Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu

Akipewa nafasi ya kujitetea akumbuke kusema yafuatayo, "Naipongeza serikali ya awamu ya tano maana inafanya kazi kwa uadilifu, tumepata raisi ambae hajawai kutokea na hatokaa atokee kama huyu, hii ni zawadi tumepewa na mwenyezi Mungu, serikali sikivu, serikali ya wanyonge, inayojali maslahi mapana ya wananchi wake, isiyopenda rushwa, na tumuombee Mh akae madarakani hata miaka mia ili atuletee maendeleo, maana hakuna kama huyu, CCM oyeee..baada ya wiki anafutiwa mashtaka yote
 
Wakishindwa uahamiaji watakupata kwenye utakatishaji.. Maisha sio poa
 
Ila kwanini tunatendeana haya yote?


Kwanini kuoneana kwa kiwango hiki?


Hivi tunakusudia kupanda mbegu gani kwa kizazi Cha Erick?


Mtiririko mzima wa hili tukio la Erick kuanzia kukamatwa kwake na Wale watu wasiofahamika na wasio kua na Sare za Kazi ukiunganisha na Matamko yenye mkanganyiko Kati ya RPC na Afisa wa Uhamiaji Kisha Waziri Mwakyembe utaona kabisa kwamba Mashtaka haya Ni "Maalum" yenye dhamira Maalum.


Tuendelee "Kumuombea" yule ambaye daima huomba kuombewa ili ikimpendeza Mungu kikombe hiki kituepuke, kwa namna yoyote atayoona inafaa.


Hii iwe Ni allert kwenu wote ambao mnaishi maisha yasiowafurahisha Wenye mamlaka na Wateule wao, jiepusheni sana na mambo ambayo kwayo yanaweza kutoa mianya ya kubambikiwa ama kupikiwa Mashtaka.

Yupo Mungu wa haki iko siku kila mmoja atatoa hesabu ya matendo yake.
 
Mkuu yule jaji Mkuu alikuwa analalamika utafikiri sio jaji Mkuu.we umepewa meno kuongoza mhimili wa mahakamani unaruhusu vipi kesi kama hizo ziendelee kusikilizwa?
Kwa uwelewa wangu mdogo wa mambo ya sheria nadhani mahakimu na majaji kazi yao ni kusimamia tafsiri ya sheria zilizopo zilizotungwa na Bunge

Hata kama kuna sheria mbaya na akili na moyo wake unaona hivyo lakini majaji na mahakimu wamefungwa mikono hawawezi kuamua nje ya wigo wa sheria hizo
 
Dah Kina Nyerere na Mkwawa wangewaza hivi pengine Victoire wa Tanzania angekuwa utumwani huko Oman kwa sasa analima mashamba ya zile za kufuturia sijui zinaitwaje! nimekumbuka zinaitwa tende
Na angekuja 0713 ningeilalua
 
Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu..plus,
there is a price to pay on every act.
 
Kwa uwelewa wangu mdogo wa mambo ya sheria nadhani mahakimu na majaji kazi yao ni kusimamia tafsiri ya sheria zilizopo zilizotungwa na Bunge

Hata kama kuna sheria mbaya na akili na moyo wake unaona hivyo lakini majaji na mahakimu wamefungwa mikono hawawezi kuamua nje ya wigo wa sheria hizo

Mhakama kuu ina uwezo wa kufuta sheria kama haipo practical lakini hii sheria ipo dunia nzima ispokuwa inatumiwa vibaya. Lakini ikiwa kuna mtu ameshtakiwa kihalali mahakama haina ujanja wala sababu ya kutaka sheria ifutwe. Swala ni kujiridhisha kwamba hapa imetumika sawa hapa sivyo ndo ngoma ipo hapo
 
Wanachofanya ni.kutumia mamlaka vibaya kwa kumkomoa kabendera baada ya kukosa ushahidi kwenye ile kesi ya Uraia.

Mahakama sasa ioneshe ukuu wake kwa kuendesha kesi ya kabendera mfululizo ili apate haki yake bila kuteswa gerezani bila hatia.

Mahakama iamke na kila mwenye kesi isiyo na dhamana,kesi isikilizwe mfululizo ili kuepusha dhulma na uonevu kwa watu wasio na hatia.

Kwa ushahidi wa mazingira Kabendera na wengine wasiopendwa wanapewa kesi ngumu ili kuwakomoa,na kuwaweka rumande muda mrefu kwa lengo la kuwakomoa ili hata wakishinda wawe wameshasota gerezani vyakutosha.

Ardhi yenye dhulma ni laana kwa vizazi
Tusishangilie haya.
 
Hakuna siku iliyokuwa tulivu hasa hapa dar kama siku ya hayo maandamano..,jiji lilikuwa kimya..
na sidhan kama itawahi tokea
Teh teh teh umenikumbusha mbali kuhusu hayo maandamano ya Da Mange.

Watu walichonga sana humu mitandaoni lakini siku ya siku ilipowadia wote wakaufyata wakajifungia makwao huku wakichungulia madirishani kuona kama kuna waliojitokeza kuandamana.

Majasiri wa kwenye mitandao hao!
 
He was too stupid/naive kuandika makala kama zile halafu unaishi bongo na unaona kinachoendelea..He had it coming to him

Angeweza kuandika makala kama zile under a false ID, pia unaweza kufuatilia kila kitu bongo ukiwa nje, dunia ni kijiji hiki, zile makala zake zilikuwa zinachambua tu hotuba za magufuli, miradi anayoifanya na sera zake ambazo hata ukiwa Australia huko ukifuatilia utafahamu tu, au unaweza kuniambia ni vitu gani aliandika ambavyo mtu ukiwa nje huwezi kuvijua? vyote vipo wazi tu, sema yeye ameandika katika kuvikosoa

pia unaweza kuwa na watu wako bongo wanaokupa taarifa za ndani ambazo haziwekwi kwa waandishi, akina Mange kimambi, Ngurumo wanapata intel nzuri tu na wapo nje, hivyo ndivyo waandishi pragmatic, wanavyoishi kulingana na uhalisia wa hali, sio kujifanya unakufa kishujaa, kesho wanakusahau, unaacha familia inateseka na hakuna mabadiliko yoyote uliyofanikiwa kuyaleta sababu ulienda kiboya
Well said, ndio maana nimeamua kujikalia zangu kimya, kwanini nice mbinafsi wa kuwa ninayejiita mwanaharakati niishie pabaya, kisha mwanangu nimuache anateseka. Idiotic thought.
 
Hata mimi nilimwambia hizi ndege unazonunua zinakufarakanisha na akina KIVYAKO na mungu wao hasikii.
Nikamwambia hizi Hospitali na vituo vya Afya unavyojenga nchi nzima vinakufarakanisha na akina KYAKO na mungu wao hasikii tu
Nikamwambia huu uwanja wa ndege wa Dar es salaam na vingine vyote unavyojenga vinakufarakanisha na akina Kivyako na Mungu wao bado hanisikii tu
Nikamwambia hawa MAFISADI unaowashughulikia unajifarakanisha na akina kivyako na mungu wao bado hanisikii tu.
Nikamwambia hizi flyover na mabarabara unayojenga nchi nzima akina kivyako na mungu wao hawapendi, bado hanisikii
Nikamwambia unavyoshughulikia vyeti feki vya akina kivyako mungu wao hapendi hanisikii tu
Nikamwambia hao watumishi hewa unaowatoa kwenye payrol, ambao akina kivyako walikuwa wanajipatia hela za kuwapa heshima mtaani, mungu wao hapendi hanisikii.
Nikamwambia vingi tu anavyofanya kwa ajili ya ustawi wa wananchi, kwa mungu wa akina kivyako ni ubatili tu.
Bado HASIKII TU.
Na kuteka, kuuwa, kubambikia kesi, kupendelea chato na ule ufisadi wa trillion 1.5 ulisahau kumwambia?
 
Pole Kaka jamani kabla ya kufanya upumbavu muwage mnafikiria na watoto wenu. Sasa watoto wanateseka kisa ujuaji wa baba yao. Yaani huyu hana tofauti na Victoire wa Rwanda aliecha familia yake Uholanzi kisa kwenda kumpinga Kagame. If you cant beat them,then join them.
We tulia acha kukebehi
Usijione Malaika hata ww wakati wwte unaweza kwenda huko.......

Ova
 
Back
Top Bottom