Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Unavyoongea hivyo, una taarifa kamili kuhusu kesi hii??
Wakikuonesha ma transaction kwenye account yake jinsi yalivyo, utabishaa???
Tukae kimya, huku vyombo vya nchi vikiendelea kutenda haki.

Wamesema ametakatisha fedha 173m hapo na amekwepa kodi ya 173m, kwa uelewa wa kawaida tu utagundua hapa wamepika maana km kakwepa kodi iweje fedha hizo hizo ziwe ndo alitakatisha?
 
......naona kuna kajamaa kamevaa magwanda ya kaki kanamsukuma hapo as if hajui pa kwenda...hawa watu ndio maana hata nimkute njiani simpagi lifti!
 
Kuna Jamaa amesema hapo Juu na tuombe Ufalme Wa Mungu Uje
 
Duuh wanamuundia kesi isiyo na dhamana...Halafu haiwezekani mashtaka yote yaanzie 2015 hadi 2019.. Kwani enzi za JK alikuwa wapi? Hayo mashtaka ni ya kupika! Halafu mbona hakuna uchochezi badala yake amehusishwa na magenge ya kihalifu? Hao wenzake mbona hawajakamatwa kama wamejiridhisha kuwapo hayo magenge?
Hawana lolote mkuu, hakuna masitaka hapa, je swali ya uraia lineishia wapi? tuliambiwa hio ndilo anahojiwea nalo, sasa mambo yamebadilika, ccm hata akili hawana kabisa
 
Nivigumu kuamini aka kutokuamini kwamba anamakosa...juzi wameachiwa watu kwa kubambikiwa kesi huko magerezani Leo iweje kpsa lirudiwe?? Lkn pia inashangaza waandishi wanaounga mkono jitihada wao hawatokei kukamatwa kwa skendo hizi hata musiba angekuwa 'opoza' ingekula kitambogani!!
 
Mwandishi wa Habari za uchunguzi, Erick Kabendera amefikishwa Mahakama ya Kisutu leo

Anashtakiwa kwa makosa matatu chini ya sheria uhujumu Uchumi ambayo ni...

1. Kujihusisha na mtandao wa uharifu, 2015-2019 katika maeneo ya Dar Es Salaam aliongoza kundi la uhalifu kwa lengo la kupata faida au manufaa mengine

2. Kukwepa kulipa kodi. Katika tarehe tofauti kati ya 2015 hadi 2019 katika jiji la Dar es Salaam alikwepa kulipa kodi zaidi ya Tsh milioni 173

3. Kutakatisha fedha haramu.

View attachment 1172905
View attachment 1172906
View attachment 1172907
MASHITAKI YA URAIA YAMEISHA???? sasa ni mengine? kwa kweli hii awamu ya 5
 
Wamesema ametakatisha fedha 173m hapo na amekwepa kodi ya 173m, kwa uelewa wa kawaida tu utagundua hapa wamepika maana km kakwepa kodi iweje fedha hizo hizo ziwe ndo alitakatisha?
Halafu hamna kesi ngumu kupata ushahidi kama ya kutakatisha fedha. Mtu kama alitumia hizo milioni 173 kuwekeza sehemu nyingine ambayo kiuhalisia ndiyo utakatishaji, utajiridhisha vipi kwamba kwa miaka yote minne hakuweza kufanya kazi ya kumuingizia fedha hizo kihalali? Halafu mtu unasema kuwa kakwepa kodi ya milioni173 then hapo hapo unamwambia kutakatisha kiasi hichohicho ilihali kodi ni sehemu ndogo sana ya kipato anachopata mtu chukulia kodi inayosemwa ni 18 asilimia then chukua hiyo M 173 izidishe mara 1.18 uone alikuwa ana uwezo wa ku make kiasi gani hadi useme katakatisha M 173? Ingekuwa kesi ya mtu aliyejipanga kumtia mtu hatiani basi wangemuweka kwenye shitaka la kukwepa kodi wakaondoa hilo la kutakatisha fedha.
 
