KISUTU: Wema Sepetu na Wafanyakazi wake wakutwa na kesi ya kujibu! Kuanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018

KISUTU: Wema Sepetu na Wafanyakazi wake wakutwa na kesi ya kujibu! Kuanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018

huyu anamfuata tuu Lulu siku kabla ya maandamano ili ie kiki ya serikali kuharibu mitandao
 
alivyo hamia ccm ndo alijua kesi imekwisha, kumbe ndo kwaanza
 
WEMA ANA KESI YA KUJIBU: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema msanii Wema Sepetu na wafanyakazi wake wanaokabiliwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya wana kesi ya kujibu, hivyo wataanza kujitetea Mei 14 na 15, mwaka huu.

Uamuzi huo, umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa serikali, Constantine Kakula kueleza kuwa kesi hiyo imehitishwa kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama lah.

Katika uamuzi wake Hakimu Simba amesema kwa mujibu wa sheria kama washtakiwa wakipatikana na kesi ya kujibu watatakiwa kujitetea, pia kama hawana kesi ya kujibu wataachiwa huru.

Hakimu Simba amesema baada ya kupitia hoja zote, mahakama imejitosheleza kwamba washtakiwa wote wana kesi ya kujibu katika mashtaka yote, hivyo wana haki kisheria kuanza kujitetea.
 
Juzi walisema kile kipisi ni cha sigara sio mbangi leo tena mapya au sijui kinachoendelea
 
wema_sepetu.jpg

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemkuta na hatia msanii Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili, kwa kosa la matumizi ya madawa ya kulevya.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Simba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano wa upande wa mashtaka waliokuwa wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, na kusema kwamba Wema na wenzake wataanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018.

Kabla ya uamuzi huo kutolewa Wakili Kakula aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa hao wana kesi ya kujibu ama la, na ndipo Hakimu Simba akasema kwa mujibu wa sheria iwapo washtakiwa watapatikana kuwa wana kesi ya kujibu wataanza kujitetea, na ndipo aliposema baada ya kupitia hoja zote zilizowasilishwa mahakamani hapo, imejitosheleza kwamba washtakiwa wote wana kesi ya kujibu katika mashtaka yote, hivyo wana haki ya kisheria kuanza kujitetea.

Wema na wafanyakazi wake wawili wanakabiliwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya aina ya bhangi, na kesi hiyo imehairishwa mpaka Mei 14 mwaka huu.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemkuta na hatia msanii Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili, kwa kosa la matumizi ya madawa ya kulevya.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Simba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano wa upande wa mashtaka waliokuwa wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, na kusema kwamba Wema na wenzake wataanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018.

Kabla ya uamuzi huo kutolewa Wakili Kakula aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa hao wana kesi ya kujibu ama la, na ndipo Hakimu Simba akasema kwa mujibu wa sheria iwapo washtakiwa watapatikana kuwa wana kesi ya kujibu wataanza kujitetea, na ndipo aliposema baada ya kupitia hoja zote zilizowasilishwa mahakamani hapo, imejitosheleza kwamba washtakiwa wote wana kesi ya kujibu katika mashtaka yote, hivyo wana haki ya kisheria kuanza kujitetea.

Wema na wafanyakazi wake wawili wanakabiliwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya aina ya bhangi, na kesi hiyo imehairishwa mpaka Mei 14 mwaka huu.View attachment 754481
bora likakae jela hata miez3 akili imrudie
 
Swali nje ya mada kwa nn wema sepetu hapendi kujumuika na wenzie kwenye shughuli mbalimbali isipokua za wcb tu??? Wema kama upo humu tunaomba ufafanuzi au wapambe wake tunaomba majibu tafadhali
 
Mleta mada usitulishe matango pori. Kilichotokea Leo ni kwamba Mahakama imeamua Mshtakiwa Wema na wenzake wana kesi ya kujibu, na ndo maana wanatakiwa kuanza kujitetea na siyo kwamba wamekutwa na hatia.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemkuta na hatia msanii Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili, kwa kosa la matumizi ya madawa ya kulevya.

e wawili wanakabiliwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya aina ya bhangi, na kesi hiyo imehairishwa mpaka Mei 14 mwaka huu.View attachment 754481
sasa mbn unasema amekutwa na hatia????
 
Back
Top Bottom