Nikamuona mfalme amekaa kwenye kiti chake cha enzi naye amejifika kwa mavazi ya fedha, aliyeshika mkononi kitu kama mti mkavu wenye moto wa kufisha.
Akauvunjavunja mti ule vikatokea vijiti viiiingi vyenye uwezo sawa na tabia za kufanana.
Vijiti vile akavigawa kwa kundi kubwa la watu wasioonekana, wote wakawa tayari kuvitumia pindi amri ikitolewa!
Vijiti vile vina miisho minne, ambayo hutoa moto uuao wote wamwaduo MUNGU.
Nikaona moto na kusikia kishindo kishindo kama cha mtu anakohoa mfululizo, mtu mmoja asiyeonekana aliyepewa kijiti kimoja aliamriwa kukitumi!
Alipigwa Mtumishi wa Mungu Ponda bali mauti haikupewa mamlaka juu yake.
Hapo awali Kijiti kilitumika kwa majaribio kikamuua yule askari shupavu Kombe!
Nikakiona kijiti maeneo ya dodoma kikiwa tayari kutumika, nao waliokibeba nikawatambua, mimi tu ili kukujuza wasioonekana hao!
Wakaifyatua mitego ya mioto ile kunielekea, lengo kuu ni kunipeleka kuzimu.
MUNGU akasimama kumkemea shetani pamoja na mfalme!
MALAIKA AKAPAAZA SAUTI KUU AKISEMA OMBENI MSIJE MKAINGIA MAJARIBUNI
Maana tazama wametumwa akina Wakudadavuwa, simiyu, kipara kipya, Barbarosa na Lemutuz ili kumfariji mfalme kwa kujikakamua kuficha uovu unaomchukiza MUNGU upeo.
====UFUNUO UNAENDELEA====