Target yao iligoma, thank God kwamba bado anaishi. Niliona picha za jamaa jana akiwa kanisani, sijui padri kama alilitafakari vizuri neno la jana, somo la kwanza lilitoka kitabu cha Mhubiri, kwamba vyeo, mamlaka, mali ni ubatili mtupu na hasa vile vinavyokufarakanisha na jamii yako ni UBATILI mtupu
Hata mimi nilimwambia hizi ndege unazonunua zinakufarakanisha na akina KIVYAKO na mungu wao hasikii.
Nikamwambia hizi Hospitali na vituo vya Afya unavyojenga nchi nzima vinakufarakanisha na akina KYAKO na mungu wao hasikii tu
Nikamwambia huu uwanja wa ndege wa Dar es salaam na vingine vyote unavyojenga vinakufarakanisha na akina Kivyako na Mungu wao bado hanisikii tu
Nikamwambia hawa MAFISADI unaowashughulikia unajifarakanisha na akina kivyako na mungu wao bado hanisikii tu.
Nikamwambia hizi flyover na mabarabara unayojenga nchi nzima akina kivyako na mungu wao hawapendi, bado hanisikii
Nikamwambia unavyoshughulikia vyeti feki vya akina kivyako mungu wao hapendi hanisikii tu
Nikamwambia hao watumishi hewa unaowatoa kwenye payrol, ambao akina kivyako walikuwa wanajipatia hela za kuwapa heshima mtaani, mungu wao hapendi hanisikii.
Nikamwambia vingi tu anavyofanya kwa ajili ya ustawi wa wananchi, kwa mungu wa akina kivyako ni ubatili tu.
Bado HASIKII TU.
 
Walikueleza wanataka kumuua? huyo ndo anatakiwa kutumika kama kielelezo cha ni namna gani hao wanaowatumia wanakiuka sheria za a sovereign state na wanapashwa kulaumiwa na jumuia ya mataifa.

kwa hiyo kabendera ni raia wa Tanzania!?
 
Aisee nimejiridhisha kuwa walitaka kumuua na kweli huenda Azory ali "Disappear and died"
Azory is dead, azory aluawa na kutupiwa mamba hapo mto rufiji, huyu ni ile kelele za raia ziliokoas uhai wake, kwani hata saa tungeabiwa ni "wasiojulikana" na polishi wanafanya "uchunguzi" ccm imejaa wanyama ambao wanavalia mili ya binadamu
 
Kwa hiyo wamemshitaki kwa hilo kosa la utakatishaji fedha ili akose dhamana?

Halafu utakatishaji fedha si kosa baya kihivyo mpaka lisiwe na dhamana.

Sheria ya kipumbavu kabisa hiyo.
Wewe mbona kigeugeu kama govi, mara uunge mkono juhudi mara ugeuke yaani hueleweki kama mkojo wa punda, shubamittt
 
Da wameshampa kesi ya kumkomoa hawa watu ni hatari sana.
Si walisema hawamu hii ni marufuku polisi kubambikiza kesi,wanafki sana hawa watu .
 
He was too stupid/naive kuandika makala kama zile halafu unaishi bongo na unaona kinachoendelea..He had it coming to him
kwa hiyo angehamia Uchina halafu awe anaandika ya Bongo, angeyajuaje na yangemhusu nini wakati kahama?

wewe ni coward, mwoga, mwenzako ni brave and patriotic...
 
Kabudi ametuthibitishia hili
Azory was feed to crocodiles hapo river rufiji, what saved this gentleman ni zile kelele watu walipiga wakati anatekwa otherwise angekuwa maiti by now, i dont know many many people ccm will kill to get okay and well with human blood sacrife in order to silence those with diffrent viwes and so, lakini kusidwa kumumaliza lissu ndiko kunauma jiwe sana kabisa kabisa
 
Hatimaye, Erick Kabendera kukosa dhamana kwa kosa la kutakatisha fedha. Kisheria, kosa la utakatishaji fedha halina dhamana. Ni kusubiri kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi yake tu mahakamani. Yajayo yako vyema sana...
Nadhani we ni mmoja wa wanasheria, kwa nini msifungue kesi mahakamani kutaka sheria hii kandamizi ifutwe? Hii ni sheria amabayo haikidhi viwango vya kimataifa, mtu anahukumiwa kabla ya mahakama kutoa hukumu. Hii ni kinyume kabisa na natural justice. Watu wakitaka kukukomoa sasa havi wanafungua kesi za hivi.
 
Back
Top Bottom