Tetesi: Kisandu ni kweli kajiengua Kanisa Katoliki

Aseee kumbe huyu Deo Kisandu alipita kwenye mikono ya Padre Ricardo Maria?Ha ha ha ha pale lazima akimbie.Maisha ya yule padre anayaweza mwenyewe!!Hataki Gari,yeye ni mwendo wa Baiskeli na kutembea pekupeku!Kula viporo na kulala kwenye ngozi.

Niliwahi kumtembelea huyu Padre,yale maisha kama ndio kwenda Mbinguni,basi kwa huyu jamaa geti lilishafunguliwa na malaika

Padre Ricardo Maria kwenye mitaa ya Morogoro
 
Daah..
Ni kwamba mimi tu au sioni mantik ya kutaftia kiki uamuz wake.
Aldhan upadri n uchingaji au.
Daaah..i believe 100%. Hayupo okay upstairs
 
endelea kusoma misale na bikra maria akuombee kwa Mungu akiwa amem-substitute Jesus christ


Na weye endelea kuwabeza wenzio wamwombapo Mama wa Kanisa awaombee. Wao wanaendelea kupata ka vinamwagwa, huku weye ukikimbila kwa nabii akuombee. Mjanja nnani hapo? Miye namwamba mama kanisa, mama wa Mungu, ananipa weye waenda kuombewa na nabii sijui malisa, nnani mwenye ufaham?? Acheni niisome misale yangu kuliko kuisoma biblia nikaombewe na nabii Frank na Tb sijui nani Mnigeria
 
H uyo papa Pius aliwadanganya wakristu WA kipindi hicho,biblia haina maagizo ya namna hiyo,mkombozi wetu nimmoja Tu,mwakilishi wetu Ni mmoja Tu,msaada wetu Ni mmoj Tu,hakuna wengine SI papa ,watakatifu hewa,Maria wala mitume ....huyo Ni YESU..(yoh3:16)
 
Akae tu kimya.... wengi tulitoka kwenye ukatoliki kimya kimya.... wengine tulifikia hatua za juu kabisa kuwa mapadre.... tumeacha ndugu huko ambao ni maaskofu so hiyo sio ishu...
"Roma Locuta causa finita est"
 
endelea kusoma misale na bikra maria akuombee kwa Mungu akiwa amem-substitute Jesus christ
Kam substitute wapi mama wa watu jamanii? Ujue kama Yesu ni Mungu manaake yule ni mama wa Mungu, No Mary, no Jesus, know Mary Know Jesus. Yule ni Eva mpya, Eva alidondoka kwa disobedience, Maria alishinda kwa Obedience akatuletea Mkombozi, sasa wewe na martin Luther jifanyeni wajuaji, ila ABANDONING THE MOTHER IS BUT ONE STEP FROM ABANDONING THE SON, ndo maana waprotestant mnahangaika hangaika hamuelewi ata mpo wapi na mnaelekea wapi, mnazolewa zolewa tu.
 


Mkuu;
Leo tumemtembelea bibi mmoja mzee na nimgonjwa kweli kweli, alichonifurahisha ni kwamba, tulimkuta akiwatolea uvivu malokole yalio enda hapo ati kumuombea. Bibi wa watu ni jana tu Padre alienda kumpaka mpako wa mwisho. Jua kwamba huu ni ufunuo wa miaka na miaka kutoka kwa Mungu kuja kwa Papa James I, kuwa alioneshwa na Mungu kuwa watu wapakwe mafuta matakatifu yanayo tengenezwa na kubarikiwa katika kipindi cha Pasaka, tangu miaka hiyo kumewekwa tone kwenye kila chupa kwani yalitoka mbinguni. Mgonjwa akiisha kupakwa hayo, hakuna tena haja ya sakramenti nyingine. Haya malokole yakenda kumuombea. Aliwatoa nje. P/up sana bibi, usiiuze imani yako kwa maneno hewa. Tutaamini maneno ya Mababa watakatifu kwani hutoka kwa Mungu Direct.
 
Soma post zangu utajua Mi ni mtu wa Aina gani. Mimi ni mkatoliki. Ila ata mkatoliki mwenzangu akitaka kupotosha lazima nimpe
 
Mbona hafahamiki ,pia nilisoma ule walakawake kunakipengele amesema hats huko aliko hamia wakimzingua ataanzisha kanisa lake.pia walipo mbania kumbatiza aliamua kujibatiza yeye mwenyewe ,mambo mengi ya ajabu ajabu ameyaandika humo ,jamaa anaonekana anamatatizo ya ubongo hayuko sawa
 
Yeye ni nani kwenye kanisa lenye utajiri wa waamini?
 
WHO ARE YOU????????
 
Hata akikwazika ukweli ndo umemkwaza sio kaka. Amina
 
Nahis akilu zinaanza kumruka,nanu akufuatilie wakati huna impact kwenye kanisa.Wameondokka mapdri na maaskofu bado kanisa liko imara. muulize dr. slaa
 
Mim smjui huyo jamaa lakini namna alivyoandika hayo maelezo unaona kuna kitu hakiko sawa akilini mwake,na hii huenda ni matokeo ya huo aliouita utawa wakati mwli wake ulikuwa hauwezi kuwa mtawa
 
Hivi ni muitaliano? Hata mimi nilipomuona nilimshangaa nikadhani sio mkatoliki maana mapadre wa katoliki wamezoeleka kuonekana na magari ya kifahari ila yeye yupo na baiskeli tu.

Kuhusu kwenda mbinguni kama ulivyomtabiria ni suala ambalo lipo nje ya hisia za kibinadamu. Ni Mungu tu ndiye achunguzaye mioyo ya watu anafahamu mtumishi wake wa kweli ni nani kwa sababu wapo watu wanaoweza kuigiza matendo ili tu wapate kutazamwa na watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…