Kisimbuzi gani cha ndani kitarusha matangazo ya Kombe la Dunia la mwaka huu?

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Nauliza, ni kisimbuzi gani cha ndani ambacho kitarusha kombe la Dunia la mwaka huu?

Miaka ya nyuma tulikuwa tunaona shamrashamra za matangazo kwenye visimbuzi vya ndani mfano Startimes kwamba watarusha, lakini mwaka huu kimya na zimebaki siku kadhaa!

CCM tulishawashauri, Watanzania tunapenda mpira ambapo husahau mambo mengine, hivyo CCM wajitahidi kadri wawezavyo wawasaidie visimbuzi vya ndani (local) au Channel Ten na Channel Ten Plus wanunue haki za kurusha matangazo ya Kombe la Dunia ili wananchi wasipate muda wa kufuatilia mambo ya nchi!

Sasa kama CCM wanaanza kupuuza hadi michezo hasa soka, naona wanajitengenezea bomu, maana kwa sasa kitu pekee kinachowazubaisha Watanzania ni mpira!

CCM toeni hela visimbuzi au chaneli yenu irushe kombe la Dunia hata bure! Msijisahau sana!
 
Ni ujinga kudhani kuwa CCM ndio Kama mzazi wako.

Kombe la dunia mechi zote zitaonesha live kwenye DStv Lipia dish Kwa around 70k na kifurushi Kwa around 54k bei za kizalendo kabisa hizi.

Au la hasha dish la Azam wataonesha baadhi ya matches
 
Channel ya taifa imepewa haki na FIFA ya kuonesha kombe hili kwahyo mechi zitaonekana TBC 2, hii channel inapatikana Kwenye king'amuzi cha startimes.

Ila kuna mdau humu alivitaja ving'amuzi ambavyo vimeshasema vitaonesha hili kombe ni Startimes, Dstv na Canal
 
Hapo ndio utaelewa ukubwa wa DSTV huko bongo acha kuishi kimaskini tafuta pesa azam tv wanawapofusha
 
Tbc ccm itaonyesha mechi 28 tu. Zingine tuzifuate DSTV
 
Habari za wakati huu wakuu, ningenda kujuzwa ikiwa kuna media yoyote tofauti na DSTV ambayo inaweza kurusha matangazo haya
 
Hii ni bei ya king'amuzu cha DSTV ama ndio bei ya kifurushi??
DSTV wanapiga promo kuwa, kwa shilingi elfu 79 tu utapewa full set (Dish na receiver) plus offer ya bure ya kifurushi cha mwezi mmoja cha compact (kwa kawaida hulipiwa shilingi elfu 55), na mechi zote 64 za world cup utaziona.
 
Kipindi hiki dstv watauza vingamuzi sana, kama wa natoa bando la mwezi mzima bure basi si hasara nikikinunua kwa 79,000 nika pewa na airtime ya mwezi mzima bure, world up ikiisha nakiuza kwa tsh 20,000-40,000 maana Azam huwa nalip a 35,000 kila mwezi na siangalii hata, ikifika January decoder za dstv lazima zishuke bei, maana nyingi zitakuwa zinauzwa mitaani.
 
DSTV wanapiga promo kuwa, kwa shilingi elfu 79 tu utapewa full set (Dish na receiver) plus offer ya bure ya kifurushi cha mwezi mmoja cha compact (kwa kawaida hulipiwa shilingi elfu 55), na mechi zote 64 za world cup utaziona.
Saf sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…