Kisiwa cha Kome Mkoani Mwanza chateketea kwa moto usiku wa leo

Kisiwa cha Kome Mkoani Mwanza chateketea kwa moto usiku wa leo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijafahamika umeibuka usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Mei 23, 2020, katika Kisiwa cha Kome eneo la Mchangani, halmashauri ya Buchosa, Sengerema, mkoani Mwanza na kuteketeza vibanda vingi vya wafanyabiashara pamoja na mali zilizokuwemo kwenye vibanda hivyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Muliro Jumanne Muliro, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo, madhara na thamani ya vitu vilivyoteketea.

Kwa mujibu wa mashuhuda,wamesema moto huo uliibuka majira ya saa 6 usiku na kudumu mpaka saa 10 alfajiri.

“Maduka, nyumba na vitu vingine vimeungua, watu wamepata hasara kubwa na wote bado wana taharuki kubwa kutokana na ajali hii. Imekuwa ni jambo la mara kwa mara kwa kisiwa hicho kukumbwa na matatizo ya moto.

“Vibanda vingi ni vya muda, vimejengwa kwa mabanzi ya mbao na vipo karibu-karibu, kwa hiyo kikiwaka moto kimoja ni rahisi sana kuteketeza na nyingine kwa sababu mbao zenyewe zina mafuta,” amesema shuhuda mmoja

Baadhi ya mali nyingine zilitoteketea ni magari matano na samaki za wafanyabiashara.
 
May 23, 2020
Buchosa, Mwanza
Tanzania

Kisiwa cha Kome eneo la Mchangani, halmashauri ya Buchosa, Sengerema, mkoani Mwanza



Source : Global TV online
 
daah poleni sana wiki iliyopita niliona maji yameongezeka hapo leo Moto hatari sana..
 
April 4, 2020
Naona huko Buchosa Mwanza kuna majanga mengi ya asili na ajali. Mfano ziwa Victoria kufurika na nyumba zaidi ya 170 ambazo zilijengwa mita 60 toka ufuo / pwani ya ziwa Victoria zimefurika maji ya ziwa hilo linalozidi kujitanua



Mkazi mmoja anasema ni takribani miezi mitano sasa maeneo yao ya makazi yamejaa maji ya Ziwa Victoria.

Source : BM TV TANZANIA
 
Kisiwa kina wachawi hicho hatari moto utakuwa umeunguza vibuyu na tunguli zao
 
Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijafahamika umeibuka usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Mei 23, 2020, katika Kisiwa cha Kome eneo la Mchangani, halmashauri ya Buchosa, Sengerema, mkoani Mwanza na kuteketeza vibanda vingi vya wafanyabiashara pamoja na mali zilizokuwemo kwenye vibanda hivyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Muliro Jumanne Muliro, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo, madhara na thamani ya vitu vilivyoteketea.

Kwa mujibu wa mashuhuda,wamesema moto huo uliibuka majira ya saa 6 usiku na kudumu mpaka saa 10 alfajiri.

“Maduka, nyumba na vitu vingine vimeungua, watu wamepata hasara kubwa na wote bado wana taharuki kubwa kutokana na ajali hii. Imekuwa ni jambo la mara kwa mara kwa kisiwa hicho kukumbwa na matatizo ya moto.

“Vibanda vingi ni vya muda, vimejengwa kwa mabanzi ya mbao na vipo karibu-karibu, kwa hiyo kikiwaka moto kimoja ni rahisi sana kuteketeza na nyingine kwa sababu mbao zenyewe zina mafuta,” amesema shuhuda mmoja

Baadhi ya mali nyingine zilitoteketea ni magari matano na samaki za wafanyabiashara.
Kicha cha habari kirekebishwe. Kisomeke kisiwa cha Kome eneo la Mchangani lateketea kwa moto na siyo kisiwa cha Kome.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia kumetokea mlipuko wa Moto kisiwa Cha Kome . Wenye habari au taarifa kamili watupe updates. Chanzo magazetini TBC redio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishtuka kwamba KISIWA KIMETEKETEA KWA MOTO!!

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Poleni sana ndugu mlioko huko, yani kuna siku zinakuwa mbaya balaa huenda mtu anaishi hapo wiki kadhaa zilizopita nyumba yake ilimezwa na maji akaamua kukopa pesa afanye biasha kubwa kidogo kusudi ajipange ajenge eneo lingine baada siku tatu moto unaunguza kila kitu hapo usipokuwa makini unaweza kujidhuru..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom