Kisigino kinaniuma sana!

Kisigino kinaniuma sana!

Alex Mponela

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
254
Reaction score
109
Wadau nawaombeni msaada, kisigino changu cha mguu wa kushoto kinaniuma sana utafikiri labda kuna msumari umeingia, nimewaona wataalamu wengine wakasema huenda ni uzito nipunguze uzito.

Nimefanya zoezi na kupunguza uzito karibia kilo tano lakini bado tu. Kisigino kinaniuma hasa wakati ninaamka asubuhi, ila nikiwa busy kinaacha, na nikiwa iddle tu kwa muda kama nikiwatch movies nusu saa tu tayari kinaanza tena!

Wakuu naomba msaada wenu!
 
Hata mimi nina ilo tatizo aseee, embu ngoja watuambie
 
Wadau nawaombeni msaada, kisigino changu cha mguu wa kushoto kinaniuma sana utafikiri labda kuna msumari umeingia, nimewaona wataalamu wengine wakasema huenda ni uzito nipunguze uzito. Nimefanya zoezi na kupunguza uzito karibia kilo tano lakini bado tu. Kisigino kinaniuma hasa wakati ninaamka asubuhi, ila nikiwa busy kinaacha, na nikiwa iddle tu kwa muda kama nikiwatch movies nusu saa tu tayari kinaanza tena! Wakuu naomba msaada wenu!!

kuna mtu yeye alikuwa anaumwa visigino vyote akiwa iddle, akiwa bize haviumi. sasa hivi amepona, lakini tiba aliyotumia sikuona kama ina make sense anasema aligundulika na typhoid na ugonjwa mwingine kwenye damu, alivyoanza kutumia madawa aliyopewa akapona na hadi sasa yuko fit.
 
Hivi ni kisigino tu au hata dole gumba la mguu saa nyingine linauma? Najaribu kueliminate gaut.
 
Mimi naumwa kisigino tu! Nawashukuru wadau hata hivo kwa mawazo yenu nimeshabadilisha hata viatu navaa very flat shoes toka sasa ila baada ya muda ntakuja kwenu nikiwa na majibu ya suggestions mlizonipa nikazifanyia kazi!
Thanks!
 
Hii hali ya kuumwa kisigino ilishawahi kunitokea miaka kadhaa iliyopita, lkn sikujua kilichoniponesha wala kilichokuwa kimesababisha maumivu hayo. Sikumbuki kutumia dawa.
 
Jaribu kuwasiliana na Dr. wako akufanyie uchunguzi pengine unaweza kuwa na kijiba kilichoota kwenye kifupa cha kisigino kwa kitaalam wanakiita calcaneal spur, kama ndio hicho watakudunga sindano ya steroid kwenye maumivu.
 
Wadau nawaombeni msaada, kisigino changu cha mguu wa kushoto kinaniuma sana utafikiri labda kuna msumari umeingia, nimewaona wataalamu wengine wakasema huenda ni uzito nipunguze uzito. Nimefanya zoezi na kupunguza uzito karibia kilo tano lakini bado tu. Kisigino kinaniuma hasa wakati ninaamka asubuhi, ila nikiwa busy kinaacha, na nikiwa iddle tu kwa muda kama nikiwatch movies nusu saa tu tayari kinaanza tena! Wakuu naomba msaada wenu!!
Dawa ya kisigino kinachouma ni kupakaa mchanganyiko wa mafuta ya taa na mafuta ya alizeti iliyochanganywa katika ratio iliyosawa. unapaka tu asubuhi na jioni kwa siku chache kama siku nne au zaidi kidogo na utapona kabisa, ukipenda unaweza kuwasiliana na mimi kwa maelezo zaidi au kama utapenda kutumiwa mchanganyiko ulio tayarishwa tayari wasiliana na mimi kwa simu no:- 0754806828.
 
Salamu wadau,
Najua ni muda umepita ila nina maarifa kidogo kuhusu haya maumivu ya kisigino kwani nami niliwahi kupata tatizo hili na nikafanikiwa kupata tiba. Nilikuwa na maumivu yanayofanana na mtoa taarifa ya awali kuwa kisigino kinauma sana muda tu ninapoamka toka kitandani (asubuhi) na maada ya shughuli chache (being busy) hayo maumivu yanatoweka ila pindi ukitulia kwa muda unayahisi yanarejea tena.

Nilionana na daktari wa mifupa akashauri kwanza nikapige picha (x-ray) ambayo ilionyesha kuwa sikuwa na athari zozote katika mifupa ya kisigino. Akanambia kama ni hivyo basi nitakuwa na tatizo la msuli kamba. Alimeleza kuwa huu ni msuli unaopita katika kisigino ukitokea katika kidole kikuu cha mguu na wakati fulani inatokea huu msuli unabanwa na nyama za kisigino hasa kutokana na kuongezeka kwa uzito au kuumia mchezoni. Na akanipatia tiba ya sindano aliyoichoma palepale katika eneo la jeraha na nashukura sasa ni zaidi ya miezi sita lile tatizo halijarejea.
 
Hii inaweza ikawa ni side effects za kutumia dawa. Kama lakini kuna dawa unazotumia.

Kama sio dawa basi jaribu kufanya mazoezi ya kutembea au jogging kwa mda wa mwezi mmoja ukiwa na viatu sahihi vya jogging.

Kama hutapata nafuu. Basi kamcheck daktari bingwa wa mifupa.
 
Asante ni Habayu na Dr. Love kwa mawazo yenu. Mimi nilishapona. Miaka mitatu sasa imepita toka nilete uzi huu.
 
Lazma utakua na matatizo cheki mchoro
upload_2016-2-18_12-36-54.png
 
Asante ni Habayu na Dr. Love kwa mawazo yenu. Mimi nilishapona. Miaka mitatu sasa imepita toka nilete uzi huu.

Mkuu ulipona kwa kutumia dawa gani, binti yangu ana hili tatizo plz help only 13 yrs, please help
 
Salamu wadau,
Najua ni muda umepita ila nina maarifa kidogo kuhusu haya maumivu ya kisigino kwani nami niliwahi kupata tatizo hili na nikafanikiwa kupata tiba. Nilikuwa na maumivu yanayofanana na mtoa taarifa ya awali kuwa kisigino kinauma sana muda tu ninapoamka toka kitandani (asubuhi) na maada ya shughuli chache (being busy) hayo maumivu yanatoweka ila pindi ukitulia kwa muda unayahisi yanarejea tena.

Nilionana na daktari wa mifupa akashauri kwanza nikapige picha (x-ray) ambayo ilionyesha kuwa sikuwa na athari zozote katika mifupa ya kisigino. Akanambia kama ni hivyo basi nitakuwa na tatizo la msuli kamba. Alimeleza kuwa huu ni msuli unaopita katika kisigino ukitokea katika kidole kikuu cha mguu na wakati fulani inatokea huu msuli unabanwa na nyama za kisigino hasa kutokana na kuongezeka kwa uzito au kuumia mchezoni. Na akanipatia tiba ya sindano aliyoichoma palepale katika eneo la jeraha na nashukura sasa ni zaidi ya miezi sita lile tatizo halijarejea.
Ni hospitali gani ama Doctor gani ulimuona mkuu?
 
Back
Top Bottom