Kisutu, Dar: Hukumu ya Kesi namba 456 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums kutolewa Januari 22, 2020

Kisutu, Dar: Hukumu ya Kesi namba 456 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums kutolewa Januari 22, 2020

Nakung'uta dua leo usiku kucha zile kwenda mbele na kurudi kinyumenyume, Maxence lazima awe huru Mungu akipenda.
 
Mimi naifuta hiyo kesi na kuwashitaki wote kwa Mungu alie juu. Nijamii forum imesaidia serikali kumulika majizi na mafedhuli serikalini. Kamwe hawawez shindana na umma wa wana jamiiforum. Amen
 
Kesho nitajihimu kufika hapo mahakamani. Jf ndio sehemu pekee siwezi kukaa bila kuingia kupata habari.
 
Mungu ibariki JF, Mungu mbariki Max Melo

Hebu tuisome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) nikinukuu "Kila mtu yuko huru kuwa na maoni yake na kutoa nje mawazo yake, kupokea na kutoa habari, kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi na pia mawasiliano yake kutoingiliwa kati na chombo chochote kile" mwisho wa kunukuu
 
Kesho hukumu saa ngapi ,kwa tuliopo city center tujitahidi kuwepo kuwatia moyo vijana wetu wakina max na mushi
Japo naamini tutashinda
 
Hizi zama si za mzaha, niguse kwa bahati mbaya nikuumize makusudi.

Kwa kuwa JF ni miongoni mwa vyombo huru kutoa maoni,na kwa bahati mbaya JF kwa muundo ipo neutral si rahisi mtu akasifiwa pekee na kinyume chache pia.

Tutarajie watesi watumie hii fursa.
 
Back
Top Bottom