Tetesi: Kisandu ni kweli kajiengua Kanisa Katoliki

Aseee kumbe huyu Deo Kisandu alipita kwenye mikono ya Padre Ricardo Maria?Ha ha ha ha pale lazima akimbie.Maisha ya yule padre anayaweza mwenyewe!!Hataki Gari,yeye ni mwendo wa Baiskeli na kutembea pekupeku!Kula viporo na kulala kwenye ngozi.

Niliwahi kumtembelea huyu Padre,yale maisha kama ndio kwenda Mbinguni,basi kwa huyu jamaa geti lilishafunguliwa na malaika
image.jpeg

Padre Ricardo Maria kwenye mitaa ya Morogoro
 
Daah..
Ni kwamba mimi tu au sioni mantik ya kutaftia kiki uamuz wake.
Aldhan upadri n uchingaji au.
Daaah..i believe 100%. Hayupo okay upstairs
 
endelea kusoma misale na bikra maria akuombee kwa Mungu akiwa amem-substitute Jesus christ

Na weye endelea kuwabeza wenzio wamwombapo Mama wa Kanisa awaombee. Wao wanaendelea kupata ka vinamwagwa, huku weye ukikimbila kwa nabii akuombee. Mjanja nnani hapo? Miye namwamba mama kanisa, mama wa Mungu, ananipa weye waenda kuombewa na nabii sijui malisa, nnani mwenye ufaham?? Acheni niisome misale yangu kuliko kuisoma biblia nikaombewe na nabii Frank na Tb sijui nani Mnigeria
 
H
mshan jr;
Umemwona wapi hapa?? Jamaa kajitoa kwa makeke hataki kuyafanya mambo kwa siri ka sisi wengine. By the way, who is Kisandu? Ana nini hadi kutangazia Katoliki kuwa wasimfuate fuate?? Kwani yeye ndo wa kwanza kuuacha Ukatoliki??
Aelewe kuwa Papa Pius wa X alisema katika mtaguso mkuu kuwa, mtu yeyote atakaye uasi Ukatoliki, akifa ni motoni milele hivyo Kisandu jiandae kabisa kwenda motoni. Tuulize tulioukulia huo Ukatoliki
uyo papa Pius aliwadanganya wakristu WA kipindi hicho,biblia haina maagizo ya namna hiyo,mkombozi wetu nimmoja Tu,mwakilishi wetu Ni mmoja Tu,msaada wetu Ni mmoj Tu,hakuna wengine SI papa ,watakatifu hewa,Maria wala mitume ....huyo Ni YESU..(yoh3:16)
 
Akae tu kimya.... wengi tulitoka kwenye ukatoliki kimya kimya.... wengine tulifikia hatua za juu kabisa kuwa mapadre.... tumeacha ndugu huko ambao ni maaskofu so hiyo sio ishu...
"Roma Locuta causa finita est"
 
endelea kusoma misale na bikra maria akuombee kwa Mungu akiwa amem-substitute Jesus christ
Kam substitute wapi mama wa watu jamanii? Ujue kama Yesu ni Mungu manaake yule ni mama wa Mungu, No Mary, no Jesus, know Mary Know Jesus. Yule ni Eva mpya, Eva alidondoka kwa disobedience, Maria alishinda kwa Obedience akatuletea Mkombozi, sasa wewe na martin Luther jifanyeni wajuaji, ila ABANDONING THE MOTHER IS BUT ONE STEP FROM ABANDONING THE SON, ndo maana waprotestant mnahangaika hangaika hamuelewi ata mpo wapi na mnaelekea wapi, mnazolewa zolewa tu.
 
H
uyo papa Pius aliwadanganya wakristu WA kipindi hicho,biblia haina maagizo ya namna hiyo,mkombozi wetu nimmoja Tu,mwakilishi wetu Ni mmoja Tu,msaada wetu Ni mmoj Tu,hakuna wengine SI papa ,watakatifu hewa,Maria wala mitume ....huyo Ni YESU..(yoh3:16)

Mkuu;
Leo tumemtembelea bibi mmoja mzee na nimgonjwa kweli kweli, alichonifurahisha ni kwamba, tulimkuta akiwatolea uvivu malokole yalio enda hapo ati kumuombea. Bibi wa watu ni jana tu Padre alienda kumpaka mpako wa mwisho. Jua kwamba huu ni ufunuo wa miaka na miaka kutoka kwa Mungu kuja kwa Papa James I, kuwa alioneshwa na Mungu kuwa watu wapakwe mafuta matakatifu yanayo tengenezwa na kubarikiwa katika kipindi cha Pasaka, tangu miaka hiyo kumewekwa tone kwenye kila chupa kwani yalitoka mbinguni. Mgonjwa akiisha kupakwa hayo, hakuna tena haja ya sakramenti nyingine. Haya malokole yakenda kumuombea. Aliwatoa nje. P/up sana bibi, usiiuze imani yako kwa maneno hewa. Tutaamini maneno ya Mababa watakatifu kwani hutoka kwa Mungu Direct.
 
Mkuu;
Kati yangu mimi na weye, nnani haswa aende shule? Weye uliyesikia kuwa kuna Katoliki wala hutaki kuupokea ndo ukasome, punguza hearsay. Biblia imesema wapi kuna kufufua misukule?? Kuna mitume wa pesa?? Luna ngurumo za kupaka?? Nadhani hujui maana ya hearsay.
Someni hiyo Biblia mtaelewa wala hamtapelekwa puta
Soma post zangu utajua Mi ni mtu wa Aina gani. Mimi ni mkatoliki. Ila ata mkatoliki mwenzangu akitaka kupotosha lazima nimpe
 
Mbona hafahamiki ,pia nilisoma ule walakawake kunakipengele amesema hats huko aliko hamia wakimzingua ataanzisha kanisa lake.pia walipo mbania kumbatiza aliamua kujibatiza yeye mwenyewe ,mambo mengi ya ajabu ajabu ameyaandika humo ,jamaa anaonekana anamatatizo ya ubongo hayuko sawa
 
Yeye ni nani kwenye kanisa lenye utajiri wa waamini?
 
WARAKA MAALUM WA KUJIVUA UUMINI NA USHIRIKI NDANI YA KANISA KATOLIKI LA ROMA.

UTANGULIZI.

Tumsifu Yesu Kristu na Bwana Yesu Atukuzwe sana.

Naanza kujivua Ukatoliki kwa Kutumia KATIBA ya NCHI ibara 19 kifungu cha 1&2 kinachosema uhuru wa kubadili dini au dhehebu au kubadili Imani.

Ndugu zangu Watanzania wenzangu na wakristu wenzangu wote wa Taifa letu Tanzania, Mimi DEOGRATIUS NALIMI KISANDU ni Mtanzania asilia, kabila langu ni mchanganyiko wa Msukuma na Mnyamwezi. Nilizaliwa Tarehe 28 Juni 1980 katika Hospitali ya wilaya ya Kahama mjini, mkoa wa Shinyanga, nimekulia vijiji/mitaa ya Busoka inyembe, Itugunhu na mtaa wa kilima wilayani kahama.

MAJINA YANGU NA UBATIZO.
Nilizaliwa siku ya jumamosi na kupewa jina la kuzaliwa MASHAKA, na na nikiwa darasa la tatu shule ya msingi Sunge, kijiji cha Itugunhu kabla ya kuhamia shule ya msingi kahama,mwaka 1992 nilibatizwa na kuwa DEOGRATIUS katika kanisa katoliki la Mtakatifu kaloli Lwanga kahama mjini,

Hivyo kwakuwa hakukuwa na utaratibu wa kubadilisha majina ukiwa shule baada ya kubatizwa niliendelea kuitwa MASHAKA KISANDU shule ya msingi na sekondari ndipo nilipo anza kutumia jina la Ubatizo yaani DEOGRATIUS KISANDU ambalo ndilo nimetumia mpaka elimu yangu ya juu.

