Kishindo cha Rais Magufuli katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa

Kishindo cha Rais Magufuli katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa

Miaka Mitano ya Magufuli Serikali ... iliweza kupokea viongozi wa nchi na Taasisi mbalimbali za kimataifa, ikiwemo Vietnam, India, Uturuki, Afrika Kusini, DRC, Ethiopia, Misri, Rwanda, Zambia, Zimbabwe, Uganda, IMF, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, IFAD na kadhalika.

Miaka mitano ya Magufuli, Serikali imefungua Balozi mpya 8 (Algeria, Cuba, Israel, Korea, Qatar, Namibia, Sudan na Uturuki) na nchi mbili za Ethiopia na Poland pia zimefungua Balozi zao hapa nchini.

Miaka mitano ya Magufuli Serikali imeendelea kushiriki katika shughuli na mipango mbalimbali ya kimataifa, ikiwemo ulinzi wa amani, ambapo kwa sasa Serikali ina askari wapatao 2,303 katika nchi za DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Lebanon, Sudan na Sudan Kusini.

Miaka mitano ya Magufuli Tanzania imeaminiwa kuongoza Jumuiya mbili za kikanda, Jumuiya ya Afrika Mashariki kuanzia 2016 hadi 2017 na pia kuongoza Jumuiya ya SADC kuanzia Agosti 2019 hadi mwezi Agosti 2020 yenye jumla ya nchi 16.

Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Afrika Kusini, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Botswana, Angola, Lesotho, DRC, Visiwa vya Madagascar, Comoro na kadhalika zinazokadiriwa kuwa na takribani watu milioni 300 na moja ya mafanikio ambayo Tanzania iliyapata katika kuongoza Taasisi hizi, ni kuzishawishi Nchi Wanachama kuridhia lugha ya Kiswahili kutumika kwenye Taasisi hizo.

Miaka mitano ya Magufuli, biashara ya Tanzania, katika nchi za nje imeongezeka kutoka shilingi trilioni 11.5 mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi trilioni 16.6 mwaka 2018/2019.

Miaka mitano ya Magufuli, Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwenye masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mfano, kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutoka mwaka 2015 hadi mwaka 2018, Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwa wastani wa Dola za Marekani milioni 288.04.

Miaka mitano ya Magufuli Kuhusu uwekezaji, Kituo cha Uwekezaji cha Tanzania kimesajili miradi mipya 1,307 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 14.607, zaidi ya shilingi trilioni 30, na itakapokamilika itatoa ajira 183,503.

Miaka mitano ya Magufuli, Sekta ya utalii imeimarika jambo ambalo limepelekea idadi ya watalii na mapato ya nchi kuongezeka. Kwa mfano, mwaka 2019 tulipokea watalii 1,510,151 kutoka watalii 1,137,182 mwaka 2015. Aidha, mapato yaliongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.9 mwaka 2015 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 2.6 mwaka 2019.

28 Oktoba, 2020 hima tukachague Maendeleo, Tukachague Chama Cha Mapinduzi na tukamchague Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Ni takwimu ambazo viongozi wa upinzani hawatamani jamii ya wapiga kura wazisikie ila kashfa za uzushi dhidi ya Rais aliyeko madarakani
 
Mataifa gani hayo aliyo na mashirikiano nae wakati hana hata mkutano mmoja wa umoja wa mataifa alioshiriki

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app

Angewezaje kuaminiwa kushika nafasi ya uenyekiti kwenye Jumuiya za EAC na SADC kama hana mahusiano nao? Na kiufupi tu Jumuiya kama ya SADC inajumuisha nchi 16 zenye takribani watu milioni 300, au ulitaka aende Ulaya pekee ndiyo useme kwamba ana Uhusiano wa kimataifa ??
 
Rais anajivunia kutosafiri nje.

Miaka mitano hajahudhuria kikao hata kimoja cha UN General Assembly , AU Summit, Commonwealth Heads of Government Meeting wala hata World Economic Forum Davos.

Hatujawahi kuwa na rais anayejifungia ndani kama mwali kama huyu.

Moja ya kazi za rais ni kuwakilisha nchi kimataifa. Magufuli hii kazi kaikwepa kabisa.

Umeongelea kuimarishwa kwa uhusianonwa kimataifa na Tanzania kupokea viongozi wa nchi nyingine.

Katika diplomasia, kuna kanuni moja ya muhimu sana, inaitwa "reciprocity".

Yani, ukitembelewa na wenzio, na wewe uwatembelee. Ukioewa zawadi, na wewe utie.

Siyo unasubiri wewe kutembelewa tu. Ukisubiri kutembelewa tu, hilo linachukuliwa kama kudharau wenzako.

Magufuli kwa nini anajivunia kujifungia Tanzania?
Ss kam kila tukio Raisi aende nje mabalozi itakua kazi yao nn?
Mbona hao maraisi wa Ulaya hatuwaoni kuzurura zurura ovyo?
Nyinyi mnanongwa tu na visokolokwinyo,
Mhe JK alivokua anasafr safr mkasema raisi gan kila cku safar, JPM hatoki toki mnalalamka tena, eeh, nyie watu wavip!
 
Hizo hata sio cheche tumeshasikia hivyo visingizio mara nyingi toka mwaka 2016.

