Kisheria, Spika wa Bunge anaweza kuondolewa. Je, Job Ndugai aondolewe?

Ulishavunjika siku mtoto wa Celina Kombani alivyowatukana wabunge waupinzani na Naibu Spika na mwenyekiti wa wanawake wa Bunge akajisahau akapiga makofi
Mlinga Goodluck anawapatieni sana Wapinzani mpaka mnamzimia!!
 
Mkuu mwandishi hiyo ni nadharia tu haina uhalisia ktk siasa za nchi yetu ambapo (1)chama tawala ndicho chama chenye wabunge wengi tena kwa kiasi kikubwa sana, (2) raisi na mwenyekiti wa chama tawala kuwa na mamlaka hadi uwezo kikatiba wa kulivunja bunge akiona inafaa kufanya hivyo.
 

Mungu aepushie mbali! wakati mwingine kama jambo ni kwa manufaa ya wengi, sio mbaya kumuomba Mungu litimie. Unajua matendo aliyofanyiwa Mnyika yamemvunja moyo kiasi gani? na kuumia kwa Mnyika kumewafanya wananchi wa Kibamba wakose mangapi?

Nilikuwa nazungumza na mkazi mmoja wa Kimara ambaye sasa hivi wanapambana kuhakikisha nyumba zao hazibomolewi bila kulipwa fidia kwanza. Kasema Mnyika alikuwa anapambana pamoja nao kuhakikisha hilo la kulipwa kwanza linafanyika.

Sasa anasema kwa jinsi alivyo vunjika moyo kwa aliyotendewa hawana haika kama ataendelea kusaidiana nao kwa moyo uleule.

Na kama hilo halifanyiki, basi nyumba zaweza kuvunjwa bila fidia na wapo watu watapoteza maisha kwa mashinikizo ya moyo. Sasa kwa nini maisha ya Ndugai mmoja yawe na thamani kuliko makumi ya watu wanaoweza kupoteza kwa sababu yake?

Kama Mungu akiona vema "ampende zaidi" ili kuwaokoa wengi.
 
Kwa KKK kama wewe labda,mie nilishawadharau almost 90% ya wabunge wa CCM so labda kwenu wanaCCM

Unawadharau CCM hao upinzani wanafanya nini cha maana? Mmejaza makapi ya CCM hao hao unaowadharau na wengine mpaka mmewapa kugombea Urais!
 

Utaombeaje Ndugai afe kwa sababu ya kusimamia kanuni za bunge? Bunge lazima liheshimiwe siyo kilabu cha pombe. Nidhamu hata kwa baba yako iko pale pale. Kama mnaleta dharau lazima mshughulikiwe.

Na mimi nasema adhabu waliyopewa ni ndogo sana. Naamini itaongezwa wakirudia tena! Ndio maana tulizuia maandamano kwa sababu ya kuleta nidhamu na utulivu ili watu wafanye mambo ya maana!
 
Spika hata aondolewe bado tatizo litakuwa palepale. Tatizo sio Spika tatizo ni hizo sheria za Bunge zinazompa Spika mamlaka ya kufanya hivo. Huyu hata mkimwondoa atakuja mwingine atafanya hivohivo maana ndio mwongozo wake.

My intake. Tusikomae tu na Spika Wabunge nao wajirekebishe, unajua kuongoza watu wazima ni kazi sana, imagine kila siku wabunge wengine wafanye kama ilivyokuwa kwa Mdee na Bulaya na Spika akae kimya si tutasema Bunge limemshinda? Hebu tuweni neutral tuone mengi
 

Umeongea kwa hekima sana Mungu kuongezee
 
Paskali mbona swali lako ni fupi tu? Naam, spika anaweza kuondolewa kwa kura ya wabunge kutokuwa na imani naye. Na Waziri Mkuu hivyohivyo.

Na hata Rais kuna sheria ya impeachment anaweza kung'olewa na Bunge. What is your problem exactly? Ila ni vizuri kukutonya kuwa katika hali ya kawaida Spika hafukuzwi kwa kumtoa Halima Mdee kwa makosa yasiyoisha, ila of course wabunge wakiona Mdee hana kosa, basi watapiga hiyo kura.

Si huyo tu, Wabunge wakiona kuwa Rais katenda kosa kuzuia wizi wa madini kwenye mchanga, basi nao watamng'oa halafu watamuweka Rais anayeruhusu wizi huo. Kwa kifupi, inahitaji MAJORITY ya wabunge, si wawili au watatu, si Mnyika na Tindulissu tu: they must be 400 plus.
 
Take a timu to know traditionally how solve our issues, disputes, and problems - hatujafika wakati huo
 
Liondolewe tuu mana kazi yake haina product yeyote kwa mustakabali wa nchi yetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…