Kwa kuwa mimi napenda Kuaficanize maisha, hivyo pia huwa napenda kutumia majina yangu yote mawili la ubatizo na la kuzaliwa yaani DEOGRATIUS MASHAKA KISANDU.

KUJIUNGA NA UTAWA-MOROGORO.
Mwaka 1998 nilijiunga na Shirika la Kikatoliki la Ndugu wa Dogo wa Afrika lililopo KOLA-Morogoro mjini chini ya Padre Ricardo Maria, hata hivyo nilikaa jumuia ya mjini kwa miezi mitatu na baada ya hapo baadhi tulihamishiwa kwenda Parokia ya KILOKA ili kujenga Jumuia nyingine yaani Convent.

Tukiwa jumuia ya ndugu wadogo wa afrika Kiroka tulifikia nyumba ya parokia na tulianza kufyeka mapori na vichaka kwa maeneo tuliyonunua na kufanikiwa kujenga nyumba mbili ya masisita naya kwetu sisi Mabruda, wakati huo mimi nilikuwa bado katika hatua za awali za UASPIRANTI yaani UTAKAJI.

Tulishirikiana vizuri tu na watawa wenzangu huko Kiroka pamoja na mafundisho mbalimbali ya kutukomaza kiroho na kimaisha, kwa kipindi chote nilichokaa Utawani nilijifunza mambo mengi sana tena sana na hapo ndipo nilipo mjua Mungu anafanya nini katika maisha ya mwanadamu.

Cha kushangaza sisi tulichelewesha hatua zote za utawa kwani tumekaa kwenye hatua ya Utakaji kwa muda mrefu bila kupewa hatua nyingine kama waliotutangulia na ikalazimu baadhi wa wenzangu tuliokuja nao utawani kuanza kuondoka, lakini huenda ilikuwa ni kusudio la Mungu ili Mungu afanye jambo jingine jipya katika maisha yangu.

KUONDOKA UTAWANI-Morogoro.
April 1999 nilimwandikia barua ya Kuachana na maisha ya Kitawa ya Ndugu wadogo wa Afrika padre Ricardo Maria ambaye ni Mkuu wa Shirika na bila hiana alikubali na kuniruhusu niondoke na nauli akanipa, nikapanda treni mpaka nyumbani Kahama.

Mwaka huo huo wa 1999 nikajiunga na EVENING CLASSES yaani ODL KISHIMBA SEKONDARI na kusoma kidato cha kwanza mpaka cha Nne huku nikitumia Jina nililochukua Utawani la Padre Pio kwasasa ni Mtakatifu, jina hilo la kitawa nilipewa na Buruda Daud tukiwa Konvent ya kiroka. Hivyo nikawa DEOGRATIUS PIO KISANDU, hata hivyo nimeshafika kwa wakili na kuapa kuondoa jina hilo na kuweka jina la mzazi wangu mzee Nalimi yaani DEOGRATIUS NALIMI KISANDU.

Hata hivyo mwaka 2007 nilitafta kituo cha kufanyia mtihani wa kidato cha sita nikapata kituo cha Tabora girls na kufanya mtihani wa kidato cha sita na mwaka 2008 nika resit tena Kituo cha kahama sekondari, pamoja na kupitia mafunzo ya uandishi wa habari, leseni ya ualimu yaani Induction Course na shahada ya maswala ya elimu maalum ndani yake nimesoma Uongozi na siasa.

Yote haya na gharama zote ziligharamiwa na mama yangu mzazi na hakuna mtawa au Padre aliyetia mkono wake zaidi ya padre Artur mkapuchin aliyenisapoti kwa gharama za mavazi.

VIRAFRA NA WASEKULARI.
Nilipotoka utawani niliendelea kuwa chini ya Utawa wa tatu wa Wafransisko wasekulari yaani wateresiari nikilelewa chini yao kama VIRAFRA kwasasa VIFRA yaani Vijana rafiki wa Mtakatifu fransisko wa Asizi nikiwa Mwenyekiti wa VIRAFRA chini ya Uangalizi wa Marehemu Bruda Richard Kinyaruhama Ofm Capuchin.

