Kisutu: Kesi ya Erick Kabendera yaendelea. Jamhuri yaweka kisiki Erick kushiriki msiba wa mama yake mzazi

Dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inasikitisha sana,epukeni kujiweka hatarini na mambo hayo ya kuungurumishana na serikali. Tukumbuke tu wameshika ncha sie makali
 
Hivi kwa siku zijazo upande wa serikali ukiamua kujitoa kwenye kesi hii vp hatutasema kuwa kesi hii ni ya kutengeneza kwa lengo la kumkomoa Bw Erick???

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo ndivyo ilivyo, unakumbuka kule mkoani mwanza, mwendesha mashtaka wa serrikali alisema hana nia ya kuendelea na kesi ya wale askari waliokuwa wanatuhumiwa kuhusika na uvushaji wa dhahabu ya magendo, walikamatwa kwa mbembwe sana, huku ndugu zao wakizuiliwa kuwaona mahakamani wakati kesi yao ilipokuwa ikiendelea
 
HIVI MNAELEWA MAANA YA HAKI SAWA KWA WOTE?

tusiandike tu bila kuangalia na kesho,Erick kafiiwa na mama yake ni haki yake kbsa kwenda kuzika apelekwe chini ya ulinzi akamzike mama,ni haki yake.

Lakini mmefikiria kuhusu kesho? wewe utakua gerezani mama ako/bibi/baba atafariki je na wewe upelekwe? msitetee kwa sababu erick anajulikana tu,hivi mmewafikiria ambao hawajulikan hata na mwenyekiti wa mtaa kama wewe na mimi?

siku na sisi yakitukuta wazazi/ndugu zetu kufariki je tutapelekwa? na tusipopelekwa tutaona tumetendewa haki na kunyamaza au tutaanza kuhoji "mbona erick alipelekwa"???

Serikali hawezi peleka kila mshtakiwa kumuaga mzazi wake atakaefariki,kama ni hivyo basi ni sawa kwa erick maana si yeye tu ambae kashawahi fiwa na mzazi angali akiwa gerezani,wapo wengi na wanaendelea kuwepo.

Je hao wajao serikali itaweza wasimamia kama erick endapo angepelekwa? kama hawawezi nadhani Erick apewe pole tu na apewe haki yake ya kuona mazishi ya mama japo kwa video akiwa huko huko gerezani lakini yote hayo afanyiwe bila wengine kuona maana treatment atayopewa Erick leo yapasa wapewe watuhumiwa wote "bila upendeleo"
 
Mungu ndiye aliyesema tiini sheria za wanadamu na tiini wenye mamlaka! Huyu kavunja sheria ina maana kavunja amri ya Mungu na wanadamu. Sasa unaposema Mungu atakulipia mi sikuelewi.
jamani eh!! Mshitakiwa siyo mfungwa.. Arghh!
 
Kuna binadamu hawana aibu kabisa. Unambambikia mtu makosa ambayo kila mtu mwenye akili timamu anajua amesingiziwa, unamweka mahabusu miezi na miezi kwa kisingizio upelelezi haujakamilika.
Mtu anashindwa kumuhudumia mama yake mgonjwa na mama huyo anasema kabisa huku analia bila mwanae yeye atakufa anaomba mwanae aachiwe.
Binadamu mwenzetu eventually anampoteza mama yake, anazuiwa hata kwenda kwenye ibada ya kumwaga mama yake achilia mbali kuzika. Yaani mtuhumiwa tu, ananyiwa hivi!

Watu tumekosa utu, tumejaa chuki na ushetani. Tunawaza kutesa wengine, kuua na kujineemesha. Tukumbushane hakuna cha kudumu, tunapita tu.
Binadamu wamekuwa beasts, wanyama pori wakatili. Siku nyingine tukianzisha mbuga mpya kama ya Burigi - Chato, tusipeleke wanyama huko kwa magari, tupeleke binadamu wenzetu ambao wameamua kuwa na roho za kinyama wakaishi huko.
 
Tunaanda njia ambayo baada sana wenyewe tutaijutia kabisa..

Kwanini tulishindwa yazuia hayo yote..

