utaifakwanza
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 14,193
- 2,813
Spika anashughulikia mambo makubwa sio nyie
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mlinga Goodluck anawapatieni sana Wapinzani mpaka mnamzimia!!Ulishavunjika siku mtoto wa Celina Kombani alivyowatukana wabunge waupinzani na Naibu Spika na mwenyekiti wa wanawake wa Bunge akajisahau akapiga makofi
SPIKA ANASHUGHULIKIA MAMBO MAKUBWA SIO NYIE MNA DEAL NA UPUUZI UPUUZI
Mlinga Goodluck anawapatieni sana Wapinzani mpaka mnamzimia!!
Nafikiri it's time now haya maamuzi ya Spika yapelekwe Mahakamani kwenda kupata tafsiri kama ni sawa au la.
Ndugai has completely failed.
Nafasi aliyo nayo ya Uspika needs someone to be humble and not rude kama alivyo..
Alipo pale ni mgonjwa anaweza kuja kudondoka pale sababu ya kuwa too emotional... Mungu epushia mbali.
Kwa KKK kama wewe labda,mie nilishawadharau almost 90% ya wabunge wa CCM so labda kwenu wanaCCM
Mungu aepushie mbali! wakati mwingine kama jambo ni kwa manufaa ya wengi, sio mbaya kumuomba Mungu litimie. Unajua matendo aliyofanyiwa Mnyika yamemvunja moyo kiasi gani? na kuumia kwa Mnyika kumewafanya wananchi wa Kibamba wakose mangapi?
Nilikuwa nazungumza na mkazi mmoja wa Kimara ambaye sasa hivi wanapambana kuhakikisha nyumba zao hazibomolewi bila kulipwa fidia kwanza. Kasema Mnyika alikuwa anapambana pamoja nao kuhakikisha hilo la kulipwa kwanza linafanyika. Sasa anasema kwa jinsi alivyo vunjika moyo kwa aliyotendewa hawana haika kama ataendelea kusaidiana nao kwa moyo uleule. Na kama hilo halifanyiki, basi nyumba zaweza kuvunjwa bila fidia na wapo watu watapoteza maisha kwa mashinikizo ya moyo. Sasa kwa nini maisha ya Ndugai mmoja yawe na thamani kuliko makumi ya watu wanaoweza kupoteza kwa sababu yake?
Kama Mungu akiona vema "ampende zaidi" ili kuwaokoa wengi.
Who are you by the way? Do you have any impact in this country?Siku ukikua utaelewa kwamba Bunge ni letu wananchi siyo la CCM wala la Ndugai
Ndio unakimbilia kwa moderator? acha ujinga wewe!Pole sana,shidayako ni KKK!Na dalili inaonyesha kwenye maneno yako unashindwa kujenga hoja unakuja na vihoja
Umeandika vizuri ingawa nina wasiwasi na kushtakiwa kwa bunge.Nahisi bunge linaweza kustakiwa kwa mfano limeshindwa kumlipa mzabuni lakini si kwa maamuzi ndani ya bunge.
Kinachoweza kuombwa toka mahakamani ni tafsiri ya kanuni au sheria katika jambo lililofanywa ndani ya bunge.
Kwa hili la Ndugai na wabunge wawili binafsi naona Ndugai kachemka mnooo.Ghadhabu ilimjaa na tayari alishakuwa na maamuzii mdomoni na busara ikashindikana.
Nawaza tu,hivi Ndugai angesema hivi,"Mheshimiwa Mnyika nimemsikia aliyekuita mwizi lakini naomba uendelee kuchangia wakati taratibu zingine zikifanyika".Angepoteza nini?
Tunaambiwa tunajenga nyumba moja na tusigombee fito lakini si kweli,tunagawanyika katika kasi ya ajabu!!
Hivi ule umoja wa kinamama wabunge bado upo?
Liondolewe tuu mana kazi yake haina product yeyote kwa mustakabali wa nchi yetu!Wanabodi,
Nilipasema Rais wa JMT anaweza Kuondolewa madarakani na Bunge, wengi walibeza kuwa nilikuwa nazungumzia hypothetical situation, yaani kitu ambacho hakipo, nikauliza hakipo vipi wakati kipo kwenye Katiba yetu?, sema haijatokea tukapata rais wa kulazimika Kuondolewa.
Leo ninazungumzia Kuondolewa kwa Spika wa Bunge la JMT. Kuna watu wanadhani mtu akiishachaguliwa kuwa Spika wa Bunge, basi anageuka mungu mtu, anaweza kufanya lolote na asiguswe!. No!. Nafasi ya Spika ipo kwa mujibu wa Katiba, na atatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba, sheria, taratibu na kanuni, akikiuka na ikathibitishwa amekiuka, Spika anaondolewa!. Swali ni Jee Spika Mhe. Ndugai amekiuka Katiba, sheria, taratibu na kanuni kustahili Kuondolewa? .