Unajua Trump amesafiri kwenda nchi ngapi toka amekuwa Rais ? Labda utafute mfano wa mtu mwingine

Mwaka 2017 ameenda nchi hizi: Saudi Arabia, Israel, Palestine, Italy, Vatican City, Belgium, Italy, Poland, Germany, France, Japan, South Korea, China, Vietnam, Phillippines.

Mwaka 2018 ameenda nchi hizi : Switerland, Canada, Belgium, United Kingdom, Finland, Argentina, Iraq, Germany

Mwaka 2019 ameenda nchi hizi: Vietnam, Japan, United Kingdom, Ireland, France, South Korea, North Korea, France, Afghanistan.

Na hizo zote ni strategic kuna vitu anavyotafuta kuweka influence katika sehemu muhimu duniani, bado marais wengine wanaokuja kutembeza bakuli kwake.

Kwenye suala la mahusiano ya kimataifa aseme tu ni changamoto ataishughulikia basi, tusifiche madhaifu mbona kuna mengine mazuri ameyafanya humu humu ?

Ni kama kuna mshikaji mmoja tulikuwa tunasoma naye chuo alikuwa anajidai yeye sio mtu wa mademu anataka tu asome afaulu, maisha yalikuwa darasani, hostel, cafeteria, kumbe alikuwa domo zege na anahangika na msongo wa mawazo mwisho wa siku hata kitabu kilishindwa kumwendea vizuri.
 
Wape salaam.
 
..aache kutudanganya.

..mbona alikimbia tafrija na mabalozi wa nchi za nje inayofanyika kila mwaka?

..huyu hajiamini kukutana na viongozi wa nje.
 
Nani mzalendo nchi hii kama Mwl. Julius Kambarage Nyerere? Nyerere hakuwahi kukosa kuhudhuria kikao chochote cha UN au OAU! Na, yeye in person, alituwakilisha vyema mno hadi tukaona fahari kuitwa watanzania.

Nyerere amefanya dhifa nyingi sana za kitaifa pale Ikulu kuwakaribisha viongozi mbalimbali wa mataifa kuitembelea nchi yetu. Nyerere amehudhuria mikutano mingi sana ya kikanda - SADC, NAM, n.k. yeye binafsi bila kutuma mwakilishi na alijibu maswali yasiyojibika kwa weledi mkubwa!

Baada ya kustaafu, Nyerere amehudhuria na ku-chair mikutano isiyo na idadi kimataifa; amehutubia mabunge (mf. lile la South Africa), n.k. Kujenga nchi sio kutohudhuria shughuli za kimataifa; hata hao wanaotumwa kuwakilisha (VP, PM, n.k.) nao wanajenga nchi vile vile.
 
Pamoja na kwamba diplomasia sio kwenda ulaya lakini kuhudhuria mikutano ni muhimu lakini kuvuruga mahusiano huku umejifungia sio diplomasia ,unavurugana na kila jirani ndio diplomasia gani?
Kwani kutoenda Ulaya kumepunguza gharama za kusafiri au utawala ambazo zilikuwa zinalalamikiwa?
Mtu hajui lugha ya kimataifa anasingizia kujenga nchi 😆😆😆😆😆
 
Kujenga nchi ni pamoja na kuhudhuria mikutano ya Kimataifa yenye faida kwa nchi yako kwa hadhi ya ukuu wa nchi
Hiyo mikutano makaburasha aweza kukuletea balozi ni kumwambia ongea hiki na hiki basi vinginevyo ni safari tu za kuzipelekea hoteli zao pesa tu za kula na kulala
 
Nani mzalendo nchi hii kama Mwl. Julius Kambarage Nyerere? Nyerere hakuwahi kukosa kuhudhuria kikao chochote cha UN au OAU! Na, yeye in person, alituwakilisha vyema mno hadi tukaona fahari kuitwa watanzania.

Nyerere amefanya dhifa nyingi sana za kitaifa pale Ikulu kuwakaribisha viongozi mbalimbali wa mataifa kuitembelea nchi yetu. Nyerere amehudhuria mikutano mingi sana ya kikanda - SADC, NAM, n.k. yeye binafsi bila kutuma mwakilishi na alijibu maswali yasiyojibika kwa weledi mkubwa!

Baada ya kustaafu, Nyerere amehudhuria na ku-chair mikutano isiyo na idadi kimataifa; amehutubia mabunge (mf. lile la South Africa), n.k. Kujenga nchi sio kutohudhuria shughuli za kimataifa; hata hao wanaotumwa kuwakilisha (VP, PM, n.k.) nao wanajenga nchi vile vile.
Hayo yalikuwa ya Nyerere usiwe mtumwa wa historia kila zama zina kitabu chake na kila kitabu cha somo huwa kina new edition .Huwezi komalia toleo la kitabu ulilosoma wakati wa Nyerere tu.Kuna new edition
 
Magufuli anawapa shida sana chadema. Waonee huruma baba watakosa hata diwani.
 
Hakika jiwe Linaendelea kusagika kweli kweli.
Kwahiyo yeye anajua kusafiri nje ya nchi ndio kujenga Diplomasia?????

Kama hafuati sheria za kimataifa, mahusiano mazuri na majirani , haki za Binadamu , uhuru wa vyombo vya habari ndio ana zidi kuizika diplomasia.

Huyu kweli alisukumizwa kuwa rais kama anavyodai
 
Back
Top Bottom