na damu lakini baba yake akawa anasema hizo ni rangi tu na siyo damu.”

Anasema wakatoa taarifa kwa ndugu, majirani na Polisi, ndipo mtuhumiwa baada ya kubanwa akawapeleka alipoutupa mwili, wakaukuta ukiwa umekatwa vipande.

Alidai ljumaa mwili ulipelekwa kuhifadhiwa mochwari ya Hospitali ya Manispaa ya Kahamana, 28 Mei 2022, Polisi walirudi na mtuhumiwa kuonesha mahali alipohifadhi viungo vingine vya mwili huo, ndipo kichwa kikapatikana kimezikwa juu ya kaburi la marehemu babu yake kwa mama.

Magdalena alidai viungo vingine vya sehemu za siri na matiti vilipatikana karibu na mlango, kwenye mafiga ya jiko, ndipo alipozika, huku akitaka watoto wake wapikie hapo mara kwa mara, kwani ameweka mbayuwayu wake akauke kwa ajili ya kutengenezea dawa.

"Baada ya askari kumhoji tena wapi vilipo viungo vingine, aliwapeleka mbugani ulikookotwa mwili katikati ya majaruba ya mpunga ilipatikana mikono na magoti, lakini wakati huo vidole vya mikono na miguu havikuonekana, kwa kweli tukio hili limetusikitisha na kutuachia simanzi kubwa," alisema Magdalena.

Hata hivyo, mama mzazi wa mtuhumiwa, Mhoja Bundala alidai kupata taarifa kwa watu kuwa mwanawe ameachana na mkamwana wake, hivyo akawa anasubiri taarifa rasmi kutoka kwake, lakini ajabu aliletewa taarifa za tukio hilo la kushitua.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyashimbi, Peter Nzingula alisema tukio hlilitokea usiku wa Mei 27, 2022.

Anasema alipohojiwa chanzo cha kufanya unyama huo, mtuhumiwa alidai alikuwa na wivu wa mapenzi.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mhongolo, Boniphace Maziku alidai kuwa tukio hilo lilitokea kwenye kata yake Mtaa wa Nyashimbi, na alishirikiana na viongozi wa ngazi ya mtaa, kutoa taarifa sehemu husika, na sasa uchunguzi wa tukio unaendelea Polisi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, George Kyando amethibitisha uwepo wa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wake unaendelea, na sheria itachukua mkondo wake.

Marehemu Rehema ameacha watoto wanne.

Source: MwanaHalisi
Aisee ana Roho ngumu afungwe tu Maisha mabaya Msamaha wa Rais asitoke
 
Mtaongea sana mtalalamika sana ila matatizo na migogoro mingi ya ndoa inaanzia kwenye simu
Simu ndo sumu namba moja ya ndoa za sasa hayo mengine ni ziada.
 
Kwa nini haya mambo huwezi kuyasikia sana pwani?
Dini na hofu ya mungu
Ukikuta mkristo anaijua dini kweli
Ukikuta muislamu anaijua dini kweli
Sio huko vita ni vita mura.
 
Mwanaume mmoja Mkazi wa Kitongoji cha Lubela, Mtaa wa Nyashimbi, Kata ya Mhongolo wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga, Bundala Mathew anashikiliwa na Polisi, kwa tuhuma ya kumuua mkewe, Rehema Nyamgila kwa kumcharanga mapanga.

Imedaiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo, alitenganisha viungo vya mwili wa mkewe na kuchukua baiskeli na kuvisafirisha mpaka mbugani usiku wa manane na kuvitawanya ili kupoteza ushahidi.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Magdalena Katambi ambaye ni mtu wa karibu na familia hiyo, alidai kuwa tukio hilo liligunduliwa na mtoto wa marehemu, Ezekiel Bundala tarehe 27 Mei 2022.

"Nilienda kumjulia hali mtoto aliyekuwa anaumwa, ndipo Ezekia akanijulisha kuwa mama yake hayupo funiani.

“Ameniambia aligombana na baba yake kwa kuwa aliona beseni likiwa na damu lakini baba yake akawa anasema hizo ni rangi tu na siyo damu.”

Anasema wakatoa taarifa kwa ndugu, majirani na Polisi, ndipo mtuhumiwa baada ya kubanwa akawapeleka alipoutupa mwili, wakaukuta ukiwa umekatwa vipande.

Alidai ljumaa mwili ulipelekwa kuhifadhiwa mochwari ya Hospitali ya Manispaa ya Kahamana, 28 Mei 2022, Polisi walirudi na mtuhumiwa kuonesha mahali alipohifadhi viungo vingine vya mwili huo, ndipo kichwa kikapatikana kimezikwa juu ya kaburi la marehemu babu yake kwa mama.

Magdalena alidai viungo vingine vya sehemu za siri na matiti vilipatikana karibu na mlango, kwenye mafiga ya jiko, ndipo alipozika, huku akitaka watoto wake wapikie hapo mara kwa mara, kwani ameweka mbayuwayu wake akauke kwa ajili ya kutengenezea dawa.

"Baada ya askari kumhoji tena wapi vilipo viungo vingine, aliwapeleka mbugani ulikookotwa mwili katikati ya majaruba ya mpunga ilipatikana mikono na magoti, lakini wakati huo vidole vya mikono na miguu havikuonekana, kwa kweli tukio hili limetusikitisha na kutuachia simanzi kubwa," alisema Magdalena.

Hata hivyo, mama mzazi wa mtuhumiwa, Mhoja Bundala alidai kupata taarifa kwa watu kuwa mwanawe ameachana na mkamwana wake, hivyo akawa anasubiri taarifa rasmi kutoka kwake, lakini ajabu aliletewa taarifa za tukio hilo la kushitua.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyashimbi, Peter Nzingula alisema tukio hlilitokea usiku wa Mei 27, 2022.

Anasema alipohojiwa chanzo cha kufanya unyama huo, mtuhumiwa alidai alikuwa na wivu wa mapenzi.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mhongolo, Boniphace Maziku alidai kuwa tukio hilo lilitokea kwenye kata yake Mtaa wa Nyashimbi, na alishirikiana na viongozi wa ngazi ya mtaa, kutoa taarifa sehemu husika, na sasa uchunguzi wa tukio unaendelea Polisi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, George Kyando amethibitisha uwepo wa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi wake unaendelea, na sheria itachukua mkondo wake.

Marehemu Rehema ameacha watoto wanne.

Source: MwanaHalisi
Mungu wangu [emoji2958][emoji26][emoji24]

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 
Huyu kaulizwa akasema wivu wa Mapenzi, mbona inaonekana hata kama hajui huo wivu wa mapenzi ni nini.

Alafu wivu gani wa kukatakata viungo, na tena sehemu nyeti kafukia jikoni...huu ni ule ule ujinga wa ushirikina kwa asilimia 90....hilo la wivu wa mapenzi inaonesha karopoka tu.
 
_King we fala si wa kanda ya ziwa? Naomba muache yule binti wa kule jukwaa la Snap it.
 
Siku hizi mwenza akianza kucheza na panga au bunduki potea nakwambia litakukuta jambo.
 
Back
Top Bottom