Declaration of interest.
Mimi ni muumini wa Katiba, unauhusisha uendeshaji wa nchi kwa mujibu wa Katiba kwa kutumia sheria, taratibu na kanuni.
Naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kufuatia bandiko hili
Tundu Lissu apinga vikali adhabu ya Mdee na Bulaya,
Tanzania ni nchi inayofuata Katiba kwa kuzingatia misingi ya haki, kuwa "no one is above the law" kumaanisha Katiba ndio the supreme law, hakuna yoyote aliye juu ya Katiba na sheria.
Chini ya Katiba hiyo, tunayo mihimili mitatu, ya Serikali, Bunge na Mahakama ambayo yote inapaswa kuwa huru kwa kutenda bila kuingiliwa na mihimili mingine (independently) lakini wakati huo huo kila mihimili ukiwa na majukumu ya kutenda kwa mujibu wa Katiba, ikitokea mihimili mmoja umekiuka mamlaka yake, then hii mihimili mingine ina jukumu la kuufanyia checks and balance.
Hii inaitwa "the doctrine of separation of powers".
Bunge lina jukumu la kutunga sheria, Mahakama inatafsiri sheria na Serikali inatekeleza sheria.
Serikali inatakiwa kuliwezesha Bunge na Mahakama ikiwemo kulidhibiti Bunge kupitia mamlaka ya rais kuteua mtendaji mkuu wa Bunge ambaye ni katibu wa Bunge.
Serikali inaidhibiti Bunge kwa kuridhia sheria zinazotungwa na Bunge haziwi sheria hadi mkuu wa serikali aridhie, na asiporidhia rais ana mamlaka ya kulivunja Bunge.
Serikali pia inawajibu wa kuihudumia Mahakama kwa kuiwezesha ila pia kulidhibiti kwa kuteua Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Jaji Mkuu lakini haiwezi kumuondoa, ila pia serikali inaidhibiti Mahakama kwa kusaini hati za capital punishment.
Bunge kwa upande wake lina jukumu la kuisimamia Serikali na Mahakama kwanza kwa kuitungia sheria, kupitisha bajeti zao, na kuisimamia matumizi yake.
Serikali inapokosea kwa kukiuka mamlaka yake, inashitakiwa Mahakamani au bungeni, na mkuu wa mihimili huu wa Serikali akienda kinyume cha Katiba, anashitakiwa na Bunge na kufukuzwa kazi kupitia "impeachment process"
Kama serikali inaweza kushitakiwa Mahakamani, Mahakama inashitakiwa Bungeni na Serikalini, Jee Bunge haliwezi kushitakiwa Mahakamani?.
Serikali imewahi kushitakiwa mahakamani mara kibao tuu na ikashindwa. Sina kumbukumbu ya Mahakama kushitakiwa nje ya Mahakama, nakumbuka zile kesi za Mtikila, lakini Bunge la Tanzania halijawahi kushitakiwa mahakamani.
Hii ya Bunge kutokushitakiwa kumemfanya Mkuu wa Mhimili huu kujisahau na kujiona mungu mtu hivyo anaweza kutoa maamuzi yoyote hata yaliyo kinyume cha sheria, taratibu na kanuni na asiguswe!.
Adhabu kwa Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya now goes down to history books za Bunge letu kwa mara ya kwanza kushitakiwa mahakamani if at all kesi itafunguliwa kweli.
Kwa kumbukumbu zangu mtu pekee mwenye kinga ya kisheria ya kutokushitakiwa mahakamani ni Rais wa JMT pekee, hivyo serikali Inashitakika, Mahakama Inashitakika swali ni Jee Bunge nalo pia Linashitakika?!.
Mihimili hii ya dola inaongozwa na binadamu ambao sio malaika na wanaweza kukosea, ikitokea wakuu wa mihimili hii kukosea, sheria imeweka utaratibu wa jinsi ya kumuondoa rais, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge. Swali ni Jee Spika wa Bunge Job Ndugai aondolewe?.
Kwa vile utaratibu wa kumuondoa spika ni kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni, kwa vile mimi sio mwanasheria, naomba niwakabidhi kwa mmoja wa wanasheria wetu humu jf,
Mkuu The Learned Brother
Petro E. Mselewa
ili muweze kupata vifungu vya sheria, kanuni na utaratibu was kumuondoa spika .
Spika anaondolewa hivi...
Paskali
Rejea
Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika!
Vurugu za Jana Bungeni: Chanzo ni Mhe. Job Ndugai!- Ni Dikteta Hatari Kuliko Spika Anne Makinda!.
Nani Zaidi Kati ya Bunge na Mahakama?!. The Doctrine of Separation of Powers is it Nothing, Just a Myth? ...
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki ...
Bunge Litii Mahakama; Lisipotii Nani Aitii Basi? | Page 15 ...