SoC01 Kiswahili Afrika na jinsi ya kukifanza kukua kiurahisi na kiulaini hali tunaongeza ajira kwa Vijana

SoC01 Kiswahili Afrika na jinsi ya kukifanza kukua kiurahisi na kiulaini hali tunaongeza ajira kwa Vijana

Stories of Change - 2021 Competition

Muharam12

New Member
Joined
Sep 1, 2021
Posts
2
Reaction score
3
TUSIJIDANGANYE kutaka Kiswahili kuenea fumba na kufumbua duniani. Tutosheke na kukiona Kiswahili kinatawala Afrika hatua kwa hatua.

KOKOTE Afrika viongozi, wanasiasa, wasomi na jamii kwa ujumla watu wanazungumzia juu ya fursa za ajira na 'baibai kwa umasikini' kwa vijana. Ila hakuna anayezichanganua kwa undani fursa na changamoto kwenye hili.

Wanaoshawishi hawajawahi kupita kwenye njia husika, na wanaoshawishiwa hawajajiona, wanaisikia tu. Je, jambo lisipokuwa ndoto kamili, linaweza kuteguliwa?

Tufanye nini ili yale yaliyo bado ruia yaweze kuonekana kwenye akili za vijana na kizazi kijacho cha wajasiriamali ? Tujiulize, ili nchi yetu izishinde nchi nyingine Afrika hivi sio lazima vijana wetu kwanza wawashinde vijana wengine kiakili, kimaarifa na kimaono ?

Katika andiko hili, mimi sintojaribu kujibu maswali hayo. Kinyume chake nitaongeza maswali zaidi. Ili kutokana na wingi wa maswali yatakayoulizwa, tuweze kuona angalau tundu la mwanga kwa aina ya majibu yatakiwayo.

Swali la kwanza, je, kwa kuwaaambia vijna kuwa kuna fursa katika teknolojia na tehama au michezo au muziki au biashara au kiimo cha kisasa bila kuwekeza kwenye mifumo na miundo mbinu ya kiuchumi inayorahisisha kuwezekana kwa ndoto za vijana, walengwa wataweza wao wenyewe bila kusaidiwa kujaribu na kufanikisha mawazo na ndoto zao za leo na ksesho ?

Sera za Mawasiliano, Teknolojia, Tehama na kadhalika zinachangia kiasi cha kutosha kufafanua fursa na changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi ? Maana, kuna wanaoona kwamba baada ya mapinduzi ya teknolojia ya 2000 kutumia sera za kabla ya hapo ni sawa na kutumia Katiba za nchi za miaka ya kudai uhuru wa bendera katika miaka ya kudai uhuru wa kiuchumi na kiteknolojia ?

Kama kweli tumeamua Kiswahili kiwe lugha namba moja Afrika, lazima serikali na watu w Tanzania waamue kukilima na kukipanda katik bara hili kwa kutumia maarifa, akili na rasilimali zetu zote. Maana inaipa.

Kama tunataka maendeleo ya kweli, budi tuwekeze fedha, muda na rasilimali tulizonazo kwenye yale yatakayochangia kutuingizia mapato na rasilimali zaidi kesho na kesho kutwa.

Kukilima na kukipanda Kiswahili ni pamoja na kuandaa mazingira ya kuchagua maeneo au ardhi yenye mvua za kutosha, rutuba na samadi ili kukifanikisha kilimo husika. Maana, mbegu zipo tayari.

Vijana wa Tanzana wamekuwa wakipigania uwepo wa Baraza la Vijana la Taifa lenye kuunganisha vijana wote bila kujali chama au sehemu wanayotokea. Lakini, kwa sababu wanazozijua wazazi wao, hadi sasa, juhudi zao zimekwama.

Swali la kujiuliza ni: ' JE, JITIHADA ZA KUUPIGA VITA WAZIWAZI AU KWA SIRI KUANDIKWA KATIBA MPYA; DEMOKRASIA NA UHURU WA KILA MTU ZITAONGEZA MAADUI AU MARAFIKI KUTOKA KWENYE MAKUNDI YA VIJANA YASIYO NA LENGO MOJA SEMBUSE UMOJA NA USHIRIKIANO ?

Binaafsi ninaamini Tanzania inaweza kuwa na Baraza Moja la Vijana Kitaifa. Baraza hilo likatumika kuwasomesha wazee ni wapi vijana wanakotaka kwenda na sio kuburuzwa na watu wasiowatakia mema. Wakiunganishwa na fursa na changamoto za kukua na kuenea Kiswahili Afrika na duniani wakajiendeleza wao wenyewe, watu wao na nchi yao fasta, fasta zaidi.......

