Kisheria imekaaje serikali inapokataa kutambua kifo cha mtu?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Tanzania tuna taasisi ya kiserikali ya RITA ambayo moja ya majukumu yake ni kutambua na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa na vifo.

Kwa Tanzania na dunia ya leo, cheti cha kuzaliwa ni muhimu maana ndiyo msingi wa kwanza wa utambulisho wako kabla haujafika huko kwenye NIDA, leseni za udereva, passport, nk. Kwa hiyo haki ya kupata cheti cha kuzaliwa ni haki ya kila raia.

Sasa kinapokuja kifo, tunategemea haki hiyo hiyo itambulike.

Kumekuwa na mzozo kuhusu idadi ya vifo kutokana na MO29. Serikali kupitia kwa Tume cha Jaji Chande inasema waliokufa ni watu 518 wakati vyanzo vingine vinasema waliokufa ni zaidi ya watu 1,000 huku wengine wakiweka idadi ikifika watu 10,000.

Swali langu linakuja.

Kama ilivyo haki ya raia kutambulika kuwa amezaliwa na kupewa cheti cha kuzaliwa, hawa waliokufa kipindi cha MO29, wana haki yoyote ya kutambulika kuwa wamekufa kipindi hicho bila ya kujali sababu za vifo vyao?
 
Tatizo limeanzia pale ambapo serikali kupitia askari ndiyo waliofanya hayo mauaji ya halaiki na kama wakiyatambua itabidi kuwe na uwajibikaji
 
Serikali wnyw hawajitambui, PM anasema hawawezi kuhesabu watu waliokufa mana sio ng’ombe, hapo hapo idadi waliokufa serikali wanaisema
 
Kama unadhani kutambuliwa kuwa umekufa ni rahisi basi kuanzia leo mtu anaweza kuibuka na kusema kynez amekufa
 
nonsense 🐒
 
Kama wanaweza kupoka haki ya marehemu kutambulika kuwa ni marehemu, hawawezi kutumia sababu hiyo hiyo kwa kukataa kutambua walio hai kuwa ni hai?

Unapofungua njia ya uovu na udanganyifu, kunakuwa hakuna mwisho wa njia hiyo.

Walitunga sheria za takwimu lakini inaonekana kama wao watawala haziwahusu kuziheshimu.

Pia unafungua fursa za udanganyifu wa utambulisho maana watu wamekufa umekataa kuwatambua kuwa wamekufa. Kesho mtu anachukua identity ya marehemu utamlaumu nani?
 
Tena hayo ndiyo maafa makubwa
 
Back
Top Bottom