Kisukari, presha na kansa ni hatari, kwanini watu wanaogopa UKIMWI zaidi?

Kisukari, presha na kansa ni hatari, kwanini watu wanaogopa UKIMWI zaidi?

Kansa na kisukari ni hatari sana kuliko hata huo ukimwi,
Kwanza saratani/kansa kufa ndio kupona kwako, kisukari masharti ni mengi mara usile hiki ila kula hiki pekee,

UKIMWI unaruhusiwa kula vingi sana pia hauna mateso kama kisukari labda mhusika asizingatie maelekezo ya daktari,

All in all ugonjwa ni ugonjwa tu, jilinde pia kula vizuri na mazoezi ili kuepuka kisukari na saratani,
Well said mkuu
 
Hatuna elimu ya kutosha juu ya haya magonjwa ndio maana mtu akisiki kansa anaona bora kumbe unateseka mpaka siku ya kufa lakini ukiwa na UKIMWI fuata mashrti tu hata wazima wataondoka wewe ukiwaangalia tu
Yeah kwetu kule nmeshuhudia jamaa mmoja hivi ambaye aligundulika toka miaka ya 1990s kuwa ni muathirika wa Ukimwi lakini mpaka leo hii jamaa yuko anakula maisha tu, wengi wameshakufa yapata miaka 20+
 
Maradhi ya Kisukari yanasumbua sana, ni ugonjwa unaokuuwa bila kujua. Utasikia unaumwa kichwa mara miguu mara mgongo kutahamaki figo zimekufa. Mungu atuokoe.

Mimi ni mhanga namshukuru Mungu naendelea vizuri kwa sasa.
Pole sana mkuu, haya ndo maisha, cha msingi zngatia masharti na maelekezo ya dr.
 
shida ni matangazo yaliyofanywa kuhusu ukimwi mfano kulikuwa na tangazo linasema "je unataka kutimiza ndoto zako? hakikisha hauambukizwi HIV " sasa hiyo ndio inajenga tafsiri kwamba ukipata ukimwi tu ndoto hazitii
Mmmh dah!! Inakatisha tamaa kabsa aisee
 
Kisukari ni ugonjwa mbaya sana maana unaathiri mpaka mifumo ya uzazi kwa mwanaume(erectile dysfunction) hata ulaji ni masharti kibao
Kweli mkuu,kuna mtoto wa jirani hapa anaumwa kisukari sasa ana kiuka masharti kwenye ulaji kimemmaliza mwili wote yani amebaki mifupa tu
 
Kweli mkuu,kuna mtoto wa jirani hapa anaumwa kisukari sasa ana kiuka masharti kimemmaliza mwili wote yani amebaki mifupa tu
Haya magonjwa ni noma sana, kisukari kwa sasa ndio tishio kwa sababu ya ulaji mbovu hasa kwa watu wazima, hii ni kwa kuwa:-
1.watu walio wengi wameboresha maisha hivyo matumizi ya vyakula vya kusindika(super market) yameongezeka, hivyo kupuuza ulaji wa vyakula vya asili. Ndio maana tatizo la kisukari lipo sana mijini na sio vijijini/shamba.

2.usafiri, suala la usafiri ni wazi kuwa mijini matumizi ya magari ni makubwa ikilinganishwa na vijijini ambapo watu hutembea angalau umbali fulani katika shughuli zao za kila siku hivyo kuipa miili yao mazoezi. Hii ni kwa ufupi tu, ndio maana ukweli haupingiki kuwa kesi/matatizo ya kisukari na kansa yapo sana mijini na si vijijini.
 
Haya magonjwa ni noma sana, kisukari kwa sasa ndio tishio kwa sababu ya ulaji mbovu hasa kwa watu wazima, hii ni kwa kuwa:-
1.watu walio wengi wameboresha maisha hivyo matumizi ya vyakula vya kusindika(super market) yameongezeka, hivyo kupuuza ulaji wa vyakula vya asili. Ndio maana tatizo la kisukari lipo sana mijini na sio vijijini/shamba.

2.usafiri, suala la usafiri ni wazi kuwa mijini matumizi ya magari ni makubwa ikilinganishwa na vijijini ambapo watu hutembea angalau umbali fulani katika shughuli zao za kila siku hivyo kuipa miili yao mazoezi. Hii ni kwa ufupi tu, ndio maana ukweli haupingiki kuwa kesi/matatizo ya kisukari na kansa yapo sana mijini na si vijijini.
Kweli kabisa mjini wagonjwa wa kisukari na kansa ni wengi sana nowdays tena kisukari si wazee tu wala watu wazima kimewakumba hata watoto wadogo walio under 18.
 
Kuna magonjwa yamekuja kwa kasi kwa sasa kama kansa na sugar ukipata sukari ni hatari maana ukipata kidonda kupona ni kazi pia inakimbilia chini, huwezi kufanya kwa ufanisi tendo la ndoa kwa kansa kupona haiwezekani labda kwa maombi.

Pia serekali imewatupa watu hawa maana dawa zake ni gharama sana za kupunguza makali ila sasa kwenye ukimwi dawa huu ugonjwa ukitumia dawa vizuri za kupunguza makali unaweza ishi miaka 30 ila umekua ugonjwa wanaougopa sana tofauti na kansa presha na kisukari hii inatokana na nini wadau?
Mkuu ni kweli unavyosema kuwa Serikali zetu za nchi za Kiafrika zimefumba macho magonjwa hayo hatari kuliko ugonjwa wa ukimwi. Kwa sababu Serikali za kiafrika zinafanya biashara na wanao uza madawa ya kuweza kutibu hayo maradhi ndio maana Serikali za nchi za Kiafrika zimeyafumbia macho na kutosema chochote kuhusu tahadhari za hayo magonjwa Presha Maradhi ya Saratani na Maradhi ya Kisukari.Na watu wengi wanakufa kwa hayo Maradhi Duniani kote haswa kwa nchi zetu za dunia ya 3 haswa bara la Afrika na bara la Asia kuna wagonjwa wengi wa maradhi ya Saratani, Maradhi Ya Presha na maradhi ya Kisukari. Inatakikana Seriakli zetu zipige vita hayo maradhi ili kupunguwe na vifo vya watu zaidi. Mmi ninazo dawa za kuweza kuyatibu hayo maradhi kwa mtu mwenye Maradhi ya Saratani (Cancer) au Maradhi ya Presha BP na ugonjwa wa kisukari (Diabetic) anitafute dawa ninazo za kuweza kumtibu na akapona akitumia dawa zangu ukihitaji Matibabu toka kwangu waweza kunitafuta kwa njia mbili njia ya kwanza unaweza kunitumia Barua ya Pepe Email Address yangu hii hapa fewgoodman@hotmai.com na njia ya pili ni hii hapa unaweza kuni add kwenye What's App yako au viber yako kwa namba hii hapa +90-534-450-81-69 Tupate kuzungumza live asante.
 
Back
Top Bottom