Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Tanzanite tv hata isipolipa kodi iko very clean!

Ndiyo maana yake kiasi hata serikali iliahidi kuwawezesha waandishi wa habari wakujitegemea 'fukara' wapate zana za kazi ili kufanya kazi nzuri ktk mkutano wa SADC.
Ila ukienda kinyume na wenye mamlaka kwa kuandika habari zinazoonekana kuichafua nchi lolote linaweza kuibuliwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
 
Unavyoongea hivyo, una taarifa kamili kuhusu kesi hii??
Wakikuonesha ma transaction kwenye account yake jinsi yalivyo, utabishaa???
Tukae kimya, huku vyombo vya nchi vikiendelea kutenda haki.
Unapokuwa muongo sanaa,na watu wakakujua hivyo,siku ukisema ukweli utaonekana mwongo tu!

There is no way watatuaminisha kuwa jamaa ametenda makosa hayo,kwa sababu tangu awali,kuanzia kumkamata na mashtaka yanavyobadilishwa badilishwa,inaonyesha wazi kuwa hapakuwa na kosa la kisheria lililopelekea kukamatwa kwake,wametafuta makosa ya kumshtakia kwayo baada ya kumkamata.
Kila ubaya una mwisho wake,na kila dhamira ovu ina malipo yake!
 
Mungu wetu hadhihakiwi yu anaona yote na hakika, hakika ipo siku wote wanaofanya ubatili huu watalipa, tena kwa machungu makubwa kuliko haya wanayo wasababishia watu. Wakati si ukuta..
 
Mkulu. Siwezi kuwasemea familia yake nini kiliwajulisha kuwa ndg yao alitekwa.
Labda waweza kupata ukweli wa hilo kutoka kwa wana familia hiyo.
Kwa kweli nawapa pole kwa maana hiki ni kipindi kigumu kwao.


Utakuwa mtu wa ajabu sana karma huelewi hili. Yaani waje watu na silaha na hawataki kujitambulisha kisha wamchukue ndugu yako kinguvu bila kuwapa sababu na uishie kusema hizo ni hisia tupu? Huu ndio mwisho wa ubinadamu wako? Taratibu za kumkamata mtu si zinaeleweka wazi kisheria?
 
Naisi wewe ni mgeni wa siasa za inji hii in latonga mrema voice.
Hivi hauoni visa wapinzani wanavyofanyiwa na serikali na vikarogosi vyake?
 
Aisee nimejiridhisha kuwa walitaka kumuua na kweli huenda Azory ali "Disappear and died"
Tanzania salama ni muhimu sana kuliko Azory Ngwanda,kama hutaki acha
 
Hatimaye, Erick Kabendera kukosa dhamana kwa kosa la kutakatisha fedha. Kisheria, kosa la utakatishaji fedha halina dhamana. Ni kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake tu mahakamani. Yajayo yako vyema sana...
Kapewa stahiki yake ,nimefurahi sana [emoji106]
 
Hahahahhah unaona eeeh. Waliogopa kipigo cha mbwa mwitu.
 
Naisi wewe ni mgeni wa siasa za inji hii in latonga mrema voice.
Hivi hauoni visa wapinzani wanavyofanyiwa na serikali na vikarogosi vyake?
Mange aliwaambia muandamane,mkajifungia ndani. Nguvu moja tu nayo ni ya wananchi ndo huwa haishindwi.
 
Nchi yetu imekuwa ngumu sana kuishi nyakati hizi.

Baada ya Kumkosa Kwenye Zile Dana Dana za "Uraia" wameona wamkomeshe kwa Mashtaka Magumu yasiyo kuwa na dhamana.


Mungu awatie ujasiri wale wote walioa amua kwa dhati kutetea Uhuru wetu wakutoa maoni na Kumkosoa awaye yote bila kujali wadhifa wake.
 
Dahhh , Injustice again
 
Kutakatisha pesa? Ishu ya uraia umeishia wapi?

Naona wameamua kumkomoa mshikaji.
Acha watu wenye kazi zao wafanye kazi, sio kila kitu ni habari, fatilia kesi then useme kama kaonewa au haki imetendeka, afu nyie watu msiwe na double standards, mtu yuko na maovu kibao watu wanamstahi ili msiongee, anavuka mipaka wanaamua kumshughulikia kwa maovu yake yaleyale anakuwa kaonewa...unamtukana mkuu wa nchi aisee afu ulimwenguni ukitegemea mie huyohuyo nikulinde na nikupatie kila kitu unachohitaji kibinadamu haipo.
 
Kukosa kumuua huyu wanaumia sana vichwa
Walikueleza wanataka kumuua? huyo ndo anatakiwa kutumika kama kielelezo cha ni namna gani hao wanaowatumia wanakiuka sheria za a sovereign state na wanapashwa kulaumiwa na jumuia ya mataifa.
 
Kenya waliiondoa KANU kirahisi sana. Kenya kuna ukabila na ule uchaguzi ulikiwa Kikuyu mmoja aliyeungwa mkono na watu wote wenye nguvu nchini against another Kikuyu aliyekuwa dhaifu. Cha kushukuru ni kuwa Moi aliamua kuwapa wananchi haki yao ili kuepusha mauaji. Ila baadaye si unaona Kibaki alijipa ushindi batili? Ukishakuwa kwenye PAWA unaweza kuamua lolote ilimradi tu busara ikutawale. Hata JK alishasema. Sasa hapa kwetu yupo wa busara kama Moi? Hapa kwetu wapo kina Kibaki ambao kujipa ushindi haramu kulipelekea maelfu kuuawa na kupoteza mali. Ukishakuwa mtawala anayeamini kutokushindwa halafu ukakutana na wananchi waliojichokea basi ndiyo kama hivyo. Ninachoamini swala la utawala wowote ule kuanguka haliwi processed bali huwa linatokea tu unashangaa na minguvu yako unadondokea kule...Mifano hai ni Tunisia na Sudan. Yan kuanguka kwa dola yoyote ile ni huwa kunatokea tu tena ndani ya muda mfupi sana. Hakujawahi kuwa Processed hata kidogo na ndiyo maana Moi na manguvu yake alitokea kujichanganya point ndogo sana. Kama unakumbuka miezi michache kabla ya uchaguzi KANU iliundwa upya ikiwa na kina Raila, Saitoti na wengine ila point moja ya Moi iliisambaratisha na ikawa bai bai... Huwa naamini kuanguka kwa utawala huja kama muujiza. Usishangae hapa 2020 wastaafu wote kuanzia marais wakamkataa JPM na kukatokea kitu cha ajabu kabisa.
 
Hatimaye, Erick Kabendera kukosa dhamana kwa kosa la kutakatisha fedha. Kisheria, kosa la utakatishaji fedha halina dhamana. Ni kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake tu mahakamani. Yajayo yako vyema sana...
Tusubirie mussiber anaweza tamka neno
 
Kwa asilipishwe faini ili sisi wanyonge tujengewe angalau daraja la mabanzi kuliko kumkalisha maabusu asambaze propaganda zake kwa wafungwa wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…