Mathalani kupitia katika:

. Elimu na mafunzo ya teknolojia na tehama kwa Kiswahili kupitia balozi zetu nje na ofisi za wakuu wa mikoa na wilaya nchini kote;

. Uzalishaji muziki kwa Kiswahili kinachosomesha bila maumivu. Muziki utakaojiuza ndani na nje ya mipaka yetu;

. Utengenezaji sinema kwa Kiswhili zitakazojiuza pia nje ya mipaka yetu;

. Kuanzisha Gazeti la Picha AFRIKA TANZANA- kwa picha na KIswahili na uwepo mtandaoni kufundisha Kiswahili kwa taswira na kdahalika;

. Utengenezaji komiki (Vitabu vya michoro na hadithi kwa Kiswahili na lugha za KIafrika) kuuzwa kote Afrika kwa lengo la kufundisha KIswahili kwa michoro na vitendo;

. Kupanua uzalishaji sinema za katuni Kwa Kiswahili na lugha za Kiafrika ili kukisambaza na kukieneza Kiswahili;

. Kuwa na televisheni moja au mbili toka Tanzania zinazotumia Kiswahili na zinazofikia takriban nchi zote Afrika. Zikiwa na maudhuui zaidi za michezo, muziki, uchumi na biashara na fedha;

. Matumizi ya sosho midia kama vibarua wa vyombo vya habari nyumbani na kimataifa;

. Kukuza matumizi ya bidhaa zitakiwazo Afrika zenye lebo na maelezo kwa Kiswahili ili kujiuza kibiashara na kukiuza Kiswahili Afrika;

. Kuwa bora katika michezo aina zote, midogo kwa mikubwa, tukianzia na soka kwa wanawake na vijana, halafu riadha na michezo mingine inayolipa haraka zaidi;

. Balozi zetu kuwapromoti Machinga na kuwa na Africn Machinga entrepreneurs kote kunakowezekana Afrika. Wanahistoria wanaaaminii wafanyabiashara hueneza lugha haraka zaidi kuiko makundi mengine katika jamiii husika;

Mkakati huu wa kujenga Kiswahili ukitumika kwa hekima na busara sio tu utakijenga Kiswahili haraka Afrika, bali utachangia ajira kwa maelfu wanaojua lugha ya Kiswahili.

Muhimu hapa ni kuanzisha upya tena magari ya sinema zitembeazo pamoja na mabasi ambayo ni maabara na madarasa ya tehama yanayozunguka maeneo yasiyofikika kiurahisi. Nayo yakachangia pia kueneza na kusambaza Kiswahili.

. Kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu kote Afrika. Je, tumejenga barabara ngapi na madaraja mangapi hadi sasa. Ongezea laini za reli, bandari na vyombo vya majini. Elimu na ujuzi wote huu uko kwenye Kiswahili. Haitakuwa ajabu tukishindwa kuuomba kandarasi za ujenzi wa vitu kama hivi Kongo, Zambia, Malawi, Angola, Afrika ya Kati na kadhalika ?

. Kitu kidogo tu kama Khanga Kikitengenezwa kwa maneno ya Kiswahili na lugha za Kiafrika kinaweza kuzaa ajira ya vijana kwa maelfu; Kazi ni kufufua tu viwanda tulivyowekeza chini ya miaka hamsini iliyopita;

. Kama serikali na washirika wake watawekeza kwenye michezo ya kompyuta na simu za mikononi kwa Kiswahili, sio tu tutakuwa na vyanzo vingine vya kipato bali pia kutachangia kueneza na kusambaza Kiswahili kwa haraka zaidi;

. Je, hatuwezi kuwa na taasisi ya kuzalisha michezo ya kuigiza kutoka lugha mbalimbali kwa Kiswahili na kuionyesha kwenye majumba ya maonyesho ndani na nje ya nchi, mradi inakidhi viwango vinavyokubalika kimataifa;

. Hivi tukiwa na gari letu wenyewe la la saloon linaloitwa motokaa au la mizigo linaloitwa Lori au la abiria linaloitwa BASI haya yatasaidia kwa kiasi gani kukieneza na kukisambaza kISWAHILI ? Hilo hapo juu linahusu pia Pikipiki aina ya Bodaboda; Bajaji aina ya BAAJAJII

Tukiwa wa kwanza kutengeneza, kutumia, na kuidhinisha matumizi ya Programu za kuendesha Serikali kuu, serikali za mitaa na taasisi zake Kwa Kiswahili nini kitatokea kwingine KIswahili kinapokubalika

Mashindano mbalimbali katika lugh ya Kiswahili kwenye magazeti, majarida, redio, televisheni na mitandaoni nayo yatachangia kwa kiasi gani kukua na kuendelea kwa lugha ya KIswahili na kuwakomboa vijana kiuchumi.

Pamoja na haya ipo haja ya kuwa na

1. Zawadi ya Afrika Katika Ukuzaji na Uendelezaji Lugha ya Kiswahili;

2. Zawadi ya Tanzania katika Kufundisha na Kueneza Kiswahili;

3. Zawadi ya Magufuli kimataifa katika matumzi na kukieneza Kiswahili SADC i....

Haya yote ni mambo ambayo sio tu yatachangia kukua na kuenea Kiswahili Afrika kirahisi na kiulaini, bali pia kuwapatia vijana wetu ajira sehemu mbalimbali duniani.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom