Tetesi: Kisandu ni kweli kajiengua Kanisa Katoliki

Tetesi: Kisandu ni kweli kajiengua Kanisa Katoliki

yani unahama dhehebu kisa umezinguana na kikundi cha watu ndani ya hilo dhehebu? vipi na huko anakoenda akikuta mchungaji ana dhambi zake, je atahama tena?
 
Pole sana ndugu.. ulijiunga utawani mwaka 98 mwaka 99 ukajitoa eti kwa kuona umekaa muda mrefu bila kupanda ngazi.. mwaka mmoja unakata tamaa?? Inaonekana una pupa sana..
 
nimeona uvivu kumalizia kwa kuwa mwandishi umegusa kanisa katoliki lenye maadui wengi sana hapa duniani...

yesu mwenyewe kwa kinywa chake alisema "wala milango ya kuazimu haitalitikisa haitalitikisa kanisa lake"...

hacha magugu na ngano vimee pamoja, ili utukufu wa Mungu uweze kujidhihilisha
 
mshan jr;
Aelewe kuwa Papa Pius wa X alisema katika mtaguso mkuu kuwa, mtu yeyote atakaye uasi Ukatoliki, akifa ni motoni milele hivyo Kisandu jiandae kabisa kwenda motoni. Tuulize tulioukulia huo Ukatoliki

shida wakatoliki wengi hawasomi biblia ndo maana papa alitamka hivyo swali
papa ni nani hadi aingilie mamlaka ya Mungu kumhukumu mtu?

ni mahala gani katika maandiko Mungu alijitangaza kuwa katolik ndo dhehebu lake?

je papa naye ana kiti chake cha hukumu ?

kuwa kanisa baba/mama mbele za Mungu si kitu cha kushikamana nacho soma habari ya Ibrahimu alibalikiwa sana na Mungu lakini baba yake hakupata hiyo neema pia
katika uongozi papa/maaskofu /mapadre hawa jukumu lao ni la kichungaji=kuwalisha kondoo neno la Mungu wasipoete ingekua hivyo mtume Petro basi asingeendelea kuhubiri injili kisa alitangazwa kuwa yeye ni mwamba na Kristo

Pia wana JF msipende kushadadia mambo without critical thinking and the reality of matter ni dhahiri kabisa uko nyumba za malezi kuna some issue za uonevu sana ukitaka kujua uliza watu waliosoma minor, junior and major seminary watakwambia

mshana jr na uchawi wako nmekushanga katika thread hii ku-comment uhalo mtupu while you have an opportunity to ask the threader so many questions

Finally wakatolik someni NENO LA MUNGU ambalo ni kweli ya Kristo nalo litawaweka huru, usinywe yale tu asemayo padre/askofu/papa ukajua ndo sahihi kwako Roho Mtakatifu humfunulia kila mtu kwa viwango tofautitofauti ndo maana kuna karama za Roho Mtakatifu
 
Aisee nilifikiria ni KISANDU huyu mtangazaji wa Coconut Fm Zanzibar kwenye Kipindi cha Michezo cha Coco Sport

Haya endeleeni,wakuu samahanini
 
Unaonekana ulitoka kwa uchungu, ndio maisha na pengine Mungu ana mpango mkubwa zaidi na wewe. Acha kulalamika, acha kumlaumu mtu, mshukuru Mungu kwani anajua anataka kufanya nini na wewe
 
Lipumba alipojitoa cuf alitangazia uma, dr slaa nae, sumaye n.k. Sasa kujitoa kwenye dini/dhehebu nayo inahitaji matangazo? Shiiiiit!!!
 
shida wakatoliki wengi hawasomi biblia ndo maana papa alitamka hivyo swali
papa ni nani hadi aingilie mamlaka ya Mungu kumhukumu mtu?

ni mahala gani katika maandiko Mungu alijitangaza kuwa katolik ndo dhehebu lake?

je papa naye ana kiti chake cha hukumu ?

kuwa kanisa baba/mama mbele za Mungu si kitu cha kushikamana nacho soma habari ya Ibrahimu alibalikiwa sana na Mungu lakini baba yake hakupata hiyo neema pia
katika uongozi papa/maaskofu /mapadre hawa jukumu lao ni la kichungaji=kuwalisha kondoo neno la Mungu wasipoete ingekua hivyo mtume Petro basi asingeendelea kuhubiri injili kisa alitangazwa kuwa yeye ni mwamba na Kristo

Pia wana JF msipende kushadadia mambo without critical thinking and the reality of matter ni dhahiri kabisa uko nyumba za malezi kuna some issue za uonevu sana ukitaka kujua uliza watu waliosoma minor, junior and major seminary watakwambia

mshana jr na uchawi wako nmekushanga katika thread hii ku-comment uhalo mtupu while you have an opportunity to ask the threader so many questions

Finally wakatolik someni NENO LA MUNGU ambalo ni kweli ya Kristo nalo litawaweka huru, usinywe yale tu asemayo padre/askofu/papa ukajua ndo sahihi kwako Roho Mtakatifu humfunulia kila mtu kwa viwango tofautitofauti ndo maana kuna karama za Roho Mtakatifu
We kweli nawe mgonjwa yani hatusomi kitabu tulichoki assemble wenyewe? Au unataka kukariri mistari unayoitaka kama kasuku? Tunaijua Tena sana kuliko mprotestanti yeyote atakayewahi na aliyewahi kutokea ulimwenguni, nkitaka nijaribu Mimi hapa.
 
shida wakatoliki wengi hawasomi biblia ndo maana papa alitamka hivyo swali
papa ni nani hadi aingilie mamlaka ya Mungu kumhukumu mtu?

ni mahala gani katika maandiko Mungu alijitangaza kuwa katolik ndo dhehebu lake?

je papa naye ana kiti chake cha hukumu ?

kuwa kanisa baba/mama mbele za Mungu si kitu cha kushikamana nacho soma habari ya Ibrahimu alibalikiwa sana na Mungu lakini baba yake hakupata hiyo neema pia
katika uongozi papa/maaskofu /mapadre hawa jukumu lao ni la kichungaji=kuwalisha kondoo neno la Mungu wasipoete ingekua hivyo mtume Petro basi asingeendelea kuhubiri injili kisa alitangazwa kuwa yeye ni mwamba na Kristo

Pia wana JF msipende kushadadia mambo without critical thinking and the reality of matter ni dhahiri kabisa uko nyumba za malezi kuna some issue za uonevu sana ukitaka kujua uliza watu waliosoma minor, junior and major seminary watakwambia

mshana jr na uchawi wako nmekushanga katika thread hii ku-comment uhalo mtupu while you have an opportunity to ask the threader so many questions

Finally wakatolik someni NENO LA MUNGU ambalo ni kweli ya Kristo nalo litawaweka huru, usinywe yale tu asemayo padre/askofu/papa ukajua ndo sahihi kwako Roho Mtakatifu humfunulia kila mtu kwa viwango tofautitofauti ndo maana kuna karama za Roho Mtakatifu
Unawataka wakatolliki wasome Biblia. Wewe mwenyewe huijui. Tatizo lako ni ujinga. Soma biblia kwa makini ili usije jikuta umechanganyikiwa. Biblia siyo sawa na hadithi za Abunuwasi.
 
Anatafuta wafuasi wa kwenda kuanzisha kanisa lake kupitia jamiiforum.
 
WARAKA MAALUM WA KUJIVUA UUMINI NA USHIRIKI NDANI YA KANISA KATOLIKI LA ROMA.

UTANGULIZI.

Tumsifu Yesu Kristu na Bwana Yesu Atukuzwe sana.

Naanza kujivua Ukatoliki kwa Kutumia KATIBA ya NCHI ibara 19 kifungu cha 1&2 kinachosema uhuru wa kubadili dini au dhehebu au kubadili Imani.

Ndugu zangu Watanzania wenzangu na wakristu wenzangu wote wa Taifa letu Tanzania, Mimi DEOGRATIUS NALIMI KISANDU ni Mtanzania asilia, kabila langu ni mchanganyiko wa Msukuma na Mnyamwezi. Nilizaliwa Tarehe 28 Juni 1980 katika Hospitali ya wilaya ya Kahama mjini, mkoa wa Shinyanga, nimekulia vijiji/mitaa ya Busoka inyembe, Itugunhu na mtaa wa kilima wilayani kahama.

MAJINA YANGU NA UBATIZO.

Nilizaliwa siku ya jumamosi na kupewa jina la kuzaliwa MASHAKA, na na nikiwa darasa la tatu shule ya msingi Sunge, kijiji cha Itugunhu kabla ya kuhamia shule ya msingi kahama,mwaka 1992 nilibatizwa na kuwa DEOGRATIUS katika kanisa katoliki la Mtakatifu kaloli Lwanga kahama mjini, hivyo kwakuwa hakukuwa na utaratibu wa kubadilisha majina ukiwa shule baada ya kubatizwa niliendelea kuitwa MASHAKA KISANDU shule ya msingi na sekondari ndipo nilipo anza kutumia jina la Ubatizo yaani DEOGRATIUS KISANDU ambalo ndilo nimetumia mpaka elimu yangu ya juu. Kwa kuwa mimi napenda Kuaficanize maisha, hivyo pia huwa napenda kutumia majina yangu yote mawili la ubatizo na la kuzaliwa yaani DEOGRATIUS MASHAKA KISANDU.

KUJIUNGA NA UTAWA-MOROGORO.

Mwaka 1998 nilijiunga na Shirika la Kikatoliki la Ndugu wa Dogo wa Afrika lililopo KOLA-Morogoro mjini chini ya Padre Ricardo Maria, hata hivyo nilikaa jumuia ya mjini kwa miezi mitatu na baada ya hapo baadhi tulihamishiwa kwenda Parokia ya KILOKA ili kujenga Jumuia nyingine yaani Convent. Tukiwa jumuia ya ndugu wadogo wa afrika Kiroka tulifikia nyumba ya parokia na tulianza kufyeka mapori na vichaka kwa maeneo tuliyonunua na kufanikiwa kujenga nyumba mbili ya masisita naya kwetu sisi Mabruda, wakati huo mimi nilikuwa bado katika hatua za awali za UASPIRANTI yaani UTAKAJI. Tulishirikiana vizuri tu na watawa wenzangu huko Kiroka pamoja na mafundisho mbalimbali ya kutukomaza kiroho na kimaisha, kwa kipindi chote nilichokaa Utawani nilijifunza mambo mengi sana tena sana na hapo ndipo nilipo mjua Mungu anafanya nini katika maisha ya mwanadamu. Chakushangaza sisi tulichelewesha hatua zote za utawa kwani tumekaa kwenye hatua ya Utakaji kwa muda mrefu bila kupewa hatua nyingine kama waliotutangulia na ikalazimu baadhi wa wenzangu tuliokuja nao utawani kuanza kuondoka, lakini huenda ilikuwa ni kusudio la Mungu ili Mungu afanye jambo jingine jipya katika maisha yangu.

KUONDOKA UTAWANI-Morogoro.

April 1999 nilimwandikia barua ya Kuachana na maisha ya Kitawa ya Ndugu wadogo wa Afrika padre Ricardo Maria ambaye ni Mkuu wa Shirika na bila hiana alikubali na kuniruhusu niondoke na nauli akanipa, nikapanda treni mpaka nyumbani Kahama. Mwaka huo huo wa 1999 nikajiunga na EVENING CLASSES yaani ODL KISHIMBA SEKONDARI na kusoma kidato cha kwanza mpaka cha Nne huku nikitumia Jina nililochukua Utawani la Padre Pio kwasasa ni Mtakatifu, jina hilo la kitawa nilipewa na Buruda Daud tukiwa Konvent ya kiroka. Hivyo nikawa DEOGRATIUS PIO KISANDU, hata hivyo nimeshafika kwa wakili na kuapa kuondoa jina hilo na kuweka jina la mzazi wangu mzee Nalimi yaani DEOGRATIUS NALIMI KISANDU. Hata hivyo mwaka 2007 nilitafta kituo cha kufanyia mtihani wa kidato cha sita nikapata kituo cha Tabora girls na kufanya mtihani wa kidato cha sita na mwaka 2008 nika resit tena Kituo cha kahama sekondari, pamoja na kupitia mafunzo ya uandishi wa habari, leseni ya ualimu yaani Induction Course na shahada ya maswala ya elimu maalum ndani yake nimesoma Uongozi na siasa. Yote haya na gharama zote ziligharamiwa na mama yangu mzazi na hakuna mtawa au Padre aliyetia mkono wake zaidi ya padre Artur mkapuchin aliyenisapoti kwa gharama za mavazi.

VIRAFRA NA WASEKULARI.

Nilipotoka utawani niliendelea kuwa chini ya Utawa wa tatu wa Wafransisko wasekulari yaani wateresiari nikilelewa chini yao kama VIRAFRA kwasasa VIFRA yaani Vijana rafiki wa Mtakatifu fransisko wa Asizi nikiwa Mwenyekiti wa VIRAFRA chini ya Uangalizi wa Marehemu Bruda Richard Kinyaruhama Ofm Capuchin.

UTUMIKIZI/USAIDIZI WA MISA KWA MAPADRE

Nimekuwa mtumikizi tangu mwaka 1992 baada ya kubatizwa katika Parokia ya kahama mjini mpaka mwaka 2002 nilipo hitimu kidato cha nne. Nimefanya kazi hii kwa muda mrefu sana chini ya Mapadre wafuatao Isaya, kadundu, Maziku na hayati Askofu Mateo Shija katika Parokia ya kahama mjini na jimbo la kahama ambao kimsingi ndio walikuwa walezi wetu miaka yote.

KUKANWA NA WATAWA WENZANGU.

