Kisiwa cha Mafia tushaamua, hatumtaki Bulji

Kisiwa cha Mafia tushaamua, hatumtaki Bulji

wakati wa kujadili hoja ya gesi nakumbuka Shibuda pamoja na mapungufu yake alitetea wakulima wa pamba na kusema hiyo ndiyo gesi yao so wakumbukwe kwenye kilimo kwanza kwa pembejeo Buji kasema nn kwenye minazi inayokufa mafia? Tulimpeleka bungeni akatetee familia yake na chama? Naomba mwana jf mwenye cv yake aiweke jamvini tuichambue.
 
wewe una elekea sio mmafia... unawatia chumvi watu wapate kughadhibika lakini hauna imani na watu wa mafia.. kila mtu hapa anataka anngalie masilahi yake tu.. bulji anaangalia masilahi ya watu wake.. inafikia kipindi nyumbani kwake kuna kuwa hakuna chakula na familia yake ina suffer.. watu kama nyinyi mnabidi mchukuliwe hatua maana mna haribu amani tuliyokuwa nayo wamafia.. nakushauri kaangalie kazi alizozifanya buji huko mafia ndio muongee nonsense zenu.. 🙂
We jamaa akili yako ndogo kama sisimizi.Hivi inawezekana familia ya mbunge ikalala na njaa?Ndo anavyowanganya huyo mbunge wenu na nyie mnadanganyika kijinga hivyo?!!Duh!Ama kweli......Kuna mchangiajia mmoja kawaita watu wa Mafia WAPUMBAVU,kwa UTUMBO huu uliouandika nadhani yule mchangiaji hakukosea kabisa.!
 
We jamaa akili yako ndogo kama sisimizi.Hivi inawezekana familia ya mbunge ikalala na njaa?Ndo anavyowanganya huyo mbunge wenu na nyie mnadanganyika kijinga hivyo?!!Duh!Ama kweli......Kuna mchangiajia mmoja kawaita watu wa Mafia WAPUMBAVU,kwa UTUMBO huu uliouandika nadhani yule mchangiaji hakukosea kabisa.!

Mkuu tuombe radhi watu wa Mafia!!! Umefanya very bad generalization...
 
na bado, mpaka mtokoma kuringa mwaka huu. wenzenu wa karatu roho zetu kwatuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu! pateni hayo mateso labda akili zenu zitawarudia huko mbeleni!
 
Wanamafia wafate kwao mfa yaonekana wewe CCM kwenda huko kaombe kula kwa bwana wenu DAU.....!! Tumeichoka CCM
 
mafia ina watu zaidi ya laki 1 haiwezekani tuongopewe kuwa mbunge mahiri aliopo hafai

mpaka uwanja wa ndege kajenga na bandari karibuni inakamilika
 
Wana Mafia kweli mmeamka

kwanza mna access to internet japo inaonekana hamko wengi

lakini wachache mliopo naona mnaitumia JF effectively

kwa hili nawapa hongera sana
 
Huyu mbunge wetu wa sasa nadhani mwenyewe keshajua. His time is up na nadhani its about time akatangaza kutogombea tena 2015.

Tushachoka na CCM wakitaka kulazimisha then bora tuwape wapinzani jimbo lakini as it is. We've had enough with Mr Shah. This does not mean kuwa tunataka Omari Kimbau awe mbunge wetu

Kisiwa kinaendeshwa na NGO's tuuu , watu wamekatazwa kuvua, hakuna umeme, barabara mbovu, vituo vya afya navyo hatuna, kila kitu kigumu hapa kisiwani

lakini tushaamua. Hatumtaki huyu Mbunge wetu. Tushamchoka!!
nawapa pole sana kwa kuchgua wabunge wa aina hii, ila nawa tahadhali pale mtakapofanya mabadiliko ya mbunge msithubutu kumchagua omari kimbau yaani huyu ni zaidi ya kimeo. alikua diwani kata ya kijitonyama, hajawahi kuoneka kwenye kata na kuhama kabisa kwy kata yake na kuhamia masaki alikojenga nyumba baada ya kupata udiwani. sasa mkimpa jimbo ndio hatahamia ngurudoto.
 
WASWAHILI husema tembea uone. Nilidhihirisha usemi huu pale nilipokuwa katika kisiwa cha Mafia kilichopo ndani ya bahari ya Hindi hivi karibuni nilipokuwa katika safari zangu za kikazi.Jambo la kushangaza nilipofika eneo hilo nilichukua chumba jirani kabisa na manispaa ya kisiwa hicho,lakini nilipokuwa nakula usiku nilikuta watoto wa kike wa shule wakiwa wanatokea ndani wakiwa wameongozana na watu wazima ambao wanaweza kuwazaa.

Nilipatwa na mshituko pale nilipoona watu wakiwa wanaona ni mambo ya kawaida kwani hakuna hata aliyeshtuka, lakini nilipojaribu kuulizia nikaambiwa, hiyo ndiyo Mafia kaka.Naweza kusema kwamba jamii yoyote ile inayotawaliwa na imani za kishirikina ni vigumu sana kwake kuendelea na hii inatokana na kwamba kila mtu wa jamii hiyo huogopa kujiendeleza akihofia kupoteza maisha yake au ya jamaa zake.

