Kisheria hili jambo la mwanamke kung'ang'ania ndani limekaaje?

Kisheria hili jambo la mwanamke kung'ang'ania ndani limekaaje?

KASULI

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2020
Posts
599
Reaction score
677
Katika mizunguko ya dunia, Rafiki yangu alileta mwanamke kwake (mpenzi) si unajua mambo ya Vijana tena.

Sasa kwa maelezo yake ni kwamba huyo mwanamke ambaye wamefahamiana kama miezi minne hivi na amekuwa akija kwake mara kwa mara kutoka mkoani Geita yeye (jamaa) yuko Mwanza.

Sasa basi huyu msichana alienda kwao siku moja akarudi kwamba kafukuzwa na ameng'ang'ania kuwa hatoondoka labda amuue. Na Jamaa anadai hakuwahi kuwa malengo yake (Lengo lilikuwa kuchakata Mbususu) japo alikuwa anampoza kuwa atamuoa.

Hapa kuna mambo mawili.

1. Kisheria hili jambo limekaaje? Kuna hatua anaweza kuzifanya ili kumuondoa huyu mwanamke?

2. Ni kitu gani akifanye ilii kumtoa huyu mwanamke?

Binafsi nimemshauri amwambie ukweli kuwa hamtaki sasa uchaguzi ni wake abaki au aendelee kubaki.

NB. Toka arudi week moja sasa jamaa kila mtu anaishi kivyake umo ndani.

Zingatia: Sio mwanafunzi wala hana mimba.
 
Neno "import" umelitumia vibaya
Mwanza na Geita ume import vipi?

Kwa wataalamu wa masuala ya customs na freight forward and clearance tunasema hapo ume "carry coastwise"

Ku import ni kuingiza ndani ya Tanzania kitu kutoka nje ya Afrika Mashariki.

Halafu mwanadamu sio bidhaa, hawezi kuwa imported au exported
Vinginevyo utajikuta una kesi kama zumaridi ukitumia msamiati huo.
 
Neno "import" umelitumia vibaya
Mwanza na Geita ume import vipi?

Kwa wataalamu wa masuala ya customs na freight forward and clearance tunasema hapo ume "carry coastwise"

Ku import ni kuingiza ndani ya TZ kitu kutoka nje ya Afrika Mashariki.
Halafu mwanadamu sio bidhaa, hawezi kuwa imported au exported
Vinginevyo utajikuta una kesi kama zumaridi ukitumia msamiati huo.
Nisharekebishaaa.......
 
Yaan kuwa na mtu ambae anakujaa kumtembeleaa kama mpenzi wake anakaa siku mbili na anaondkaa, mara mkoa huu mara huu
Atumie busara tu kumuondoa huyo mwanamke, atoke na huyo mwanamke kwenda sehemu kisha yeye arudi hapo kwake bila huyo mwanamke kujua kisha afunge mlango kwa kufuli halafu aende sehemu yeyote ile alale hata siku 3 hivi,huyo mwanamke ataondoka mwenyewe,au baada ya siku 3 ahame hapo kama ni Nyumba ya kupanga.
 
Hivi mtu kama humpendi unawezaje kukaa nae ndani yaani akakuja na kurudi miezi minne yote? Matatizo mnayatafuta wenyewe.

Hilo swala analimaliza mwenyekiti wa mtaa ila mkae mkijua huyo dada ataondoka ila hawezi kukubali udhalilishaji huo.

Kama mwanaume hawezi kukaa chini wakalimaliza friendly atakata nguvu ya mwenyekiti ajiandae ila yajayo yanafurahisha.

Kama humpendi mtu usimkaribishe kwako, mkikutana huko hotelini ukaona sio chaguo lako, kata mawasiliano.

Jitu limejilia miezi minne ati halimtaki? Nyoooolo.

Afu ni wewe wacha kusingizia jamaa yako.
 
Yalishawahikunita mkuu mtu asikwambie sasa ngoma ilikuwa kwenye lugha maana nilikuwa taifa ilingine. Ngoma ilikuwa hivi: siku moja jumamosi nimetoka kibarua nikaona niende beach moja kupata upepo mwanana. Nikawa nimekaa kibanda fulan napata ya moto maana nitoka kuogelea na maji ya chumvi na yalikuwa ya baridi hatari siku hiyo.

Basi pale nilipokaa wakaja wadada watatu na vichupi vyao vya kuongelea basi nikawatizama kwa bashasha mara mdogo kashoboka akanisogelea sasa ngoma ikawa lugha mimi na lugha ya malikia mbovu yeye na vireno vyao . Basi nikawaagizia vinywaji wakapiga.

Siku hiyo tukaagana kila mtu kivyake tukapeana contact. Baada ya siku kama tatu nikakutana supermarket hapo tukafanya shopping naona anifuata baada ya kulipa naona tunangozana hadi kwenye gari nikaendesha gari kwa ustadi kwangu hapo mambo yakaanza akapewa ubatizo akaondoka kesho yake akarudi mida ya jioni akapewa kipaimara akasema anaomba kupumzika maana aniambia alikuwa chuo kikuu mwaka wa pili hivyo hawezi kwenda hostel ngoja apumzike kumbe ndio mbinu.

We kilichofuata mara natabulishwa kwa mama mkwe mara wale akina dada marafiki hataki tuzoeane nao nikamwambia nina mke Tanzania. Baada ya siku dem hataki kuondoka ikawa mbinde akamwita akata kula vindoge kijiua mara akachukua cable eti anajinyonga afie kwangu.

Kesho yake mama yake kaja eti kama namfukuza nimpatie haki yake maana ni biashara. Nikaona hawa masikini tu wakachukua jokofu walitaka kitanda na godoro.

Nilikuwa na tv yangu Kuna mtu akanitonya nitoe kabla wakati yule dada analeta vurugu jamaa akawa ameichukuwa ndio ikawa pona yake. Tokea siku hiyo abdalah kichwa wazi nimwambia atulie mambo ya kujifanya anachagua pisi kali zina madhara.
 
Yalishawahikunita mkuu mtu asikwambie sasa ngoma ilikuwa kwenye lugha maana nilikuwa taifa ilingine. Ngoma ilikuwa hivi: siku moja jumamosi nimetoka kibarua nikaona niende beach moja kupata upepo mwanana....
Noma, Nchi gani hiyo??
 
Hivi mtu kama humpendi unawezaje kukaa nae ndani yaani akakuja na kurudi miezi minne yote? Matatizo mnayatafuta wenyewe...
Mwenyekiti wa mtaa Analimalizaje...???
 
Neno "import" umelitumia vibaya
Mwanza na Geita ume import vipi?

Kwa wataalamu wa masuala ya customs na freight forward and clearance tunasema hapo ume "carry coastwise...
Lugha inakuwa na kupanuka haraka mno mkuu!

Siku moja nilikuwa bar napata ka-laga na rafiki yangu, akaja teja na kuliuliza dingi hii ngano shinda ya nani nataka kuzamia!

Nimebaki namshangaa, akachukua ile bia shinda kwenye glasi akanywa akaiweka ile glasi mezani na kuniambia kausha dingi na akaondoka![emoji56][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kesho yake mama yake kaja eti kama namfukuza nimpatie haki yake maana ni biashara. Nikaona hawa masikini tu wakachukua jokofu walitaka kitanda na godoro.
iyo mbususu bei gani, yani ndio kuchukua vyote hivyo.
 
Back
Top Bottom