Kisukari, presha na kansa ni hatari, kwanini watu wanaogopa UKIMWI zaidi?

Ni ile dhana tu VVU/UKIMWI kuambukizana kwa njia ya ngono, pipo zinachukulia kama ugonjwa wa kujitakia...... Hayo magonjwa mengine watu hawana time nayo wakijua kupata kwayo ni nguvu za Rabana na si kwa utashi wao
 
tatizo ni chanzo kikuu cha kuambukiza UKIMWI ndio kinaletaga ukakasi
 
Nadhani umeshanielewa.


'unadhani' nimekuelewa eeh. hahaha Mkuu acha kuishi kwa kubashiri kama Rufufu.

Inshu sio kukuelewa. Inshu ni 'usahihi' wa hicho nilichokuelewa.

By the way, ningekuwa nimekuelewa nisingekuuliza.
 
sababu wanaamini ni ugonjwa unatokana na ngono zembe wanaona aibu
shida ni matangazo yaliyofanywa kuhusu ukimwi mfano kulikuwa na tangazo linasema "je unataka kutimiza ndoto zako? hakikisha hauambukizwi HIV " sasa hiyo ndio inajenga tafsiri kwamba ukipata ukimwi tu ndoto hazitii
 
Wengi wanaamini ni ugonjwa unaopatikana kwa uzinzi/uzinifu na mila na desturi zetu uzinzi/uzinifu no tendo la aibu.uzinifu ni moja ya amri iliyokatazwa na mungu kati ya zile amri 10 kwa baadhi ya waamini was dini Fulani.so kuna Hepatitis b pia ni hatari Zaidi ya yote uliyoyaeleza.
 
ndiyo ugonjwa gani huo
 
Wenye ukimwi wote siku hizi tukikonda, tunasingizia tuna visukari.
 
Tuombe sana kwa Mungu atuepushe na maradhi mbalimbali! Tuwaombee pia wale wanaoumwa,Mungu awaponye na kamwa wasikate tamaa
 
Hizi avatar zingine kaa.Moderators nao mm,yaani wameikubali na wamekaa kimya.
kwa nini mtu akiwa na kisukari ni rahisi kusema kwa jamii ila ukimwi hasemi
 
UKIMWI ni shida ila sio siri nilishauguza wagonjwa wa ukimwi na kansa kwa wakati tofauti .

Mgonjwa wa kansa nilimuonea huruma mpaka nilikuwa namuombea kwa Mungu afe mapema kwa sababu ya shida alizokuwa anazipata.Mbaya zaidi ilikuwa ni kansa ya koo yaani hali wala hanywi kila kitu ni drip tu.
Ila huyu wa UKIMWI alipata shida pale alipoendekeza starehe na kusahau ratiba ya kumeza vidonge vyake.
 
MAGONJWA YOTE NI HATARI KWA MAISHA YA BINADAMU KAMWE HAKUNA UGONJWA NAFUU NDIO MAANA YANATUUA KILA SIKU
 
kwa nini mtu akiwa na kisukari ni rahisi kusema kwa jamii ila ukimwi hasemi
Hasemi kwa sababu tumeaminishwa ukimwi unapatikana kwa ngono zembe...ila kama ni mimi siwezi sema nina UKIMWI kwa sababu sio ugonjwa bali ni mapungufu katika mwili.
 
UKIMWI- upungufu wa kinga mwili.

Upungufu wa kinga mwilini unasababisha magonjwa yote hayo uliyosema hatari!

Upungufu wa kinga mwilini ndio mzizi wa hayo magonjwa..

Wapo sahihi wanapoogopa upungufu wa kinga mwilini..
 
Hayo matatu uliyoyataja si magonjwa ya kuambukiza na ukiyaugua wanaona ni bahati mbaya. Lakini ngoma ni ya kuambukiza na inatokana na zinaa. Kwa kifupi NGOMA inatesa na inadhalilisha
 
UKIMWI- upungufu wa kinga mwili.

Upungufu wa kinga mwilini unasababisha magonjwa yote hayo uliyosema hatari!

Upungufu wa kinga mwilini ndio mzizi wa hayo magonjwa..

Wapo sahihi wanapoogopa upungufu wa kinga mwilini..


The best post in this thread. Mkuu umemaliza kila kitu.
 
hivi ngoma inaweza sababisha shindikizo la damu? au kisukari
 
Ndugu zangu kansa ndio ugonjwa tishio zaidi yaani nauogopa kuliko kitu kingine. Nimempoteza mama yangu mpenzi mwenzi April 2016 kwa ugonjwa wa kansa. Eee Mwenyezi Mungu tunusuru waja wako, na tunaomba mwisho mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…