Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tunarudi nyuma
Kichwa chako kibovu, sasa umefurahia nini? Kuumiza watu kwa DPP kuwa anedendele kuwepo? Kichwa chako kibovu klumbe: Kamfuate kati li Jiwe mshangilie.....Hahahaaaa.......kumbe bado ni DPP!
Chadema mkuje huku mkiongozwa na Mrangi!!
Hahahaaaa...... Na wewe pia Eid Mubarak bwashee!Kichwa chako kibovu, sasa umefurahia nini? Kuumiza watu kwa DPP kuwa anedendele kuwepo? Kichwa chako kibovu klumbe: Kamfuate kati li Jiwe mshangilie.....
Eid Mubarak rafiki johnthebaptist
wenzako bado tupo mbeleTunarudi nyuma
Yule Kamishna mkuu wa Idara ya Sheria Uhamiaji naona nae Jana wamemuachia kimyakimya.Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, leo Alhamisi imewaachia huru, aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na Mkurugenzi wa Logistiki, Byekwaso Tabura. Hatua hiyo imefikiwa Baada ya aliyekuwa DPP, Biswalo Mganga kutokuonesha nia ya kuendelea na kesi dhidi yao.
Upande wa Jamhuri uliwasilisha maombi ya DPP mahakamani kwamba hana nia ya kuendelea kuwashtaki vigogo hao dhidi ya kesi ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa inawakabili.
Mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kassian Matembele, ilipokea maombi hayo mapema leo.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliomba kuwasilisha hati hiyo iliyotiwa saini Mei 10, 2021 na aliyekuwa DPP (kwa sasa Jaji mteule), Biswalo Mganga.
Hati hiyo ilisainiwa chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20 iliyofanyiwa mapitio mwaka 2019.
Tarehe 05/06/2020 aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu na mwenzake, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la utakatishaji fedha zaidi ya Sh bilioni 1.6. Sambamba na Bwanakunu, mwingine ni aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Logistiki MSD, Byekwaso Tabura.
Wote walifikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate. Wakili wa Serikali, Faraji Nguka akiwasomea mashtaka washtakiwa hao, alidai kuwa kati ya Juai 1, 2016 na Juni 30, 2019 maeneo mbalimbali ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma, kwa pamoja walitengeneza genge la uhalifu kwa ajili ya kujipatia faida.
Katika shtaka la pili ilidaiwa kuwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 20, 2019, washtakiwa wote kwa pamoja waliisababishia MSD hasara ya Sh 3,816,727,112.75.
Shitaka la tatu ambalo linamkabili Bwanakunu ni matumizi mabaya ya madaraka, ambapo ilidaiwa kuwa kati ya Julai 1, 2916 na June 30, 2019 katika maeneo ya Keko wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam, kwa makusudi alitumia nafasi yake kulipa kiasi cha Sh 3,816,727,112.75 kwa wafanyakazi wa MSD kama nyongeza ya mishahara na posho, bila ruhusa ya Katibu Mkuu Utumishi, na hivyo kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya kiasi hicho cha fedha.
Katika shtaka la nne, washtakiwa wote wanadaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 katika maeneo ya tofauti ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa pamoja waliruhusu uhifadhi mbaya wa vifaa tiba, uliosababisha vifaa hivyo kuharibika, hivyo kuisababishia MSD hasara ya Sh 85,199,879.65
Shitaka la tano linalowakabili washtakiwa hao ni utakatishaji fedha, ambapo inadaiwa kati ya Julai 1, 2016 na Juni 30, 2019 katika maeneo ya Keko Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam, wote kwa pamoja walijipatia Sh 1,603,991,095.37 wakijua fedha hizo ni zao la uhalifu, ambao ni kuongoza genge la uhalifu.
Zaidi;
Vigogo wawili wa Bohari ya Dawa (MSD) kufikishwa Mahakamani leo
Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurian Bwanakunu pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Lojistiki Byekwaso Tabura watafikishwa Mahakama ya Kisutu kujibu mashtaka yanayowakabili. Taarifa iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema wanakabiliwa na mashtaka...www.jamiiforums.com
Uonevu wa magufuli hauta sahaulika kamwe.Hahahaaaa.......kumbe bado ni DPP!
Chadema mkuje huku mkiongozwa na Mrangi!!
Rudini tuTunarudi nyuma
Ofisi ya DPP inazidi kuonesha kuwa kuna kesi nyingi hazikutakiwa kufika mahakamani wala watu kuozea mahabusu na magerezani.
Mfumo wa "Haki za Jinai " Criminal Justice System ya Tanzania unabidi ufumuliwe ili usitumike kukomoa, kunyima watu dhamana au kuswekwa mahabusu wakati upelelezi hauna ushahidi wa kutosha wakati kesi hiyo haitishii usalama wa taifa au watu.
Fidia zipi hizo? Hao wote Convicts tu sema wameonewa huruma!Awalipe fidia sasa.Ni aibu kumweka mtu ndani kisha unakosa ushahidi unamuachia.Civilized country ushahidi kwanza kisha ndo unashikiliwa
Leta ushahidi na sio majungu. Watu wanachafuliwa, wengine mnashangilio. Huu ni wakati wa haki.Fidia zipi hizo? Hao wote Convicts tu sema wameonewa huruma!
Haki ipi mzeeLeta ushahidi na sio majungu. Watu wanachafuliwa, wengine mnashangilio. Huu ni wakati wa haki.
Inakera Sana KiukweliKesi za hovyo hovyo sana hizi! Dah eti hana nia ya kuendelea na kesi hizo. Pumbavu kabisa!