Kisutu: Mzigo wa Madini wenye thamani ya Bil 61 Wataifishwa, ni ule Uliokamatwa Uwanja Ndege wa Dar

Kisutu: Mzigo wa Madini wenye thamani ya Bil 61 Wataifishwa, ni ule Uliokamatwa Uwanja Ndege wa Dar

Faini ya milioni 1 kwa hasara zote izo[emoji41]
Mr Kuku yeye.... Et alikusanya Bilion 17

Ila akaisababishia serikali Hasara ya Bilion 5.4

Pesa ambayo ni ileile ya jamaa alokua nayo Akauntin[emoji23][emoji23] ikapigwa yote

Akaambiwa alipe fain milion 5 imeishaaaa


Hawa ni bilion 61..ila fain 1 M...


Hahahahah wanaangalia, kinachotaifishwa kwanza, kama ni kikubwaaaaa ,faini inakua ndooooogo.
 
Watumishi 22 TRA wamesimamishwa kazi lakini hawa hasara ya 61bil wanatozwa faini 1m.

QNET hawawezi kuwarudishia watu hela zao

250gm za heroine jela miaka 20.

DPP jamani kweli hii mizani inabalance?
Huyo ndio DPP wa inji hii
 
Yaani sahivi utoki mule bila kuweka mpunga mezani kwa Dipipii, tena huyu dipipiii tangu kompyuta zake zipotee kusiko julikana amekua mkali sana.

Wachina wawai kuleta hizo pesa tunusurike aisee
Haa😂😁🤣😃😄😅😂😁😀
Unajua Mtanivuruga Hapa Sasa Hivi
 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetaifisha mzigo wa madini ya almasi ambao ulikutwa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, ukiwa unasafirishwa kwenda nchini Ubelgiji, wenye thamani ya sh. bilioni 61, 970,625,864.

Almasi hizo zina uzito wa carats wa 71,654.45 ambazo zilikuwa zinasafirishwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania(TANSORT), Archard Kakugendo na Mthamini almas wa Serikali Edward Rweyemamu.

Pia mahakama hiyo, imewahukumu wathaminishaji hao ambao ni Kalugendo na Rweyemamu , kulipa faini ya sh. milioni moja kila mmoja au kwenda jela miaka mitatu, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuisababishia Serikali hasara sh. bilioni 61.9.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya, baada ya washitakiwa kuandika barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini( DPP), Desemba 17, mwaka huu ya kuonyesha nia ya kuingia makubaliano ya kukiri kosa lao.

Awali kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, jopo la mawakili watatu wa Serikali Wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Monica Mbogo, walidai shauri lilipelekwa kwa kutajwa na upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kwa Mamlaka ya sheria ya Uhujumu uchumi, DPP ameridhika kuwashitaki washitakiwa katika mahakama hii.

Pia Wakili wa Serikali Jacqueline Nyantore, alidai kesi hii ni Uhujumu Uchumi, hivyo DPP ameipa kibali mahakama hii kesi kusikilizwa.

Akiwasomea shitaka alidai washitakiwa wote wanakabiliwa na shitaka la kuisababishia Serikali hasara ambapo alidai Agosti 25 na 31, mwaka 2017 katika maeneo mbalimbali ya mikoa wa Dar es Salaam na Shinyanga, washitakiwa hao kwa pamoja wakiwa wathamini wa Wizara ya Nisahati na madini walisababisha hasara ya dola za 29,509, 821.84, sawa na sh. bilioni 61.9
Pecuniary jurisdiction ikoje hapo?
 
Hao jamaa ukiangalia hakuna aliekamatwa na ushahidi Ila inaonekana serikali iliwafanyia uchunguzi kwenye akaunt zao za benk ikakuta zimenona balaa...ikaamua inyoke nao..
 
Faini ya milioni 1 kwa hasara zote izo[emoji41]
Haijawa hasara kwa upande wa mwenye mali kuwa mzigo ulipatikana, ila ni hasara kwa aliyekamatwa nao, inawezekana aligharimia sana kuutia mkononi.
 
Kutorosha rasilimali za nchi kwa serikali ya sasa utaishia pabaya asee.
 
Watumishi 22 TRA wamesimamishwa kazi lakini hawa hasara ya 61bil wanatozwa faini 1m.

QNET hawawezi kuwarudishia watu hela zao

250gm za heroine jela miaka 20.

DPP jamani kweli hii mizani inabalance?
Usikute hawa majamaa ndio wanatuita sisi sio wazalendo humu kwa kiwango cha juu sana. Wakipongeza kinafiki mateso ya wapinzani.
Wameramba ramba weweee.. Wamepamba juhudi mpaka, kumbe "timu tumbo kwanza."

Mali ya mjinga huliwa na wajanja.
 
Cheo DPP imekuwa zaidi ya dili
Huyu DPP atakuwa anakula rushwa! Yaani wanapiga bingo la billion 61 halafu wanatozwa faini ya milioni 1 tu? Sasa si watu wataendelea kubahatisha ili wakifanikiwa kupita wanapiga pesa ya maana na wakikamatwa wanalipa tu hiyo faini?
 
Mr Kuku yeye.... Et alikusanya Bilion 17

Ila akaisababishia serikali Hasara ya Bilion 5.4

Pesa ambayo ni ileile ya jamaa alokua nayo Akauntin[emoji23][emoji23] ikapigwa yote

Akaambiwa alipe fain milion 5 imeishaaaa


Hawa ni bilion 61..ila fain 1 M...


Hahahahah wanaangalia, kinachotaifishwa kwanza, kama ni kikubwaaaaa ,faini inakua ndooooogo.
Just imagine
 
Back
Top Bottom