Kishindo cha Rais Magufuli katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa

Kishindo cha Rais Magufuli katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa

Mwaka 2017 ameenda nchi hizi: Saudi Arabia, Israel, Palestine, Italy, Vatican City, Belgium, Italy, Poland, Germany, France, Japan, South Korea, China, Vietnam, Phillippines.

Mwaka 2018 ameenda nchi hizi : Switerland, Canada, Belgium, United Kingdom, Finland, Argentina, Iraq, Germany

Mwaka 2019 ameenda nchi hizi: Vietnam, Japan, United Kingdom, Ireland, France, South Korea, North Korea, France, Afghanistan.
Kwa miaka yote mitatu uliyotaja hakuna nchi hata moja ya Africa Raisi Trump aliyotembelea sasa sisi tukazurure Marekani kutafuta nini ? Balozi yuko kule anatosha
 
Hayo yalikuwa ya Nyerere usiwe mtumwa wa historia kila zama zina kitabu chake na kila kitabu cha somo huwa kina new edition .Huwezi komalia toleo la kitabu ulilosoma wakati wa Nyerere tu.Kuna new edition
... diplomasia ni kati ya mambo yamekuwepo tangu kale, yapo, na yataendelea kuwepo hadi ukamilifu wa dahari! Msemaji rasmi wa nchi kimataifa ni rais wa nchi. Hakuna siku mahusiano hususan kujenga mahusiano mema na mataifa mengine yatakoma eti ni "historia".
 
Kwa miaka yote mitatu uliyotaja hakuna nchi hata moja ya Africa Raisi Trump aliyotembelea sasa sisi tukazurure Marekani kutafuta nini ? Balozi yuko kule anatosha
Marekani si kwa Trump tu.

Makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako New York City.

Hapo viongozi wote wa dunia nzima huwa wanakutana kila mwaka mwezi wa September.

Katika mkutano unaitwa United Nations General Assembly.

Miaka mitano yote ya utawala wa Magufuli hajaenda.

Unaelewa hilo?
 
Raisi Magufuli awashangaa wanaodhani kujenga diplomasia ya mahusiano ya kimataifa ni kufanya safari za kwenda ulaya!!

Raisi Magufuli atema cheche asema asema ana mialiko ila hataenda atatuma balozi yeye anajenga nchi

Ninakubaliana naye Uingereza na Marekani wana mahusiano mazuri sana na nchi nyingi tu ya kimataifa na nchi nyingine duniani lakini huwezi waona MALKIA AU WAZIRI mkuu wa Uingereza au Raisi Trump wa MAREKANI kutwa wanaburuza masanduku yenye magurudumu yenye nguo zao airports wakienda kuzurura huko na huko nchi mbalimbali kujenga diplomasia ya mahusiano ya kimataifa iwe Kenya au Ubelgiji alikoenda Lisu au Dubai alikoenda Membe

Nchi haijengwi kwa kuchoma nyavu halali
 
Hii ya ndani kaishindwa vipi kuhusu ya nje.😁😁
IMG-20200902-WA0014.jpg
 
Ss kam kila tukio Raisi aende nje mabalozi itakua kazi yao nn?
Mbona hao maraisi wa Ulaya hatuwaoni kuzurura zurura ovyo?
Nyinyi mnanongwa tu na visokolokwinyo,
Mhe JK alivokua anasafr safr mkasema raisi gan kila cku safar, JPM hatoki toki mnalalamka tena, eeh, nyie watu wavip!
Kwani wapi nimesema aende kila tukio?

Unajua kusoma kwa ufahamu?
 
Marekani si kwa Trump tu.

Makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako New York City.

Hapo viongozi wote wa dunia nzima huwa wanakutana kila mwaka mwezi wa September.

Katika mkutano unaitwa United Nations General Assembly.

Miaka mitano yote ya utawala wa Magufuli hajaenda.

