Kisutu: Maafisa wa EU, UN na Mabalozi wa Marekani, Sweden na Ujerumani wahudhuria Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe

Kisutu: Maafisa wa EU, UN na Mabalozi wa Marekani, Sweden na Ujerumani wahudhuria Kesi ya Ugaidi inayomkabili Freeman Mbowe

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hivyo ndivyo ilivyokuwa leo Mahakamani, ambapo Wadau wa Maendeleo wa Tanzania kutoka kwenye Taasisi za Kimataifa wameshiriki kesi hiyo ya Ugaidi kwa lengo la kujua kinachoendelea, Maofisa hao wengi wao wamefika ili kujiridhisha na mwenendo wa kesi hiyo.

Ugaidi katika nchi ni jambo baya linaloweza kuwatisha wawekezaji , hivyo ilikuwa ni lazima wadau wa maendeleo kuhudhuria kesi hiyo ili kupima kiwango cha ugaidi kwa lengo la kulinda wawekezaji kutoka kwenye nchi zao, maana ni hatari kuwekeza kwenye nchi yenye Ugaidi.

Balozi_wa_Mareka_na_Mabalozi_wengine_wa_nchi_tatu_wamefika_mahakama_ya_hakimu_mkazi_kisutu_Leo...jpg

2880237_AMDRiN.jpg
2880236_Ak88-A.jpg
2880238_AEAEd6.jpg
 
Je walisemaje walipoambiwa haletwi Leo mahakamani kwa sababu magari ni mabovu?
Baada ya IGP na viongozi wa Tanzania kufahamu uwepo wa Mabalozi na maofisa wa EU na UN wakaamua kuweka mpira kwapani kwa kusingizia ubovu wa gari , huku magari ya kusomba wafuasi wa chadema na yale ya washawasha yakiwa mazima
 
Hayo si maandamano aliokataza IGP Sirro??? Mbona vijana wa IGP Sirro wamejikausha hawaja wakamata sasa wala kuwatawanyisha na mabomu ya machozi?

Halafu utakuta hata huyo huyo IGP Sirro ametoa mpaka escort ya police na ulinzi kwa wahusika wa haya maandamano. Aibu ilioje hii.

Ama kweli wahenga walisema "Debe lililo tupu, ndio lenye kelele zaidi". Kelele zote, Vitisho Vyote, Vitimbi Vyote, Uonevu Wote na Kutunishiwa misuli wanafanyiwa wanyonge wasio jiweza na wasio na nguvu ya kujitetea tu nchi hii.
 
Hao mabeberu mnadhani watawasaidia?. Nyumbu mna matatizo Sana.
Mabeberu wamekusaidia haya..

1. Chanjo ya korona. Kama sio wao wewe na mchepuko wako msinge chanjwa.

2. Barabara

3. Reli.

5. Stigla goji

6. Misaada ya elimu..

7. Ujenzi wa vyoo mashuleni baada ya kuona serikali ya ccm haina uwezo.

8. Bajeti ya serikali inawategemea mabeberu.

9. Buku 7 mnazo lipwa pale lumumba zimetoka kwao..

10. Nk nk nk...
 
Hivyo ndivyo ilivyokuwa leo Mahakamani , ambapo Wadau wa Maendeleo wa Tanzania kutoka kwenye Taasisi za Kimataifa wameshiriki kesi hiyo ya Ugaidi kwa lengo la kujua kinachoendelea , Maofisa hao wengi wao wamefika ili kujiridhisha na mwenendo wa kesi hiyo .

Ugaidi katika nchi ni jambo baya linaloweza kuwatisha wawekezaji , hivyo ilikuwa ni lazima wadau wa maendeleo kuhudhuria kesi hiyo ili kupima kiwango cha ugaidi kwa lengo la kulinda wawekezaji kutoka kwenye nchi zao , maana ni hatari kuwekeza kwenye nchi yenye Ugaidi

HS Code

1628851028661.png

2878995_images_9.jpeg
 
Kutuhumiwa na kufikishwa mahakamani yote ni michakato ya kutimiza sheria
Hao wazungu wamekuja kuona kama haki inaonekana inatendeka katika michakato hiyo,hawana uwezo wowote wa kubadili mashitaka
Wekeni nguvu katika kupangua mashitaka kisheria
 
Duh! I can see the strong ones having their eyes open and their ears on the ground monitoring the entire movie.
 
Leteni watuhumiwa mahakamani pia, wacheni woga usio na sababu. Mahakama pekee ndipo penye jibu ya hofu yenu.
Kutuhumiwa na kufikishwa mahakamani yote ni michakato ya kutimiza sheria
Hao wazungu wamekuja kuona kama haki inaonekana inatendeka katika michakato hiyo,hawana uwezo wowote wa kubadili mashitaka
Wekeni nguvu katika kupangua mashitaka kisheria
 
Halafu wanaambiwa Mbowe hajafikishwa mahakamani kwa sababu hakuna gari la kumpeleka huko, naamini kuanzia hapo hao maofisa wataona hii serikali yetu ina matatizo kichwani, haiwezekani Sabaya kila siku anapelekwa mahakamani halafu Mbowe wa kila baada ya wiki anakosa gari.
 
Hiyo kesi inakwenda kufutwa. Kitendo cha hao wadau wa maendeleo kwenda mahakamani leo ilikuwa sawa na kutuma ujumbe Serikalini kwamba hawapo na Serikali bali wapo na Mbowe.

Mwenye akili yeyote atajitafakari. Na ikitokea hii kesi ikafutwa, itakuwa aibu kubwa kwa Mkuu wa Nchi. Ingebaki kuwa aibu kwa IGP na Polisi wake, lkn yale mahojiano ya BBC yamehamishia fedheha hii upande wa juu zaidi.

Lkn ni heri nusu shari kuliko shari kamili. Kesi itafutwa, IGP ataondoka. Maisha yanaweza kuanza upya.

Uwezekano wa Warioba kuitwa kazini upo wazi.. ikishindikana, itakuja kuwezekana tukiwa tumechelewa.

Nashauri Chama changu kitumie HEKIMA YA MWALIMU NYERERE MIAKA ILE YA 90!
 
Back
Top Bottom