Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Hatimaye, Erick Kabendera kukosa dhamana kwa kosa la kutakatisha pesa. Yajayo yako vyema sana...
Halafu unaunga mkono huu utawala...My brother my University mate emb jitafakari. Ukiona utawala unaojisifia sana, kuminya uhuru wa kusema, kuwepo makesi ya ajabu kwa watu makini na watu kupotea hovyo jua kuwa huo ni UTAWALA WA KIDIKTETA kama zile za kina Idd Amin! Hazina tofauti yoyote ile!

"Udikteta ni utawala wa kikundi kidogo cha watu ambao neno la mkuu wao ndiyo sheria na halihojiwi popote pale"
 
Mwandishi wa Habari za uchunguzi, Erick Kabendera amefikishwa mahakama ya Kisutu leo

Anashtakiwa kwa makosa matatu ambayo ni...

1. Kujihusisha na mtandao wa uharifu, 2015-2019 katika maeneo ya Dar Es Salaam, katoa msaada katika genge la uharifu

2. Kukwepa kulipa kodi. Katika tarehe tofauti kati a2015 hadi 2019 katika jiji la Dar es Salaam alikwepa kulipa kodi zaidi ya Tsh milioni 173

3. Kutakatisha fedha haramu.
Ndiyo maana alikuwa anaichafua serikali ili afiche uovu wake.
 
He was too stupid/naive kuandika makala kama zile halafu unaishi bongo na unaona kinachoendelea..He had it coming to him

Angeweza kuandika makala kama zile under a false ID, pia unaweza kufuatilia kila kitu bongo ukiwa nje, dunia ni kijiji hiki, zile makala zake zilikuwa zinachambua tu hotuba za magufuli, miradi anayoifanya na sera zake ambazo hata ukiwa Australia huko ukifuatilia utafahamu tu, au unaweza kuniambia ni vitu gani aliandika ambavyo mtu ukiwa nje huwezi kuvijua? vyote vipo wazi tu, sema yeye ameandika katika kuvikosoa

pia unaweza kuwa na watu wako bongo wanaokupa taarifa za ndani ambazo haziwekwi kwa waandishi, akina Mange kimambi, Ngurumo wanapata intel nzuri tu na wapo nje, hivyo ndivyo waandishi pragmatic, wanavyoishi kulingana na uhalisia wa hali, sio kujifanya unakufa kishujaa, kesho wanakusahau, unaacha familia inateseka na hakuna mabadiliko yoyote uliyofanikiwa kuyaleta sababu ulienda kiboya
 
Unavyoongea hivyo, una taarifa kamili kuhusu kesi hii.
Wakikuonesha ma transaction kwenye account yake jinsi yalivyo, utabishaa???
Tukae kimya, huku vyombo vya nchi vikiendelea kutenda haki.
Chifu hatukatai hilo usemalo,lakini tukumbuke miaka iyo yote ya nyuma walikuwa wapi,alichokamatiwa mwanzo walisema ni Uraia mambosasa alipotudhibitishia sasa hili la ukatishaji na hilo genge la uhalifu linakujaje hapo na hilo genge hao waliokuwa wanashirikiana nao wako wapi ?
 
Hatimaye, Erick Kabendera kukosa dhamana kwa kosa la kutakatisha fedha. Kisheria, kosa la utakatishaji fedha halina dhamana. Ni kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake tu mahakamani. Yajayo yako vyema sana...

Kwa hiyo wamemshitaki kwa hilo kosa la utakatishaji fedha ili akose dhamana?

Halafu utakatishaji fedha si kosa baya kihivyo mpaka lisiwe na dhamana.

Sheria ya kipumbavu kabisa hiyo.
 
Back
Top Bottom