Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Maviii!polisi haiaminiki tena...
Asubuhi wanakukamata kwa kesi ya bhangi mchana wanatangaza umekamatwa na mavi ya fisi... nyara ya taifa!!!
Ili dhamana ikosekane...
Naota ya kwamba yajengwe magereza mengi tu na vitanzi vya kunyongea tusiofanana nao mawazo na pia baada ya yote tuwe na maisha marefu kama Farao...
 
He was too stupid/naive kuandika makala kama zile halafu unaishi bongo na unaona kinachoendelea..He had it coming to him

Angeweza kuandika makala kama zile under a false ID, pia unaweza kufuatilia kila kitu bongo ukiwa nje, dunia ni kijiji hiki, zile makala zake zilikuwa zinachambua tu hotuba za magufuli, miradi anayoifanya na sera zake ambazo hata ukiwa Australia huko ukifuatilia utafahamu tu, au unaweza kuniambia ni vitu gani aliandika ambavyo mtu ukiwa nje huwezi kuvijua? vyote vipo wazi tu, sema yeye ameandika katika kuvikosoa

pia unaweza kuwa na watu wako bongo wanaokupa taarifa za ndani ambazo haziwekwi kwa waandishi, akina Mange kimambi, Ngurumo wanapata intel nzuri tu na wapo nje, hivyo ndivyo waandishi pragmatic, wanavyoishi kulingana na uhalisia wa hali, sio kujifanya unakufa kishujaa, kesho wanakusahau, unaacha familia inateseka na hakuna mabadiliko yoyote uliyofanikiwa kuyaleta sababu ulienda kiboya
Kwahiyo unakubaliana na wanaosema kuwa ameshitakiwa kwa makosa ya kufikirika kwaajili ya kumkomoa kwa aliyoyaandika?

Kama hajashitakiwa kwa alichokiandika basi hicho kilikuwa kizuri ndiyo maana haijawezekana kushitakiwa kwacho.
 
Kwahiyo watu wanyamaze kisa yeye malaika,kama hakutaka kukosolewa angebaki kijijini kwake achunge ngombe burigi aliomba kura ili tumuajiri sasa kapata ajira ndio anakua chinjachinja
Pole Kaka jamani kabla ya kufanya upumbavu muwage mnafikiria na watoto wenu. Sasa watoto wanateseka kisa ujuaji wa baba yao. Yaani huyu hana tofauti na Victoire wa Rwanda aliecha familia yake Uholanzi kisa kwenda kumpinga Kagame. If you cant beat them,then join them.
 
Kwahiyo watu wanyamaze kisa yeye malaika,kama hakutaka kukosolewa angebaki kijijini kwake achunge ngombe burigi aliomba kura ili tumuajiri sasa kapata ajira ndio anakua chinjachinja
Kaka hebu andika maneno haya kwa real identity yako au jirecord na sura yako ukiongea uonekane. If you can't then you know what I mean.
 
Shida ya victoire ni udc,ataandika kusifia ujinga ili aonekane na lumumba
Madame Victoire... unaita taaluma ya Kabendera upumbavu? Kosa lake liko wapi? Yeye ni muandishi wa habari za kiuchunguzi, aliandika kadiri ya uchunguzi wake ulipofikia.
Kosa lake ni kuandika kwa kutumia taaluma yake?
Na kama kila mmoja akifikiria familia yake tutajenga Taifa la namna gani?
 
Kwahiyo watu wanyamaze kisa yeye malaika,kama hakutaka kukosolewa angebaki kijijini kwake achunge ngombe burigi aliomba kura ili tumuajiri sasa kapata ajira ndio anakua chinjachinja
Mkuu kweli kabisa bora tu angebaki kwao achunge ng'ombe maana hataki kukosolewa bora Mkuu tutengeneze group letu LA kupinga vitu hivi kama hutojali nipm no yako tunajenge
 
Let's say nikweli eti Kwamba aliandika Lugha mbaya na isiyofaa kwa Mkuu wa Nchi je Kwanini hajashtakiwa kwa makosa hayo myasemayo kwamba alimuandika vibaya Mnayemuabudu?

Je mashataka haya yasiyo na dhamana aliyofunguliwa ndio mbadala wa shtaka ambalo mnadhani alilistahili?
Naona kuna kasoro kidogo kwenye matumizi ya lugha ya Kiswahili sifahamu level yako ya uelewa.

Mimi ni mpenzi na msomaji wa jarida la Economist na pia ninalipia kusoma (subscription) jarida la "Africa Confidential", hivyo nimesoma makala nyingi za Kabendera kwenye vyombo hivyo.

Nilijiunga na Africa Confidential mwaka 2006 nilipojiunga na JF hivyo nina kahistoria kidogo na jarida hilo na nawafahamu waandishi wake wengi hata kama wanaficha majina.

Kwa kweli makala hizo zinaweza kuwa na lengo jema la kukosoa lakini aliweka maneno ya kashfa na lugha ya dharau kwa kiongozi wa nchi, hapo kakosea sana na amekuwa kama Kashoggi.

Makala aloiandika tarehe 26 Julai (mwezi ulopita) ilikuwa "too critical but worse" na ilikuwa lazima isimamishe kope za walengwa.

Pili, hayo mashtaka alosomewa leo mahakamani mimi na wewe hatufahamu lolote mpaka kesi itapoanza hivyo tuwe na subira.

Mfuatilie Paschal Mayala na jaribu kuelewa aina ya uandishi wake na kama ni mwelewa unaona namaanisha nini katika kumkosoa Kabendera kwamba yeye ni muumini wa chequebook Journalism.
 
Inaumiza sana sana, wajuvi wa mambo mtutabainishie, kukundi cha kihalifu alichokuwa akiongoza ni kipi? Na kilihusika na uhalifu upi?
 
Huyu IBILISI wa Ikulu ameifanya Tanzania iwe si salama kuishi kwa sasa, Nduli Idd Amini alianza hivi hivi. Ndugu zangu anzeni kuchukua hatua haraka.
 
Mkuu acha tu watu wafunguke usijali kaka
Unavyoongea hivyo, una taarifa kamili kuhusu kesi hii??
Wakikuonesha ma transaction kwenye account yake jinsi yalivyo, utabishaa???
Tukae kimya, huku vyombo vya nchi vikiendelea kutenda haki.
 
Hujanielewa hao walifanya hayo wakiwa safi. Sasa wewe unaandika against gouvernement huku unafanya uhalifu,unakwepa kodi. Sasa kosa la kutakatisha pesa halina mdhamana. Atajijua. Unaporusha mawe hakikisha upo safi.
Hivi wewe na Kinana ni yupi ana mizizi ccm ? chunga sana !
 
Lazima usome alama za nyakati kaka,unless hautajali kama familia yako ikipay matokeo.Hapa sio USA kaka.Mange aliwaambia muandamane wote mkajifungia makwenu why ? Kwa sababu mlifikiria kuhusu familia zenu. Sawa ni Dikteta ila ndo Rais wetu.Kama mpo serious uchaguzi 2020 mtoeni kwa kura.
Hivi Tanzania ina watu wa ajabu namna hii?
 
Back
Top Bottom