Kisima cha ajabu cha Kaole - Bagamoyo

Kisima cha ajabu cha Kaole - Bagamoyo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kaole, mji wa zamani wa Bagamoyo una mambo mengi ya kustaajabisha ikiwemo kisima cha ajabu chenye miaka zaidi ya 800.

Uajabu wa kisima hicho ni kuwa maji yake hayapungui bila kujalisha kipindi cha mwaka au kiasi cha maji kinachochotwa.

Ajabu lingine la kisima hiko ni kuwa kipo karibu na bahari lakini kinatoa maji baridi(yasiyo na chumvi) hali hiyo ndio imeongeza imani ya watu wengi.

Kisima hicho kilichimbwa kwa ajili ya kutawadha waislamu, kipo pembeni mwa Msikiti wa kwanza kujengwa tangu walipoingia Washirazi.

Kaole ilikuwa ni bandari ya kwanza iliyotumika ambayo karne ya 17 ilihamia ilipo hivi sasa kutokana na kina cha maji kupungua hivyo tangu hapo Mji wa Bagamoyo ukaanza kutumika huku Kaole ikiwa imeachwa kama makumbusho.

IMG_20201220_095030_148.jpg
 
Ulifika makaburi ya Masherifu?

Niliwahi kwa miezi sita kusoma shule ya sekondari Kaole enzi hizo ni ya ufundi na kilimo.

Maajabu na visanga vya Kaole vilinipatia hamu ya kupakimbia huko maana majini na watu ilikuwa kama mnapishana sokoni Kariakoo
 
Nimetembelea hapo. Siku moja nilikuwa nafanya utalii wa ndani. Nilitembea toka India street hadi Kaole! Mwanafunzi ilikuwa kiingilio 500.

Nilijifunza mengi sana. Hicho kisima ni maajabu kuwa na maji baridi, sijui sababu ya mikoko mingi eneo hilo?
 
Nimetembelea hili eneo, limejaa historia kubwa sana ya wageni na wazawa kina Mwanamakuka
Nilipata historia ya kusisimua toka kwenye kaburi ya wapendanao na mengine mengi
Waumini wengi wa hufika pale na kufanya ibada
 
hilo kaburi nielezee kidogoo ningependa kujua
 
Kaburi la wapendanao bagamoyo walizikwa wanandoa wawili ambao maiti zao zilikutwa pamoja ufukweni. Inasadikiwa kwamba chombo walichokua wakisafiria kilikumbwa na dhoruba na wanandoa hao waliamua kutumia nguo zao kujifunga pamoja ili wasipoteane kwenye bahari na pale inapotokea wamepona wapone wote.
Mapenzi ya Mungu walishindwa kuhimili dhoruba wakafa wote na baadae maji yakawatupa pwani na waliowakuta kwa kujua mapenzi yao wakaamua kuwazika pamoja
 
Kaole, mji wa zamani wa Bagamoyo una mambo mengi ya kustaajabisha ikiwemo kisima cha ajabu chenye miaka zaidi ya 800.

Uajabu wa kisima hicho ni kuwa maji yake hayapungui bila kujalisha kipindi cha mwaka au kiasi cha maji kinachochotwa.

Ajabu lingine la kisima hiko ni kuwa kipo karibu na bahari lakini kinatoa maji baridi(yasiyo na chumvi) hali hiyo ndio imeongeza imani ya watu wengi.

Kisima hicho kilichimbwa kwa ajili ya kutawadha waislamu, kipo pembeni mwa Msikiti wa kwanza kujengwa tangu walipoingia Washirazi.

Kaole ilikuwa ni bandari ya kwanza iliyotumika ambayo karne ya 17 ilihamia ilipo hivi sasa kutokana na kina cha maji kupungua hivyo tangu hapo Mji wa Bagamoyo ukaanza kutumika huku Kaole ikiwa imeachwa kama makumbusho.

View attachment 1655991
Hakuna mahali labda kwenye website unaweza kupata taarifa hizi?
 
....
Maajabu na visanga vya Kaole vilinipatia hamu ya kupakimbia huko maana majini na watu ilikuwa kama mnapishana sokoni Kariakoo
... ulishaambiwa ndipo palipokuwa makazi ya kwanza ya washirazi; ingekuwa kinyume ndio ingekuwa maajabu!
 
... mitandaoni huko kumetapakaa elimu nyingi kuhusu majini; zitafute ujisomee utapata mwanga kwanini washirazi na wengine wanapenda kuyafuga.
mmh kwasasa niko freebasics lakin pia mtandao ni kama bahari ni ngumu kujua dagaa wanapatikania wapi
Nielezee kwa kifupi tu mkuu natanguliza shukran
 
Kaole, mji wa zamani wa Bagamoyo una mambo mengi ya kustaajabisha ikiwemo kisima cha ajabu chenye miaka zaidi ya 800.

Uajabu wa kisima hicho ni kuwa maji yake hayapungui bila kujalisha kipindi cha mwaka au kiasi cha maji kinachochotwa.

Ajabu lingine la kisima hiko ni kuwa kipo karibu na bahari lakini kinatoa maji baridi(yasiyo na chumvi) hali hiyo ndio imeongeza imani ya watu wengi.

Kisima hicho kilichimbwa kwa ajili ya kutawadha waislamu, kipo pembeni mwa Msikiti wa kwanza kujengwa tangu walipoingia Washirazi.

Kaole ilikuwa ni bandari ya kwanza iliyotumika ambayo karne ya 17 ilihamia ilipo hivi sasa kutokana na kina cha maji kupungua hivyo tangu hapo Mji wa Bagamoyo ukaanza kutumika huku Kaole ikiwa imeachwa kama makumbusho.

View attachment 1655991
Shukrani ziwarudie WAARABU walezi na watunzi wa Amani na maskani....
Historia haidanganyi wala haipotoshi ..
Mola tutunzie mshikamano..
 
Back
Top Bottom