Hali hii pia inasababisha hata maendeleo yanakosekana kama suala la elimu kwani kila mtu anajitahidi kadri awezavyo kutafuta njia ama ya kujilinda mwenyewe, familia, ukoo au jamaa kwa ujumla ili asilogwe na wenzake. Kwa jinsi hiyo nathubutu kusema kuwa kama umefika mahali ukakuta imani za kishirikina zimetawala, basi ujue hakika asilimia kubwa ya jamii hiyo haijaelimika.

Mwalimu mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini alitamka wazi kuwa kuna mwenzake amehama Mafia kutokana na imani za kishirikina kwani siku moja alikuwa amelala akasikia mtu anabisha hodi alipokwenda kumfungulia anakuta ni mbwa amelala chini .

“Yule mwalimu inaonekana hakuaga kwao kwani alitokea bara kama mimi, lakini wengi huku tumeaga ndio maana unatuona huku, tunadunda suala la kuona vituko huku ni la kawaida kaka,”anasema
Anaongeza kuwa kutokana na hali hiyo inaaminika kuwa walimu wengi wanaohamishiwa katika kisiwa hicho wamekuwa wakikimbia wenyewe kutokana na vitendo hivyo vya ushirikina.

“Mimi mwenyewe kuna kipindi nilikuwa nikilala najikuta naamkia uwanja wa mpira, nikaamua kwenda kuaga kwanza nyumbani kwa sababu kila nikiwasimulia wenzangu walikuwa wakinicheka.

‘’Wizara husika (Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Tawala za Mikoa wa Serikali za Mitaa ) zinatakiwa kuweka mikakati madhubuti kuwanusuru watoto wanaoonekana kuikosa elimu yao, huku walimu nao wakikataa kuhamishiwa huku kwa kuhofia usalama wa maisha yao,”anasema

Pia, inaaminika kuwa karibu maeneo mengi yanayoambaa kando kando ya mikusanyiko ya maji mengi kama vile maziwa, mito mikubwa na bahari, yana historia ya kuamini na kutegemea ushirikina

Katika hatua nyingine ya kusikitisha wazazi wamedaiwa kuwatetea watu wanaowapa ujauzito watoto wao kwa kumalizana kifamilia , huku wakitoa vitisho kwa walimu wanaopeleka kesi hizo mahakamani wilayani Mafia.
Akizungumza wilayani humo katika kongamano lililoandaliwa na shirika la Kimarekani la Action- Aid, ofisa elimu wa wilaya hiyo , Mohamedi Kahundi alisema kuwa hali hiyo imeshazoeleka wilayani hapo kutokana na kujaa kwa imani za kishirikina.

Anasema kuwa walimu wanashindwa kuwasaidia watoto kuendelea kupata elimu kutokana na kupata mimba kila mwaka na wanaowapa mimba hizo wakiwa wanafahamika na kuwaachwa wakirandaranda tu mitaani.
Kahundi anaeleza kuwa hadi sasa hivi watoto 35 wanaosoma shule za msingi na sekondari wamepata ujauzito kuanzia mwaka 2008, lakini hakuna jitihada zilizofanikiwa kuwakamata wahusika kutokana na walimu kutishiwa na wazazi wa watoto hao.

“Kinaschoharibu hapa ni imani za kishirikina kwani watu wanawatishia walimu kuwaroga kwa sababu wamewapeleka kesi polisi za watoto kupatiwa mimba ,sasa badala ya mzazi kutoa ushirikiano wanatoa vitisho tena,”anasema Kahundi

Akizungumza wilayani hapo katika kongamano lililoandaliwa na Aid, afisa elimu wa wilaya hiyo Mohamedi Kahundi anasema kuwa hali hiyo imeshazoeleka wilayani hapo kutokana na kujaa kwa imani za kishirikina.
Anasema walimu wanashindwa kuwasaidia watoto kuendelea kupata elimu kutokana na kupata mimba kila mwaka na wanaowapa mimba hizo wakiwa wanafahamika na kuwaachwa wakirandaranda tu mitaani.

Anasema kwa sasa hivi jumla ya watoto 35 wanaosoma shule za msingi na sekondari wamepata ujauzito kuanzia mwaka 2008 mpaka mwaka huu lakini hakuna jitihada zilizofanikiwa kuwakamata wahusika kutokana na walimu kutishiwa na wazazi wa watoto hao.

