Kuchezea fedha za umma ni pamoja na kufungulia watu kesi ambazo kwa macho ya kawaida tu zinaweza kuonekana ni "vexatious" ama za kubambikiana tu.
Hati ya mashtaka ukiisoma, unapata shaka kabisa kwa uundwaji (ama uhalali) wa mashtaka aliyoshtakiwa nayo Bw. Kabendera.
Shtaka la Pili,
Anatuhumiwa kutolipa kodi kwa TRA kiasi cha Tshs. 173,247,047.02/= ambazo ilipaswa azilipe kati ya Januari 2015 na Julai 2019.
Shtaka la Tatu
Anatuhumiwa kuosha fedha (kutakatisha) chafu kiasi cha Tshs. 173,247,047.02/= kati ya Januari 2015 na Julai 2019, ambazo alizipokea huku akijua zinahusika na ukwepaji wa kodi.
Mashaka
1. Kiasi kinachodaiwa katika shtaka la pili ndicho kinachozungumzwa katika shtaka la tatu, sasa kama kweli ishu ni kukwepa kulipa kodi, inashangaza kama kodi inakuwa sawa na kiasi unachotakiwa mtu kulipia kodi..yaani umepata elfu 5 kama kipato na ulipe shilingi elfu 5 kama kodi;
2. Kwenye shtaka la tatu, shtaka ni utakatishaji wa fedha, ingawa kwenye maelezo ya shtaka imesemwa kuwa alipokea hela huku akijua inahusika kwenye ukwepaji wa kodi..sasa serikali inaweza kupokea kodi kutoka hela chafu? Si inakuwa imesafisha hela hizo yenyewe?
Mimi nashauri wanaohusika na mashtaka wawe wanajiridhisha na kushauri "kitaaluma" kabla ya kuyawasilisha mahakamani ili kuepusha gharama zisizo na msingi kwa kesi kuondoshwa mahakamani baadae pamoja na utumikaji mbovu wa kodi zetu wanazolipwa maafisa wakati wa uendeshaji wa kesi ambazo mashtaka yake yanaweza kuwa ni ya kweli, lakini yanayofunguliwa vibaya.