Kisima cha ajabu cha Kaole - Bagamoyo

Kisima cha ajabu cha Kaole - Bagamoyo

Wanasayansi waje watuambie Kwanini kisima hicho hakikauki maji tangu kilipochimbwa karne ya 17 hadi leo karne ya 21,

Pia kwanini kisima kina maji baridi licha ya kua kipo karibu sana na bahari?

Umenikumbusha makaburi ya Masharifu, wanasema vile visahani walivyonakshia kwenye kuta za makaburi vilikua vina madini wajanja wakaving'oa vyoteee.

Kuna kaburi la Sharifat na washirika wake pia, niliingia kupiga picha mule ndani bahati mbaya picha nimezihifadhi sehemu, ningeshare nanyi hapa.
 
Kaburi la Wapendanao,
Couples huenda kubariki mapenzi yao wapendane hadi kufa na kuzikwa pamoja kama hao wapendanao waliozama kwenye jahazi na kukutwa wamejifunga nguo huku wamekumbatiana.
images%20(19).jpg
 
Kaburi la Sharifat na vijakazi wake, huyu alikua ni mtabiri na alikua bikra pamoja na vijakazi wake mabinti wote walikua bikra, alipofariki Safiya na wale vijakazi wake wakajiua na kwa lengo la kuendelea kumuhudumia huko waendako.
images%20(18).jpg
 
Nilikuwa na mpango wa kumwoa mshirazi ila dah kama wanafuga majini duh
 
Wanasayansi waje watuambie Kwanini kisima hicho hakikauki maji tangu kilipochimbwa karne ya 17 hadi leo karne ya 21,

Pia kwanini kisima kina maji baridi licha ya kua kipo karibu sana na bahari?

Umenikumbusha makaburi ya Masharifu, wanasema vile visahani walivyonakshia kwenye kuta za makaburi vilikua vina madini wajanja wakaving'oa vyoteee.

Kuna kaburi la Sharifat na washirika wake pia, niliingia kupiga picha mule ndani bahati mbaya picha nimezihifadhi sehemu, ningeshare nanyi hapa.
Chini ya ardhi kuna siri nyingi. Kuna mito inayomwaga maji baharini ipitayo chini kwa chini na vyanzo vyake huwa ni vya mbali sana. Eneo laMpera hapa Kigamboni kuna maji mengi sana na ni baridi kabisa hayana chumvi. Huo ndio uumbaji wa Mwenyezi Mungu ambao wewe na mimi tutapita lakini tutakuwa hatumaliza elimu yake
 
Duniani kuna mambo ya maajabu mnegi. Kuna visima vyenye maji ya moto kama vile yamechemshwa huko Mkoa wa Katavi, Solai huko Nakuru nchini Kenya. Tatizo ni kuwa hatuna tabia ya kuandika historia vizuri. Kwa mfano, pale Bagamoyo kuna historia nzuri sana kama ingeandikwa vizuri katika vitabu ungekuwa urithi mzuri wa watoto wetu.
 
Kaole, mji wa zamani wa Bagamoyo una mambo mengi ya kustaajabisha ikiwemo kisima cha ajabu chenye miaka zaidi ya 800.

Uajabu wa kisima hicho ni kuwa maji yake hayapungui bila kujalisha kipindi cha mwaka au kiasi cha maji kinachochotwa.

Ajabu lingine la kisima hiko ni kuwa kipo karibu na bahari lakini kinatoa maji baridi(yasiyo na chumvi) hali hiyo ndio imeongeza imani ya watu wengi.

Kisima hicho kilichimbwa kwa ajili ya kutawadha waislamu, kipo pembeni mwa Msikiti wa kwanza kujengwa tangu walipoingia Washirazi.

Kaole ilikuwa ni bandari ya kwanza iliyotumika ambayo karne ya 17 ilihamia ilipo hivi sasa kutokana na kina cha maji kupungua hivyo tangu hapo Mji wa Bagamoyo ukaanza kutumika huku Kaole ikiwa imeachwa kama makumbusho.

View attachment 1655991
Uliuona mti wa kuongeza maisha?
 
Back
Top Bottom