Kisaikolojia; Watu wanaoonyesha Kujali mbele za watu ndio Wakatili na wale wenye kutoonyesha kujali Mbele za watu ndio wenye Huruma

Ogopa sana mwanaume anaejifanya anampenda mke wake mbele za watu..anaejifanya anahuruma.na mkewe akiumwa kidogo atamsend off kwao akaangaiwe kwa ukaribu zaidi ..hao mara nyingi huwa wanamichepuko yao ya kudumu mara nyingi wakivivusha wake zao kwao ujue ataleta kimada ndani ya nyumba na wamalizana uzinzi wao kwa kitanda ya mkewe..
Mtu unamjua in and out kuwa unaroho mbaya lakini unashangaa how comes anasifiwq huko nje anaroho njema na anajitoa kwa matatizo ya watu qkati watu wake wa karibu hafanyi hivyo..wakimsifia wasimjua unabaki unashangaa hivi hawa watu wakos serious wanachozungumza?
 
KISAIKOLOJIA; WATU WANAOONYESHA KUJALI MBELE ZA WATU NDIO WAKATILI NA WALE WENYE KUTOONYESHA KUJALI MBELE ZA WATU NDIO WENYE HURUMA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Mara nyingi lakini sio zote. Watu wengi utakaowaona wanaonyesha kujali au kuonyesha huruma mbele za watu ndio makatili, wanyanyasaji, waumizao, wadhulumaji kwa kiwango kikubwa.

Mfano,
Watu wengi unaowasikia wanatetea na kuwajali Wanawake mbele za watu, ukiwafutilia zaidi utagundua wao ndio WAKATILI, wanyanyasaji na wakandamizaji WA haohao wanawake.

Alafu wale ambao mbele za watu huonekana wakali kwa Wanawake, WAKATILI, washenzi, na wakandamizaji WA wanawake. Ukifuatilia utagundua ndio wanaojali maslahi ya Wanawake. Ukifuatilia familia zao wake na mabinti Zao Wana furaha na Amani kuliko wale wanaojali mbele za Watu.

Kikawaida Watu wabaya hujionyesha kama wazuri wawapo mbele za watu. Huvaa Uhusika na vazi Bandia.

Uchunguzi wangu unaonyesha, familia zenye watu wanaojionyesha ni Wema mbele za watu kama familia za kidini ndizo zinaongoza kwa kufanya matendo ya kikatili kwa baadhi ya wahusika katika familia.

Watu wabaya kikawaida hutembea kwa kufuata mihemko ya umma, huonyesha kile ambacho umma unataka bila kujali ukweli na HAKI ya Jambo husika. Hii ni tofauti na watu Wema ambao kikawaida wao hawaangalii Mihemko ya Umma/watu isipokuwa wanazungumzia mambo kiuhalisia/ukweli na HAKI.

Watu wabaya kikawaida huangalia wingi wa watu upo sehemu Ipi bila kujali wingi huo upo upande wa dhulma au Haki. Hii ni tofauti na Wema ambao wao hawaangalii wingi au udogo wa watu. Wanachoangalia ni upande upi ipo HAKI na KWELI.

Hivyo, kutokana na waovu kuangalia wingi wa watu na kukaa upande huo wao huonyesha na kuonekana Wema na wenye kujali kumbe ni kinyume na uhalisia wao.

Chunguzi zangu zinaonyesha,

1. Asilimia 90% ya watu walioonyesha ni wakali, wakatili, wabaya na wenye kupewa majina Mabaya. Nilipokaa nao na kuwadadisi bila ya wao kujua, matokoe niliyo yapata walikuwa sivyo walivyo, wanavyoonekana, wanavyosema. Walikuwa Watu Wema Sana.
Jambo kubwa kwao ni watu straight, watu wa nyeusi ni nyeusi na nyeupe ni nyeupe.

2. 90% ya watu waliojionyesha ni Wema mbele za watu nilipokaa nao nilishangazwa na matokeo niliyoyapata. Wengi sivyo wanavyoonekana, sivyo wanavyosemwa. Wengi ni wakatili, waovu na wenye Roho za Hatari na Mbaya.

3. Niligundua pia, watu wengi ambao wanalazimisha uwaone ni waaminifu na kujionyesha ni waaminifu asilimia 99% sio waaminifu.

4. Niligundua pia, watu wengi wanaojali maoni ya wengine kwa kutaka utukufu, kusifiwa, kulazimisha wengine waonekane wao ni Bora. 99% ya watu hao ni wafitinishaji, wachonganishi na wanaroho mbaya.

Watu wasiojali maoni ya wengine juu Yao hiyo humaanisha wanaheshimu Uhuru wa maoni, na watu hao kikawaida sio madikteta, wakatili.
Lakini watu wanaojali maoni ya wengine kwa asilimia 90 hawaheshimu maoni ya wengine.

5. Watu ambao hupenda kuelezea Jinsi wanavyosaidia watu wengine. 90% hawana Shukrani, ni wanyanyasaji, na hupenda kuabudiwa.
Hii ni tofauti na watu ambao hawataki kujulikana kuwa wao ndio wametoa msaada.

Hii inamaanisha, 99% ya Mtu anayekupa msaada mbele za watu, msaada huo utakuwa mtego kwako. Ni deni na lazima akutangaze. Na wengi hutaka uwaabudu.

6. 90% ya watu ambao watakusifia hata kwa Mabaya yako. Haohao ndio watakaohusika na anguko Lako ikiwezekana kukuua.
Na wale ambao unawaona wabaya kwa kukusema ukweli. 90% hao ndio watakuokoa.

Mimi acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
100% perfect Andiko
 
Aisee hili andiko unaweza kuwa umewataja watu wawili wakubwa hapa Nchini.
 
Back
Top Bottom