Unaelewa hilo?
Mkutano ni mkutano tu uwe wa umoja wa mataifa au kikao cha harusi
kwa teknolojia iliyopo na corona zilizoko huko Marekani mtu waweza fuatilia mkutano online,ukatoa comment na decisions online kama kuna mtu anatakiwa Live mkutanoni unamwambia tu balozi nenda watsap me ukiona chochote kinachotaka decision nikurushie jibu kwenye namba yako ya watsapp uwajibu humo mkutanoni .Mimi niendelee na mambo mengine
 
Mada ya kijinga kabisa. Yani Magufuli kafungamana na madikteta ndiyo unasema kishindo?

Kiongozi gani wa nchi hajawahi kushiriki baraza lolote lile la umoja wa mataifa!
tulikuwa na wa namna hiyo lkini tulishuhudia mpaka wanyama wetu nao wakisafirishwa kwenda huko, na hata hivyo ni ninyi mlizomea Sana mtindo wa Raisi kusfiri nje, inakuweje mkuu kila mtindo wa viongozi wetu kwenu ni matatizo?
 
Wanakuwa na mitindo too much! Yani nyie viongozi wenu sijui mnawatoa wapi!
 
Yote haya ni kwa sababu Mh Lissu amewa chokonoa kisawa sawa ,hebu tuhodhoreshee ni kwa namna gani kama Nchi tumefaidika na haya mahusiano Mkuu.Wakati wa Mh Mkapa (R.I.P.) na Mzee wetu Jakaya tulipata wlaau nafuu ya kusamehewa baadhi ya Madeni yetu kwa Sehemu kubwa ,vipi kwa Mzee Jiwe Deni letu linazidi kukua pamoja na Mahusiano mazuri uliyo yataja hapa !!?..

Nna subiri Majibu Mkuu.
Ni kweli Lissu kachokonoa kwa kueneza yaliyo uzushi mtupu. Uzushi ukiachwa usambae unakuwa ukweli

Isitoshe, mwenye "pressure" ni Lissu. Mwanzo wa Kampeni zake alikuwa na ugomvi na Tume, kisha vyombo vya habari, na kwa mbali Rais Magufuli.

Baada ya kuona Serikali haistuki na mikwara yake hiyo jukwaani, na wagombea wa CCM wabajikita na hoja za maendeleo zibazojibu jibu baadhi ya uzushi wake, akamua kuporomosha tuhuma za uzushi dhidi ya Tume na Magufuli.

Nia yake jukwaani ni kuilazimisha Serikali imchukulie hatua akinukishe kwani hakuna shaka, kwa pesa kidogo tu, wapo vijana ambao wako tayari kufanya vurugu wakiagizwa kufanya hivyo.

Ushauri kwa Serikali ni kumwacha aendelee na mikwara yske hiyo, jamii ya wastaarabu watamwadhibu kwa kura.
 
Miaka Mitano ya Magufuli Serikali imeimarisha uhusiano na ushirikiano na Mataifa ya nje pamoja na taasisi za kimataifa. Hii ndiyo sababu Serikali iliweza kupokea viongozi wa nchi na Taasisi mbalimbali za kimataifa, ikiwemo Vietnam, India, Uturuki, Afrika Kusini, DRC, Ethiopia, Misri, Rwanda, Zambia, Zimbabwe, Uganda, IMF, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, IFAD na kadhalika.

Miaka mitano ya Magufuli, Serikali imefungua Balozi mpya 8 (Algeria, Cuba, Israel, Korea, Qatar, Namibia, Sudan na Uturuki) na nchi mbili za Ethiopia na Poland pia zimefungua Balozi zao hapa nchini.

Miaka mitano ya Magufuli Serikali imeendelea kushiriki katika shughuli na mipango mbalimbali ya kimataifa, ikiwemo ulinzi wa amani, ambapo kwa sasa Serikali ina askari wapatao 2,303 katika nchi za DRC, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Lebanon, Sudan na Sudan Kusini.

Miaka mitano ya Magufuli Tanzania imeaminiwa kuongoza Jumuiya mbili za kikanda, Jumuiya ya Afrika Mashariki kuanzia 2016 hadi 2017 na pia kuongoza Jumuiya ya SADC kuanzia Agosti 2019 hadi mwezi Agosti 2020 yenye jumla ya nchi 16.