Kuna jambo halipo sawa pahala...watu hawalalamiki tu..
 
what's come around goes around
 
yatalipwa haya
 
huyu mtu ni mshitakiwa mama yake akizikwa hatapata tena nafasi ya kumuona zaidi ya kutembelea kaburi lake ni vema aruhusiwe apate nafasi ya mwisho kutoa heshima kwa mama yake hakuna mtu ajuaye kesho yake

Wote tumezaliwa na mwanamke kama Rais Magufuli alivozaliwa na mwanamke aliye sawa na mama wa Kabendera Bi Mjwahuzi......!!! Kuna siku wote hawa wataiacha hii dunia ni swala la muda tu....!!!

 
December 31, 2019

Angalizo la Askofu Mwamakula kwa waTanzania
Kushiriki dhambi ya Kijamii kwa kuhukumu Watuhumiwa kabla hawajaonekana na Mahakama kuwa wanahatia pasi na shaka yoyote

Ujumbe wa kuelekea Mwaka Mpya wa Askofu Emmaus Mwamakula kwa Jamii bila kujali wana imani au la, ila ujumbe huu ni kwa Jamii yote kiTanzania

Dhambi ambayo Jamii nzima, dhambi ya taasisi na dhambi ya kiTaifa ambayo wote tuna inashiriki kuitenda na kuilinda badala yakuikemea. Katika kemeo hili hakuna anayebaki salama, awe raia wa kawaida au watawala walio mamlakani sote tunapaswa kukemewa. Pia kemeo hili linahusu mtu mmoja mmoja, familia, jamii, pia mfumo na sera mbovu bila kujali mtawala ni nani.

Mfano ktk nafasi zetu tumetumia fursa mbalimbali kupora mali za wengine, tumewaumiza kwa namna mbalimbali wenzetu n.k huku sisi kama jamii nzima tuona lakini hatukemei hivyo tushiriki ktk dhambi hii ya Kijamii.

Jamii ya kiTanzania haijaandaliwa na ndiyo maana kuna upungufu wa maadili iwe kwa viongozi wa kisiasa, wafanyabishara, watu wa media na jamii nzima kwa ujumla na ndiyo maana dhambi hii ya kijamii tunaishiriki bila kujua.

Source: MwanaHALISI TV
 
huyu mtu ni mshitakiwa mama yake akizikwa hatapata tena nafasi ya kumuona zaidi ya kutembelea kaburi lake ni vema aruhusiwe apate nafasi ya mwisho kutoa heshima kwa mama yake hakuna mtu ajuaye kesho yake
Utaratibu ukiwa hivyo basi kila siku mamia ya wafungwa/watuhumiwa watakuwa wanatolewa kwenda kuwazika wazazi/ndugu zao, wakati mzee Nguza Viking yupo gerezani mama yake mzazi alifariki lakini hatukusikia kelele za hivi........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huu ndo tunaita unyama na kutozipa heshima haki za binadamu
siku zote raia huwa upande wa anayeonewa na huruma huwa nyingi sana

kisiasa hili swala limembomoa magufuri
balozi zinashangaa ufedhuri na uhayawani wa awamu hii.
 
Hivi kwa siku zijazo upande wa serikali ukiamua kujitoa kwenye kesi hii vp hatutasema kuwa kesi hii ni ya kutengeneza kwa lengo la kumkomoa Bw Erick???

Sent using Jamii Forums mobile app
Hujanielewa kesi ni ya kutengeneza lakini kosa hasa halitajwi. Jaribu kusoma maelezo yangu tena Mkuu
 

Maagizo ili wasiwaudhi policcm wakashindwa kuwasaidia kupata ushindi kwani ccm na police ni ndugu wa damu yaani baba mmoja na mama mmoja.
 
Mkuu hizi sio Kelele bali ni sauti itokayo nyikani, wewe nani alikuzuia wakati huo kupiga kelele ili Nguza aruhusiwe kwenda kuzika ?,
 
Nani aliwahitoka mahabusu kwenda kwenye mazishi ya mama ama baba yake ama mtoto wake? Kwani watu wangapi waafiwa wakiwa magerezani lini wakaachiwa?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio report ya daktari inavyosema au umejiongeza na kile kimsemo MTANZANIA mpe muktasari tu NEWS anatiririka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…