UTUMIKIZI/USAIDIZI WA MISA KWA MAPADRE
Nimekuwa mtumikizi tangu mwaka 1992 baada ya kubatizwa katika Parokia ya kahama mjini mpaka mwaka 2002 nilipo hitimu kidato cha nne. Nimefanya kazi hii kwa muda mrefu sana chini ya Mapadre wafuatao Isaya, kadundu, Maziku na hayati Askofu Mateo Shija katika Parokia ya kahama mjini na jimbo la kahama ambao kimsingi ndio walikuwa walezi wetu miaka yote.

KUKANWA NA WATAWA WENZANGU.
Katika hali ya kushangaza sana nilipoanza kuonekana kisiasa na pia kupanda juu kielimu, watu walianza kuhoji ujio wangu hasa kipindi nilipotangaza kugombea urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania nikiwa mkoani Tanga, watawa wenzangu inasadikika walipoulizwa kama niliwahi kuwa mtawa walinikana kabisa kitu kilichosababisha mateso na kuonekana mimi ni muongo na mbabaishaji, hata kuzushiwa mambo mengine yasiyo ya msingi kwa Taifa.

Nimekubali kudhalilika na kufedheheka ili Mungu ajitukuze kwa kukanwa. Mimi sija laaniwa ila wanaotengeneza laana ndio walio laaniwa. Nina washukru hata mapadre walio nilea hata wao wamenikana kuwa hawanijui ili hali wananijua. Nimekubali kuzodolewa kwakuwa nilikwisha achana na maisha hayo ya kitawa tangu mwaka 1999. Hali hii imesababisha kutoaminika sehemu nyingi na kucheleweshwa maisha yangu naya watoto wangu.

MAAMUZI MAGUMU.
Mimi ni mzazi na ni baba wa watoto huwezi kunilazimisha maisha ya kitawa wakati nilishaga toka miaka mingi sana. Nimelitumikia kanisa katika mambo mengi sana ya kijamii naya kiroho, kwa mjibu wa KATIBA ya Nchi ibara ya 19 kifungu kidogo cha 1 na cha 2 kina mpa ruhusa Mtanzania kubadilisha Dini au Dhehebu pia kubadili Imani ya kuabudu na kuwa huru katika imani yake.

Kwa mantiki hiyo na tangaza rasmi leo kuwa Mimi kuanzia sasa sio Mkristu Mkatoliki tena, nimeamua kuungana na makanisa yanayoamini NGUVU ZA ROHO MTAKATIFI yaani UVUVIO WA ROHO MTAKATIFU, nitashirikiana na wakatoliki kwenye maswala ya kijamii ya kujenga nchi kama ninavyo shirikiana na waislamu kwenye Maswala ya kijamii ya kujenga nchi.

Lakini kwenye swala la Kiimani kuanzia leo niko makanisa ya UVUVIO wa Roho Mtakatifu na hata wao wasipoonesha ushirikiano taanzisha Dhehebu langu likiwa chini ya UVUVIO WA ROHO MTAKATIFU. Siogopi kupigwa risasi wala kuvamiwa wala kuzomewa wala kutengwa kwani mmekwisha nitenga miaka mingi kwa kuninyima ushirikiano.

Kuanzia leo kwa Damu ya Yesu na kula Kiapo kuwa mimi DEOGRATIUS NALIMI KISANDU jana tarehe 17 Oktoba 2016 nilijibatiza kwa Nguvu za Roho Mtakatifu kupitia Damu ya Yesu kwa maji mengi baada ya kuona wachungaji wanakuwa waoga kunibatiza, kwani Yesu angeweza kujibatiza lakini alimshinikiza Yohana ambatize, kwa kuwa nimekosa wa kunibatiza kwa maji mengi kisa wanaogopa vitisho basi nimebatizwa na Roho Mtakatifu mwenyewe kwa maji mengi. Ubatizo huu ni halali mbele za Mungu.

