Kishindo cha Rais Magufuli katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa


Ni takwimu ambazo viongozi wa upinzani hawatamani jamii ya wapiga kura wazisikie ila kashfa za uzushi dhidi ya Rais aliyeko madarakani
 
Mataifa gani hayo aliyo na mashirikiano nae wakati hana hata mkutano mmoja wa umoja wa mataifa alioshiriki

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app

Angewezaje kuaminiwa kushika nafasi ya uenyekiti kwenye Jumuiya za EAC na SADC kama hana mahusiano nao? Na kiufupi tu Jumuiya kama ya SADC inajumuisha nchi 16 zenye takribani watu milioni 300, au ulitaka aende Ulaya pekee ndiyo useme kwamba ana Uhusiano wa kimataifa ??
 
Ss kam kila tukio Raisi aende nje mabalozi itakua kazi yao nn?
Mbona hao maraisi wa Ulaya hatuwaoni kuzurura zurura ovyo?
Nyinyi mnanongwa tu na visokolokwinyo,
Mhe JK alivokua anasafr safr mkasema raisi gan kila cku safar, JPM hatoki toki mnalalamka tena, eeh, nyie watu wavip!
 
Hizo hata sio cheche tumeshasikia hivyo visingizio mara nyingi toka mwaka 2016.

Unajua Trump amesafiri kwenda nchi ngapi toka amekuwa Rais ? Labda utafute mfano wa mtu mwingine

Mwaka 2017 ameenda nchi hizi: Saudi Arabia, Israel, Palestine, Italy, Vatican City, Belgium, Italy, Poland, Germany, France, Japan, South Korea, China, Vietnam, Phillippines.

Mwaka 2018 ameenda nchi hizi : Switerland, Canada, Belgium, United Kingdom, Finland, Argentina, Iraq, Germany

Mwaka 2019 ameenda nchi hizi: Vietnam, Japan, United Kingdom, Ireland, France, South Korea, North Korea, France, Afghanistan.

Na hizo zote ni strategic kuna vitu anavyotafuta kuweka influence katika sehemu muhimu duniani, bado marais wengine wanaokuja kutembeza bakuli kwake.

Kwenye suala la mahusiano ya kimataifa aseme tu ni changamoto ataishughulikia basi, tusifiche madhaifu mbona kuna mengine mazuri ameyafanya humu humu ?

Ni kama kuna mshikaji mmoja tulikuwa tunasoma naye chuo alikuwa anajidai yeye sio mtu wa mademu anataka tu asome afaulu, maisha yalikuwa darasani, hostel, cafeteria, kumbe alikuwa domo zege na anahangika na msongo wa mawazo mwisho wa siku hata kitabu kilishindwa kumwendea vizuri.
 
Wape salaam.
 
..aache kutudanganya.

..mbona alikimbia tafrija na mabalozi wa nchi za nje inayofanyika kila mwaka?

..huyu hajiamini kukutana na viongozi wa nje.
 
Nani mzalendo nchi hii kama Mwl. Julius Kambarage Nyerere? Nyerere hakuwahi kukosa kuhudhuria kikao chochote cha UN au OAU! Na, yeye in person, alituwakilisha vyema mno hadi tukaona fahari kuitwa watanzania.

Nyerere amefanya dhifa nyingi sana za kitaifa pale Ikulu kuwakaribisha viongozi mbalimbali wa mataifa kuitembelea nchi yetu. Nyerere amehudhuria mikutano mingi sana ya kikanda - SADC, NAM, n.k. yeye binafsi bila kutuma mwakilishi na alijibu maswali yasiyojibika kwa weledi mkubwa!

Baada ya kustaafu, Nyerere amehudhuria na ku-chair mikutano isiyo na idadi kimataifa; amehutubia mabunge (mf. lile la South Africa), n.k. Kujenga nchi sio kutohudhuria shughuli za kimataifa; hata hao wanaotumwa kuwakilisha (VP, PM, n.k.) nao wanajenga nchi vile vile.
 
Pamoja na kwamba diplomasia sio kwenda ulaya lakini kuhudhuria mikutano ni muhimu lakini kuvuruga mahusiano huku umejifungia sio diplomasia ,unavurugana na kila jirani ndio diplomasia gani?
Kwani kutoenda Ulaya kumepunguza gharama za kusafiri au utawala ambazo zilikuwa zinalalamikiwa?
Mtu hajui lugha ya kimataifa anasingizia kujenga nchi πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Kujenga nchi ni pamoja na kuhudhuria mikutano ya Kimataifa yenye faida kwa nchi yako kwa hadhi ya ukuu wa nchi
Hiyo mikutano makaburasha aweza kukuletea balozi ni kumwambia ongea hiki na hiki basi vinginevyo ni safari tu za kuzipelekea hoteli zao pesa tu za kula na kulala
 
Hayo yalikuwa ya Nyerere usiwe mtumwa wa historia kila zama zina kitabu chake na kila kitabu cha somo huwa kina new edition .Huwezi komalia toleo la kitabu ulilosoma wakati wa Nyerere tu.Kuna new edition
 
Magufuli anawapa shida sana chadema. Waonee huruma baba watakosa hata diwani.
 
Hakika jiwe Linaendelea kusagika kweli kweli.
Kwahiyo yeye anajua kusafiri nje ya nchi ndio kujenga Diplomasia?????

Kama hafuati sheria za kimataifa, mahusiano mazuri na majirani , haki za Binadamu , uhuru wa vyombo vya habari ndio ana zidi kuizika diplomasia.

Huyu kweli alisukumizwa kuwa rais kama anavyodai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…