Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Kaole, mji wa zamani wa Bagamoyo una mambo mengi ya kustaajabisha ikiwemo kisima cha ajabu chenye miaka zaidi ya 800.
Uajabu wa kisima hicho ni kuwa maji yake hayapungui bila kujalisha kipindi cha mwaka au kiasi cha maji kinachochotwa.
Ajabu lingine la kisima hiko ni kuwa kipo karibu na bahari lakini kinatoa maji baridi(yasiyo na chumvi) hali hiyo ndio imeongeza imani ya watu wengi.
Kisima hicho kilichimbwa kwa ajili ya kutawadha waislamu, kipo pembeni mwa Msikiti wa kwanza kujengwa tangu walipoingia Washirazi.
Kaole ilikuwa ni bandari ya kwanza iliyotumika ambayo karne ya 17 ilihamia ilipo hivi sasa kutokana na kina cha maji kupungua hivyo tangu hapo Mji wa Bagamoyo ukaanza kutumika huku Kaole ikiwa imeachwa kama makumbusho.