“Kinachoharibu hapa ni imani za kishirikina kwani watu wanawatishia walimu kuwaloga kwa sababu wamewapeleka kesi polisi za watoto kupatiwa mimba ,sasa badala ya mzazi kutoa ushirikiano wanatoa vitisho tena”anasema Kahundi

Mwalimu mkuu wa shule ya Kilindoni, Mwajuma Likindi anasema kuwa wazazi wanachangia sana watoto wao kupata mimba huku wakiwa tupia lawama walimu hao,akitoa mfano anaeleza kuwa kuna mzazi alimfuata shuleni hapo akimuuliza kuwa amemtuma wapi mototo wake mbona amekutana naye akiwa anaingia nyumba ya wageni?
Mwalimu huyo alisema alipatwa na mshangao sana kwani mzazi Yule badala ya kumwuliza binti yake anaenda kufanya nini katika nyumba ya wageni anakuja na kumwuliza mwalimu kuwa mbona mwanaye anaingia nyumba za wageni.

“Yaani mimi nimtume mwanafunzi nyumba ya wageni afuate nini sasa wakati mimi nakemea vitendo vya ngono,”anasema mwalimu Yule.Naye mwalimu mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake gazetini anasema kuwa kuna mwanafunzi wa darasa la nne alipewa mimba na rafiki wa baba yake, lakini mzazi wa yule mtoto aliposikia rafiki yake anatafutwa alimwambia atoroke.

‘’Nilipoendelea kufuatilia nikatishiwa maisha na wahusika nikaachana nao, lakini mpaka leo ninaumia sana roho hali hii itaendelea mpaka lini, “analalamika mwalimu huyo. Kwa upande wake mratibu wa Action Aid nchini, Jovina Nawenzake anasema kuwa wanaotakiwa kupewa lawama ni wazazi kwani wanakosa muda wa kukaa na watoto wao.

Anasema kwa wilaya ya Mafia kuwaona wanafunzi wakiingia katika nyumba za wageni ni jambo la kawaida ,huku wazazi wakiwa wanafahamu hayo, lakini wanakosa muda wa kuwaadabisha.

Mwanasheria wa wilaya hiyo, Simon Rendika anasema kuwa mpaka leo hakuna hata kesi ya mwanafunzi mmoja aliyepewa mimba iliyomalizikia mahakamani kwani zote wazazi wanamalizana kifamilia.Anasema hali hiyo imeshazoeleka Mafia kwa sababu za imani za kishirikina na ndio hasa watoto wanaendelea kufanya uhuni na kuzaa hovyo huku wakisema ni ugumu wa maisha.

Hiyi ndio hali ya elimu Mafia
 
Duuuh aisee! you made my day....yaani hujakosea kabisa,maana 95% ya wakazi wa Mafia ni waislaam....so CDM wakitia timu tu hapo ili
kuwakomboeni, ccm watakuja na single ya udini na nyinyi kwa akilizenu zilivyombovu mtakubali na mtawapigia kura magamba.
Kaeni chini,mtafakari na kisha fanyeni maamuzi ya kuwakaribisha wapinzani "hasa CDM"

huko CUF ndo itaeleweka sio cdm
 
Acheni kulalamika nyie, mlifurahi kupewa kofia,t.shirt na ubwabwa .ngojeni warudishe gharama za hivi vitu mlivyokula kwanza ,salio likiwepo mtakumbukwa 2014 ama 2015 mmesikia!mateka wa magamba nyie!wacha cha moto mkipate mpaka akili ziwazibuke!
 
Wakati wa kuchagua Mnadanganywa mnadanganyika..Acha kupiga Mayowe..huo ni mshahara wa kutokufikiri kwenu
 
huko CUF ndo itaeleweka sio cdm

CUF yenyewe kama CCM B. Watu wa majimbo mengi ya pwani,na kusini mashariki,kama Lindi na Mtwara,kuna nguvu ya wana CUF zaidi. Hata CCM hushinda kwa kuchakachua! Ila kutokana na 'propaganda kali..',wana CUF bora waipigie CCM kuliko Chadema....!
 
Huyo Mbunge wenu Kimeo!

Nilishangaa siku alivyokuwa anatumika na akina Mtemvu kushabikia hoja ya UDA. Jamaa alitumia mda wake wote akiongea kwa jazba juu ya usafiri dar es salaam, Huku akisahau wananchi wake hawana usafiri wa uhakika wa boti ya kusafiria, akisahau kukumbushia ahadi aliyoitoa Rais Kikwete juu ya kukamilisha gati la mafia ifikapo februari 2011. Akisahau kukumbusha ahadi ya serikali kuipatia Mafia chuo cha ufundi, shule ya kidato cha Tano nk.

Mnachotakiwa hapo ni kuikataa CCM, sio mbunge pekee!

Hata huyo Omari kimbau mnaemsema si Kiongozi kama mnavyofikiria, mtakuja kulia mara mbili! Tuulizeni sisi mjini huku!
KIkwete is a liar big time aiseee.....hamuogopi hata Mungu huyu jamaa
 
Mnatakiwa muikatae CCM kwa ujumla wake sio tu huyo mbunge.

Nilivyokusoma ni kama vile CCM wakileta mgombea mwingine mtamchagua. Kama hivyo ndivyo mtakuwa hamjatatua tatizo!
wakati ni ukuta-----muda ni mwalimu mzuri sana,.........muda umefanya ulambe matapishi yako,hakika muda ni mwalimu wa haki
 
Back
Top Bottom