Kisutu: Mahakama imewatia hatiani aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa katibu wake Mwesigwa, watakiwa kulipa laki 5 au kifungo cha mwaka1

Kisutu: Mahakama imewatia hatiani aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa katibu wake Mwesigwa, watakiwa kulipa laki 5 au kifungo cha mwaka1

pantheraleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
692
Reaction score
880
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewatia hatiani aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa katibu wake, Selestine Mwesigwa na kuwaachia huru aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na karani Flora Rauya.

Malinzi ametiwa hatiani kwa kosa la kutengeneza nyaraka za uongo na mwenzake makosa mawili ya kutumia nyaraka za uongo, hivyo Mwesigwa anatakiwa alipe Mil 1.

Kila mmoja amepigwa faini ya laki tano kwa kila kosa au kwenda jela miaka miwili. Kwa sababu benki zimeshafungwa, wamerudishwa mahabusu.

1576077187211.png
Malinzi (57), Katibu Mkuu wake, Mwesigwa Celestine (46) na Mhasibu, Nsiande Mwanga (27) walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwamo ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418 (Sh840 milioni).

Malinzi anashtakiwa kwa makosa 28, huku wenzake wakishtakiwa kwa makosa yasiyozidi manne.

Walisomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga ambaye alidai kuwa katika shtaka la kwanza, Malinzi na Mwesigwa, Juni 5, 2016 wakiwa Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya, walighushi nyaraka zinazoitwa Maazimio ya Kamati ya Utendaji (Executive Committee Resolution) wakionyesha Kamati ya Utendaji ya TFF imebadili mtia saini wa akaunti ya benki ya TFF, Edgar Leonard Masoud kuwa Nsiande Isawafo Mwanga wakati wakijua si kweli.

Zaidi, soma;



======


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatano Desemba 11, 2019 imewahukumu aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na aliyekuwa Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh500,000 kila mmoja.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatano Desemba 11, 2019 imewahukumu aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na aliyekuwa Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh500,000 kila mmoja.

Washtakiwa hao wamekubali kulipa kiasi hicho cha fedha.

Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo leo Jumatano Desemba 11, 2019 baada ya kuwatia hatiani Malinzi na Mwesigwa.

Wakati Malinzi akitiwa hatiani kwa shtaka moja la kutengeneza nyaraka za uongo, Mwesigwa alitiwa hatiani kwa kutumia nyaraka hizo.

Mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wawili katika kesi hiyo ambao ni aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Frola Rauya ambaye alikuwa karani.

Katika shtaka hilo Malinzi anadaiwa kutengeneza nyaraka hizo zinazoeleza kuhusu kikao cha kamati tendaji ya TFF kwa kubadili watia saini badala ya Edagar Masoud aliwekwa Mwanga.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 213/2017 washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 20 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha ambazo ni Dola 173,335 za Marekani.
 
Hukumu gani imetolewa..... mbona unaharaka hivyo, toa taarifa kamili
Juzi bwana mkubwa kaachia wafungwa.... magereza yana nafasi ya kutosha hivi sasa...

Nadhani ushapata kapicha kiduchu...

Mleta mada ana kiherehere
 
Duh! Nimebaki kuduwaa tu haya bwana welcome back mtaani mzee Malinzi
 
Back
Top Bottom