Kishindo cha Rais Magufuli katika Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa

Kwa miaka yote mitatu uliyotaja hakuna nchi hata moja ya Africa Raisi Trump aliyotembelea sasa sisi tukazurure Marekani kutafuta nini ? Balozi yuko kule anatosha
 
Hayo yalikuwa ya Nyerere usiwe mtumwa wa historia kila zama zina kitabu chake na kila kitabu cha somo huwa kina new edition .Huwezi komalia toleo la kitabu ulilosoma wakati wa Nyerere tu.Kuna new edition
... diplomasia ni kati ya mambo yamekuwepo tangu kale, yapo, na yataendelea kuwepo hadi ukamilifu wa dahari! Msemaji rasmi wa nchi kimataifa ni rais wa nchi. Hakuna siku mahusiano hususan kujenga mahusiano mema na mataifa mengine yatakoma eti ni "historia".
 
Kwa miaka yote mitatu uliyotaja hakuna nchi hata moja ya Africa Raisi Trump aliyotembelea sasa sisi tukazurure Marekani kutafuta nini ? Balozi yuko kule anatosha
Marekani si kwa Trump tu.

Makao makuu ya Umoja wa Mataifa yako New York City.

Hapo viongozi wote wa dunia nzima huwa wanakutana kila mwaka mwezi wa September.

Katika mkutano unaitwa United Nations General Assembly.

Miaka mitano yote ya utawala wa Magufuli hajaenda.

Unaelewa hilo?
 
Nchi haijengwi kwa kuchoma nyavu halali
 
Hii ya ndani kaishindwa vipi kuhusu ya nje.😁😁
 
Kwani wapi nimesema aende kila tukio?

Unajua kusoma kwa ufahamu?
 
Mkutano ni mkutano tu uwe wa umoja wa mataifa au kikao cha harusi
kwa teknolojia iliyopo na corona zilizoko huko Marekani mtu waweza fuatilia mkutano online,ukatoa comment na decisions online kama kuna mtu anatakiwa Live mkutanoni unamwambia tu balozi nenda watsap me ukiona chochote kinachotaka decision nikurushie jibu kwenye namba yako ya watsapp uwajibu humo mkutanoni .Mimi niendelee na mambo mengine
 
Mada ya kijinga kabisa. Yani Magufuli kafungamana na madikteta ndiyo unasema kishindo?

Kiongozi gani wa nchi hajawahi kushiriki baraza lolote lile la umoja wa mataifa!
tulikuwa na wa namna hiyo lkini tulishuhudia mpaka wanyama wetu nao wakisafirishwa kwenda huko, na hata hivyo ni ninyi mlizomea Sana mtindo wa Raisi kusfiri nje, inakuweje mkuu kila mtindo wa viongozi wetu kwenu ni matatizo?
 
tulikuwa na wa namna hiyo lkini tulishuhudia mpaka wanyama wetu nao wakisafirishwa kwenda huko, na hata hivyo ni ninyi mlizomea Sana mtindo wa Raisi kusfiri nje, inakuweje mkuu kila mtindo wa viongozi wetu kwenu ni matatizo?
Wanakuwa na mitindo too much! Yani nyie viongozi wenu sijui mnawatoa wapi!
 
Ni kweli Lissu kachokonoa kwa kueneza yaliyo uzushi mtupu. Uzushi ukiachwa usambae unakuwa ukweli

Isitoshe, mwenye "pressure" ni Lissu. Mwanzo wa Kampeni zake alikuwa na ugomvi na Tume, kisha vyombo vya habari, na kwa mbali Rais Magufuli.

Baada ya kuona Serikali haistuki na mikwara yake hiyo jukwaani, na wagombea wa CCM wabajikita na hoja za maendeleo zibazojibu jibu baadhi ya uzushi wake, akamua kuporomosha tuhuma za uzushi dhidi ya Tume na Magufuli.

Nia yake jukwaani ni kuilazimisha Serikali imchukulie hatua akinukishe kwani hakuna shaka, kwa pesa kidogo tu, wapo vijana ambao wako tayari kufanya vurugu wakiagizwa kufanya hivyo.

Ushauri kwa Serikali ni kumwacha aendelee na mikwara yske hiyo, jamii ya wastaarabu watamwadhibu kwa kura.
 
Miaka mitano ya Magufuri ndio kumekua na makampuni (agents) wengi wakuagiza mizigo na magari nje ya nchi, na watu wanaagiza kila iitwapo leo. Hii nitafsiri tosha kua tunakua kiuchumi na hata kwa pato la mtu mmoja mmoja.
 
Magufuli hajatoa hotuba UN General Assembly hata online.

Point yako ingekuwa na nguvu kama angekuwa katoa hotuba online ila hajaenda.
 
Ukweli mchungu
 
Kishindo gani ameonyesha huyo mshamba na limbukeni mkubwa, labda kuteka watu na kuua wasio na hatia. Mshamba na muuaji mkubwa, taahira huyo.
Punguza makali, haina haja ya kukejeli, kutuhumu bila udhibitisho, unaweza kuonyesha tu haukibaliani nae kwa lugha ya kiungwana zaidi!
 
Danganyeni wasiojielewa.Mnatumia nguvu nyingi kutakatisha kaniki.
 
Chadema wakishika dola ikulu itahamia Ubelgiji ili kudhihirisha kuimarika kwa uhusiano wa kimataifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…