Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Hatimaye, Erick Kabendera kukosa dhamana kwa kosa la kutakatisha fedha. Kisheria, kosa la utakatishaji fedha halina dhamana. Ni kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake tu mahakamani. Yajayo yako vyema sana...
Wewe kama mwanasheria nadhani kuna haja ya kuangalia sheria hii kwa mapana,
Kama inawezekana basi ibadilishwe ili kosa lolote liweze kupata dhamana,
Inasikitisha kijana wa watu anauguliwa na mama yake
 
Halafu kinachoniboa kwa hizi kesi zao uchwara utakuta wanamsumbuaa mara ushahidi haujakamilika sijui upelelezi. Halafu mara afutiwe mashitaka kisha akamatwe tena! Yani ni full vurugu mechi. Ila naye Kabendera aliona jinsi huu utawala ulivyo then anaandika vile na kusalia Tanzania! Ashukuru Mungu hakuuawa ingawa mida ya usiku safari za STAKI SHARI zitamuhusu na kule ni kilio na kusaga meno. Wapo waliopelekwa kule na bahati mbaya sana au bila mpigaji kujua (Maana kuna giza sana) anashusha rungu sehemu mbaya na wengine wanapigwa vibaya wanaondoka jumla baadaye tunakutana ufukweni mwa bahari! Sitosahau kile kipindi aisee eti tunaambiwa ni raia haramu!
 
Hakuna tatizo, kama inadaiwa alikuwa mkwepa kodi na mdhamini wa uhalifu sheria itafuatwa bila shuruti na atapata haki yake kwenye mahakama zetu huru.
 
Hawa jamaa wakikutafuta..., mwisho wa siku watakupata tu....

Hii inanikumbusha story ya kondoo na mbwa mwitu.., baada ya Mbwa mwitu kumwambia Kondoo lazima nikufanye Kitoweo sababu ulinitukana mwaka juzi..., Kondoo akajibu mwaka juzi nilikuwa sijazaliwa.., Mbwa Mwitu akajibu haina shaka kama haukuwa wewe basi itakuwa alikuwa mjomba wako...

Conclusion.., You are damned either way..., na hii dunia ya wote tunaishi kwenye nyumba za vioo wakiamua kurusha mawe lazima yakupate tu...
 
Duuh wanamuundia kesi isiyo na dhamana...Halafu haiwezekani mashtaka yote yaanzie 2015 hadi 2019.. Kwani enzi za JK alikuwa wapi? Hayo mashtaka ni ya kupika! Halafu mbona hakuna uchochezi badala yake amehusishwa na magenge ya kihalifu? Hao wenzake mbona hawajakamatwa kama wamejiridhisha kuwapo hayo magenge?

Kama alikuwa mwandishi wa the economist si alikuwa analipwa, na kama alilipwa hiyo pesa ilipitia wapi, kodi alilipa kutokana na hayo malipo? Kama alipata malipo kwa kujificha sasa ndio faida yake, ni sawa n pesa haramu, angejisajiri kama mwandishi wa the Economist akajulikana na akalipa kodi isingejuwa shida, mengine yangevumilika.
 
Unavyoongea hivyo, una taarifa kamili kuhusu kesi hii??
Wakikuonesha ma transaction kwenye account yake jinsi yalivyo, utabishaa???
Tukae kimya, huku vyombo vya nchi vikiendelea kutenda haki.
kila mkosoaji wa awamu ya tano lazima lazima apate heka heka...hapa ndipo tunaweka mashaka kama hata haya mashtaka ni ya ukweli.

sasa jamani watu 50m nchi nzima wote tuwe na mawazo sawa sawa kweli, tunakwenda kujenga Taifa gani??
 
Back
Top Bottom