Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mwandishi wa Habari za uchunguzi, Erick Kabendera amefikishwa Mahakama ya Kisutu leo
Anashtakiwa kwa makosa matatu chini ya sheria uhujumu Uchumi ambayo ni...
1. Kujihusisha na mtandao wa uharifu, 2015-2019 katika maeneo ya Dar Es Salaam aliongoza kundi la uhalifu kwa lengo la kupata faida au manufaa mengine
2. Kukwepa kulipa kodi. Katika tarehe tofauti kati ya 2015 hadi 2019 katika jiji la Dar es Salaam alikwepa kulipa kodi zaidi ya Tsh milioni 173
3. Kutakatisha fedha haramu.
Erick Kabendera asomewa mashtaka mahakamani Tanzania
Mwandishi habari Tanzania Erick Kabendera amepandishwa kizimbani kusomewa mashtaka mapya matatu ya ubadhirifu wa kiuchumi .
Katika mashtaka hayo Kabendera anatuhumiwa na kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja za kitanzania.
Kosa la tatu ni la utakatishaji fedha zenye thamani ya zaidi ya millioni mia moja na sabini.
Kwa mujibu wa mashtaka yaliowasilishwa, Kabendera anadaiwa kuyatekeleza hayo baina ya Januari 2015 na Julai mwaka huu mjini Dar Es Salaam na kwa baadhi ya makosa anadaiwa kuyafanya kwa ushirikiano wa watu ambao hawakuwepo mahakamani leo.
Makosa yote hayana dhamana.
Mawakili wake wameondoa ombi la dhamana kutokana na mashtaka hayo mapya.
Akizungumza na waandishi habari punde baada ya Kabendera kusomewa mashtaka, wakili wake Jebra Kambole amesema
'Wakati Erick anakamatwa siku ya kwanza aliambiwa kosa lake ni la uhamiaji, akapelekwa kwenye mamlaka za uhamiaji, akahojiwa, pasipoti yake ikachukuliwa. Uhamiaji wakamkabidhi kwa jeshi la polisi makao makuu Central Jeshi la Polisi wakamhoji kwa makosa ya uchochezi.
'Kuanzia hapo hajawahi kuhojiwa kwa makosa mengine zaidi ya hayo' amesema Jebra Kambole.
Amefafanuwa kwamba kutokana na kwamba mashtaka aliyosomewa Kabendera hayana, ameshindwa kutoka leo.
'Tunachofanya sasa, ni kuangalia upelelezi unafanyika kwa wakati' ameeleza Wakili huyo.
Kesi dhidi ya Erick Kabendera inatarajiwa kusikilizwa Agosti 19.
'Kwanini tulimkamata Kabendera'
Erick Kabendera mwandishi habari anayeandika magazeti ya ndani na nje ya Tanzania alikamatwa Jumtatu 29 Julai wiki iliopita na watu waliojitambulisha kuwa ni maafisa wa polisi.
Katika mkutano na vyombo vya habari, kamanda wa polisi kanda maalum ya mji wa Dar Lazaro Mambossasa amesema kuwa mshukiwa huyo alikaidi agizo la polisi la kufika mbele yao kwa ajili ya mahojiano.
''Mwandishi huyu aliitwa hakutekwa lakini kwa ujeuri alikaidi wito huo.... kimsingi pengine iwapo angewasili angehojiwa na kuachiliwa'', alisema Mambossasa
Matukio yalivyojiri:
Julai 29:
Taarifa kuhusu kutoweka kwa Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera zachipuka Tanzania.
Kulikuwa na utata wa awali kuhusu iwapo ametekewa na watu wasiojulikana kama ilivyo kwa baadhi ya visa vya kutoweka kwa watu Tanzamnia tangu 2015 na kutojulikana waliko hadi leo.
Kamati inayolinda waandishi wa habari barani Afrika (CPJ) kupitia ujumbe huu wa Twitter ilisema inachunguza taarifa ya kutoweka kwa mwandishi wa habari za uchunguzi nchini Tanzania Erick Kabendera aliyechukuliwa kutoka nyumbani kwake na "watu wasiojulikana " na mahala aliko hakufahamaiki.
Hili lilizidi mshindo kutokana na taarifa kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki zake walioeleza kuwa alichukuliwa kwa nguvu na watu kutoka kwake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam eneo la Mbweni.
Julai 30:
Polisi nchini Tanzania yasema kuwa mwanahabari wa Erick Kabendera aliyedaiwa kutoweka - hakutekwa bali amekamatwa.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya mji wa Dar Lazaro Mambossasa amesema polisi wanafanya uchunguzi kuhusu uraia wa mwandishi huyo kwa ushirikiano wa idara ya uhamiaji kabla ya kumwasilisha mahakamani.
Julai 31:
Siku mbili baadaye, Idara ya uhamiaji ilithibitisha kuwa inamshikilia Kabendera kutokana na kuwa na mashaka na uraia wake, kamishna wa uraia na mdhibiti wa pasi Gerald Kihinga amethibitisha.
Idara ya uhamiaji imesema kama chombo kilichopewa dhamana ya kusimamia na kutekeleza sheria ya uraia ya Tanzania, inayo mamlaka ya kuchunguza na kuthibitisha uraia wa mtu yeyote anayetiliwa mashaka baada ya kupokea taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali.
Idara ya uhamiaji ilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu utata wa uraia wa Bwana Erick Kabendera.
''Baada ya idara kupata taarifa hizo ilianzakuzifanyia kazi.Hata hivyo, Bwana Kabendera mwenyewe hajawahi kuhojiwa kuhusu uraia wake, kwa kuwa hakufika ofisini pamoja na kutumiwa wito mara kadhaa wa kumtaka kufika ofisini kwa mahojiano'' Ilieleza taarifa ya Idara ya uhamiaji.
Julai 31:
Mke wa mwandishi Erick Kabendera aliruhusiwa kumuona mume wake Erick Kabendera siku mbili baada ya kamatwa na jeshi la Polisi siku ya Jumatatu jioni nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaaam.
Polisi walimsindikiza Kabendera nyumbani kwake kwa ajili ya kupata nyaraka za uthibitisho wa uraia wake.
Agosti 3:
Mama ya mwanahabari Eric Kabendera, Verdiana Mujwahuzi, 80 amezungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza tangu mwanawe akamatwe.
Amepinga kauli ya polisi kuhusu uraia wa mwanawe.
''Kabendera ni mwanangu, nilimzaa hapa Tanzania na hapajawahi kuwa na utata kuhusu anakotoka, polisi iseme ukweli inamshikilia kwa nini'' aliliambia Gazeti la The Citizen nchini Tanzania.
Gazeti la Citizen liliripoti kuwa Siku ya Jumatano Mama Mujwahuzi alihojiwa na watu kumi amabo alifahamishwa baadae ni maafisa wa uhamiaji waliotaka kuthibitisha uraia wa mwanawe.
Soma: Breaking News: - Erick Kabendera aachiwa huru baada ya kukiri makosa na kufutiwa shtaka