Nchi hizo ni pamoja na Tanzania, Afrika Kusini, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Botswana, Angola, Lesotho, DRC, Visiwa vya Madagascar, Comoro na kadhalika zinazokadiriwa kuwa na takribani watu milioni 300 na moja ya mafanikio ambayo Tanzania iliyapata katika kuongoza Taasisi hizi, ni kuzishawishi Nchi Wanachama kuridhia lugha ya Kiswahili kutumika kwenye Taasisi hizo.

Miaka mitano ya Magufuli, biashara ya Tanzania, katika nchi za nje imeongezeka kutoka shilingi trilioni 11.5 mwaka 2014/2015 hadi kufikia shilingi trilioni 16.6 mwaka 2018/2019.

Miaka mitano ya Magufuli, Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwenye masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mfano, kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutoka mwaka 2015 hadi mwaka 2018, Tanzania imekuwa na urari chanya wa mauzo ya bidhaa kwa wastani wa Dola za Marekani milioni 288.04.

Miaka mitano ya Magufuli Kuhusu uwekezaji, Kituo cha Uwekezaji cha Tanzania kimesajili miradi mipya 1,307 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 14.607, zaidi ya shilingi trilioni 30, na itakapokamilika itatoa ajira 183,503.

Miaka mitano ya Magufuli, Sekta ya utalii imeimarika jambo ambalo limepelekea idadi ya watalii na mapato ya nchi kuongezeka. Kwa mfano, mwaka 2019 tulipokea watalii 1,510,151 kutoka watalii 1,137,182 mwaka 2015. Aidha, mapato yaliongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.9 mwaka 2015 hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 2.6 mwaka 2019.

28 Oktoba, 2020 hima tukachague Maendeleo, Tukachague Chama Cha Mapinduzi na tukamchague Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Miaka mitano ya Magufuri ndio kumekua na makampuni (agents) wengi wakuagiza mizigo na magari nje ya nchi, na watu wanaagiza kila iitwapo leo. Hii nitafsiri tosha kua tunakua kiuchumi na hata kwa pato la mtu mmoja mmoja.
 
Mkutano ni mkutano tu uwe wa umoja wa mataifa au kikao cha harusi
kwa teknolojia iliyopo na corona zilizoko huko Marekani mtu waweza fuatilia mkutano online,ukatoa comment na decisions online kama kuna mtu anatakiwa Live mkutanoni unamwambia tu balozi nenda watsap me ukiona chochote kinachotaka decision nikurushie jibu kwenye namba yako ya watsapp uwajibu humo mkutanoni .Mimi niendelee na mambo mengine
Magufuli hajatoa hotuba UN General Assembly hata online.

Point yako ingekuwa na nguvu kama angekuwa katoa hotuba online ila hajaenda.
 
Raisi Magufuli awashangaa wanaodhani kujenga diplomasia ya mahusiano ya kimataifa ni kufanya safari za kwenda ulaya!!

Raisi Magufuli atema cheche asema asema ana mialiko ila hataenda atatuma balozi yeye anajenga nchi

Ninakubaliana naye Uingereza na Marekani wana mahusiano mazuri sana na nchi nyingi tu ya kimataifa na nchi nyingine duniani lakini huwezi waona MALKIA AU WAZIRI mkuu wa Uingereza au Raisi Trump wa MAREKANI kutwa wanaburuza masanduku yenye magurudumu yenye nguo zao airports wakienda kuzurura huko na huko nchi mbalimbali kujenga diplomasia ya mahusiano ya kimataifa iwe Kenya au Ubelgiji alikoenda Lisu au Dubai alikoenda Membe

Ukweli mchungu
 
Kishindo gani ameonyesha huyo mshamba na limbukeni mkubwa, labda kuteka watu na kuua wasio na hatia. Mshamba na muuaji mkubwa, taahira huyo.
Punguza makali, haina haja ya kukejeli, kutuhumu bila udhibitisho, unaweza kuonyesha tu haukibaliani nae kwa lugha ya kiungwana zaidi!
 
Danganyeni wasiojielewa.Mnatumia nguvu nyingi kutakatisha kaniki.
 
Chadema wakishika dola ikulu itahamia Ubelgiji ili kudhihirisha kuimarika kwa uhusiano wa kimataifa.
 
Back
Top Bottom