UHURU.
Naomba tena niachwe kuwa huru katika nchi yetu na taifa letu Tanzania na yeyote atakayetangulia mahakamani, mimi nitamtanguliza jela kwa Jina la Yesu. Mimi ni kanisa linalotembea THE MOVING CHURCH IN JESUS NAME. Nitajishughulisha na mambo yote ya kijamii ikiwemo Dini, Siasa za vyama, maisha ya kijamii n.k. Na mkitengeneza Deogratius Kisandu wa Kubumba mtakiona cha moto.

Ninawashukru wote ndani ya kanisa Katoliki mlionilea na mlioshirikiana na mimi katika mambo ya kidini, napokea mapingamizi yote maana ofisi yangu inatembea THE MOVING OFFICE. Sijamchokoza mtu bali nataka uhuru ndani ya Nchi yetu.

Ni mimi niliyekuwa Mkristu Mkatoliki na sasani Mkristu wa Nguvu za Roho Mtakatifu.

Mdharauliwaaaa,

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU

Mtumishi Mdogo sana wa Mungu.

18 Oktoba 2016
WHO ARE YOU????????
 
Mkuu mie Mkatoliki na kulingana na mafundisho niliyopewa/kuzwa ktk Katoliki kila kitu kinaenda kwa mapenzi ya Mungu,mimi kukosa hiki wewe kupata kile ni kawaida natakiwa kushukuru na kuomba Mungu anionyeshe njia ninini kingine nikafanye sio kulaumu,mnaolaumu kuukosa Upadre au mlishawahi kuwa mkaachishwa Mungu hakuwachagua mumtumikie kwa njia hiyo ila kuna njia nyengine aliwaandalia but kutokana na kukengeuka kwenu mme-paanic na kuanza kulaum na sichelei kusema kuhisi au hata kuamini kwamba mlikuwa mnatafuta maslahi binafsi ndani ya Kanisa so mlipotolewa mnalaum na kushusha kashfa.samahani sana kaka kama nitakukwaza kwa post yangu.
Hata akikwazika ukweli ndo umemkwaza sio kaka. Amina
 
Nahis akilu zinaanza kumruka,nanu akufuatilie wakati huna impact kwenye kanisa.Wameondokka mapdri na maaskofu bado kanisa liko imara. muulize dr. slaa
 
Mim smjui huyo jamaa lakini namna alivyoandika hayo maelezo unaona kuna kitu hakiko sawa akilini mwake,na hii huenda ni matokeo ya huo aliouita utawa wakati mwli wake ulikuwa hauwezi kuwa mtawa
 
Aseee kumbe huyu Deo Kisandu alipita kwenye mikono ya Padre Ricardo Maria?Ha ha ha ha pale lazima akimbie.Maisha ya yule padre anayaweza mwenyewe!!Hataki Gari,yeye ni mwendo wa Baiskeli na kutembea pekupeku!Kula viporo na kulala kwenye ngozi.

Niliwahi kumtembelea huyu Padre,yale maisha kama ndio kwenda Mbinguni,basi kwa huyu jamaa geti lilishafunguliwa na malaika
View attachment 424216
Padre Ricardo Maria kwenye mitaa ya Morogoro
Hivi ni muitaliano? Hata mimi nilipomuona nilimshangaa nikadhani sio mkatoliki maana mapadre wa katoliki wamezoeleka kuonekana na magari ya kifahari ila yeye yupo na baiskeli tu.

Kuhusu kwenda mbinguni kama ulivyomtabiria ni suala ambalo lipo nje ya hisia za kibinadamu. Ni Mungu tu ndiye achunguzaye mioyo ya watu anafahamu mtumishi wake wa kweli ni nani kwa sababu wapo watu wanaoweza kuigiza matendo ili tu wapate kutazamwa na watu.
 
Back
Top Bottom