Katika hali ya kushangaza sana nilipoanza kuonekana kisiasa na pia kupanda juu kielimu, watu walianza kuhoji ujio wangu hasa kipindi nilipotangaza kugombea urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania nikiwa mkoani Tanga, watawa wenzangu inasadikika walipoulizwa kama niliwahi kuwa mtawa walinikana kabisa kitu kilichosababisha mateso na kuonekana mimi ni muongo na mbabaishaji, hata kuzushiwa mambo mengine yasiyo ya msingi kwa Taifa. Nimekubali kudhalilika na kufedheheka ili Mungu ajitukuze kwa kukanwa. Mimi sija laaniwa ila wanaotengeneza laana ndio walio laaniwa. Nina washukru hata mapadre walio nilea hata wao wamenikana kuwa hawanijui ili hali wananijua. Nimekubali kuzodolewa kwakuwa nilikwisha achana na maisha hayo ya kitawa tangu mwaka 1999. Hali hii imesababisha kutoaminika sehemu nyingi na kucheleweshwa maisha yangu naya watoto wangu.

MAAMUZI MAGUMU.

Mimi ni mzazi na ni baba wa watoto huwezi kunilazimisha maisha ya kitawa wakati nilishaga toka miaka mingi sana. Nimelitumikia kanisa katika mambo mengi sana ya kijamii naya kiroho, kwa mjibu wa KATIBA ya Nchi ibara ya 19 kifungu kidogo cha 1 na cha 2 kina mpa ruhusa Mtanzania kubadilisha Dini au Dhehebu pia kubadili Imani ya kuabudu na kuwa huru katika imani yake. Kwa mantiki hiyo na tangaza rasmi leo kuwa Mimi kuanzia sasa sio Mkristu Mkatoliki tena, nimeamua kuungana na makanisa yanayoamini NGUVU ZA ROHO MTAKATIFI yaani UVUVIO WA ROHO MTAKATIFU, nitashirikiana na wakatoliki kwenye maswala ya kijamii ya kujenga nchi kama ninavyo shirikiana na waislamu kwenye Maswala ya kijamii ya kujenga nchi. Lakini kwenye swala la Kiimani kuanzia leo niko makanisa ya UVUVIO wa Roho Mtakatifu na hata wao wasipoonesha ushirikiano taanzisha Dhehebu langu likiwa chini ya UVUVIO WA ROHO MTAKATIFU. Siogopi kupigwa risasi wala kuvamiwa wala kuzomewa wala kutengwa kwani mmekwisha nitenga miaka mingi kwa kuninyima ushirikiano. Kuanzia leo kwa Damu ya Yesu na kula Kiapo kuwa mimi DEOGRATIUS NALIMI KISANDU jana tarehe 17 Oktoba 2016 nilijibatiza kwa Nguvu za Roho Mtakatifu kupitia Damu ya Yesu kwa maji mengi baada ya kuona wachungaji wanakuwa waoga kunibatiza, kwani Yesu angeweza kujibatiza lakini alimshinikiza Yohana ambatize, kwa kuwa nimekosa wa kunibatiza kwa maji mengi kisa wanaogopa vitisho basi nimebatizwa na Roho Mtakatifu mwenyewe kwa maji mengi. Ubatizo huu ni halali mbele za Mungu.

UHURU.

Naomba tena niachwe kuwa huru katika nchi yetu na taifa letu Tanzania na yeyote atakayetangulia mahakamani, mimi nitamtanguliza jela kwa Jina la Yesu. Mimi ni kanisa linalotembea THE MOVING CHURCH IN JESUS NAME. Nitajishughulisha na mambo yote ya kijamii ikiwemo Dini, Siasa za vyama, maisha ya kijamii n.k. Na mkitengeneza Deogratius Kisandu wa Kubumba mtakiona cha moto.

Ninawashukru wote ndani ya kanisa Katoliki mlionilea na mlioshirikiana na mimi katika mambo ya kidini, napokea mapingamizi yote maana ofisi yangu inatembea THE MOVING OFFICE. Sijamchokoza mtu bali nataka uhuru ndani ya Nchi yetu.

Ni mimi niliyekuwa Mkristu Mkatoliki na sasani Mkristu wa Nguvu za Roho Mtakatifu.

Mdharauliwaaaa,

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU

Mtumishi Mdogo sana wa Mungu.

18 Oktoba 2016

Ulitakiwa ufanye uamuzi ukiwa na moyo usio na kinyongo ili uwe na uamuzi huru na siyo kutokana na makovu ya utawani. Kwa baadaye, utajisikia vibaya na utajuta kwa nini uliacha.
 
Mantiki ya hii topic ni nini kwa anayeelewa??
Ninavyojua jua mimi waumini wengi wa madhehebu madogo wametokana na madhehebu yale makubwa. Honestly, sijaelewa issue hapo nini..
amekonfyuzi. sijui anamkomoa nani? Alidhani RC ni sawa na makanisa ya uamsho!
 
Fika salama uendako, nadhani mahali sahihi pa wewe kuabudu ni kwa Kibwetere, subiri huko alipo anasoma waraka wako atakuita nawe utaitika.
 
Back
Top Bottom