Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Salaam,
Neno "Mjinga" ni tukano, ila sio tusi!. Mtu kuwa mjinga ni ile hali ya kutokujua. Hivyo mtu akikuita mjinga, anamaanisha wewe hujui kitu fulani anachokuitia mjinga. Ukiwa hujui kitu fulani na ukaitwa mjinga, hujatukanwa bali umeambiwa ukweli kuhusu hali ya kutokujua kwako. Ila ikitokea unakijua kitu fulani halafu ukaitwa mjinga, hapo ndipo utakuwa umetukanwa.
Kwa vile mjinga ni unatokana na ujinga, hali ya kutokujua, mjinga akielimishwa, anakuwa ameufuta ujinga, na kufuatia sio Watanzania wote walioelimika na kuufuta ujinga, mara baada ya Tanzania kupata uhuru wetu kutoka kwa wakoloni Waingereza, tulitangaza vita na maadui wetu wakuu watatu walikuwa ni ujinga, umasikini na maradhi.
Hadi leo tunaelekea miaka 60 ya uhuru wetu, tungali, tunaendelea kupigana vita hii, hivyo mtandao wetu huu wa jf ni silaha muhimu sana katika uelimishaji watu, umma, katika masuala mbalimbali, hivyo kuufuta ujinga.
Hivyo leo, naomba kuchukua fursa hii, kuendeleza matumizi ya jukwaa letu hili la JF, kusaidia kuelimisha wengine kwa kuwafuta ujinga kwa kuwapa elimu kwa jambo wasililijua.
Kiukweli baadhi ya Watanzania ni wajinga mpaka basi!. Ni walalamishi wa ajabu kwa vitu vidogo vidogo vya kijinga jinga hadi wanakera!. Baada ya rais Magufuli kushinda urais wa Tanzania katika uchaguzi huru, wa haki na wa kidemokrasia, na serikali ikaamua kujenga uwanja wa ndege Chato, kuna watu humu walipinga sana ujenzi wa uwanja huo kwa sababu za kijinga tuu!. Kwa vile sisi waandishi wa habari ni waelimishaji human, mimi ni miongoni mwa wachache tuliojitokeza kuunga mkono ujenzi wa uwanja huo wa Chato, na kujitolea kuelimisha umma umuhimu wa uwanja huo, hivyo kuwasaidia kuwatoa ujinga Watanzania wenzetu kwa kuwaelimisha umuhimu wa uwanja huo.
Naunga Mkono Uwanja wa Ndege wa Chato, Una Justification, Utakuwa kama Ggabolite, au Yamoussoukro, Watalii Watamiminika! - JamiiForums
Sasa rais Magufuli yuko Chato, watu humu wanaanza tena ujinga mwingine wa kupiga kelele za kijinga jinga, eti kwanini rais Magufuli yuko Chato kwa muda mrefu?!.
Tuambizane ukweli, Chato si ndio kwao rais Magufuli?. Kuna ubaya gani kama rais Magufuli atakuwa kwao kwa muda mrefu kadri atakavyo as long as anaendelea kutimiza majukumu yake mbalimbali kikamilifu?.
Japo Kiswahili ndio lugha yetu ya taifa, lakini kiukweli Kiswahili ni kigumu hata kwa baadhi ya Waswahili wenyewe, hivyo kwa vile ni mmoja wa Watanzania tuliobahatika kuzaliwa mjini, kukulia mjini, kusomea mjini na sasa tunaishi mjini, wakati wengi wetu wamezaliwa vijijini, lugha yao kuu ya kwanza ni kilugha chao, kisha ndipo kije Kiswahili, lakini kwa sisi tulio zaliwa mjini, yaani "born town", Kiswahili ndio lugha yetu kuu ya kwanza, tunakimanya vilivyo, hivyo kunapotokea wajinga wajinga wasiojua vizuri lugha ya Kiswahili, hakuna ubaya, kujitolea kuwandeshea darasa la kuwafunza, ndicho ninachokifanya kwenye bandiko hili.
Wengi wasiojua Kiswahili barabara, wanadhani Ikulu ni eneo rasmi specific la makazi ya rais kuishi na kufanyia shughuli zake kama ilivyo Ikulu ya Magogoni au Ikulu ya Chamwino, kumaanisha rais asipokuwa Ikulu ya Magogoni au Ikulu ya Chamwino, akiwa pengine popote, anakuwa hayuko kazini, hivyo huku kwenye mitandao ya kijamii sasa kuna kelele za watu wajinga kutaka kulazimisha lazima wamuone rais Magufuli na kumsikia akitokea ama Ikulu ya Magogoni, au Ikulu ya Chamwino!. Hawa ni wajinga na huu ni ujinga!.
Ikulu sio eneo lolote specific, bali eneo lolote la makazi rasmi ya rais ambapo anaweza kutimiza majukumu yake ya urais, eneo hilo hugeuka Ikulu. Hivyo kwa Tanzania tuna ikulu ya Magogoni, Ikulu ya Chamwino, Ikulu ndogo ya Lushoto na karibu kila mkoa kuna Ikulu ndogo kama ya Arusha, Tanga, Morogoro, Moshi, Iringa, etc, na mikao ambayo haina Ikulu ndogo, then kuna state lodge.
Enzi za Nyerere aliamua yeye hakai Ikulu bali aliishi Msasani, kama angeamua kufanyia kazi zozote za urais pale Msasani, then Msasani napo pangekuwa ni ikulu ndogo ya Msasani. Mwalimu Nyerere alikuwa anakwenda likizo Butiama, wakati Mwalimu Nyerere akiwa Butiama, angeamua kufanya majukumu yoyote ya kirais, wakati akiwa Butiama kama kuteua, kuapisha, etc, then hapo Butiama panakuwa ni Ikulu ya Butiama.
Kwa muda sasa rais Magufuli yuko kijijini kwake Chato, kwa vile wakati rais Magufuli yuko huko Chato kwa mapumziko matupu, lakini wakati huo huo, anaendelea kutimiza majukumu yake yote ya urais, then hapo Chato ni ikulu ya Chato, as long as mambo yote yanakwenda, hizi kelele za watu wajinga kutaka kumuona rais Magufuli akiwa ikulu ya Magogoni au ikulu ya Chamwino za nini?!. Ni kelele za ujinga tuu!. Watanzania wenzangu tusiwe wajinga!.
Hii ni press release ya leo
Hitimisho.
Kufuatia rais wetu, akiwa mahala popote bado anaweza kutimiza majukumu yake ya ki rais, ukiondoa wajinga wachache wapiga kelele, Watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, watapenda kumuona rais wao akitimiza majukumu yake ya urais akiwa mahala popote na tungependa rais wetu awe free kukaa mahali popote anapopenda as long as it takes.
Kuna hawa watu wenye akili fupi wanaodhani uwepo wa rais Magufuli Chato ni kuikimbia ugonjwa wa Corona, it's not!.
Japo Corona ni ugonjwa wa kweli na ni ugonjwa wa hatari na unaua watu kwa kasi!, kwa baadhi yetu, wenye imani kali, tunaihesabu ugonjwa wa Corona kama ka Kolona tuu, ni kaugonjwa kadogo tuu ambacho hakatishi kivile, hivyo tusitishane!. Na ikitokea ka Kolona kamekuja, kametukuta watu tuko mapumzikoni kwenye vacations zetu, hatuwezi kukatisha vacations zetu kwasababu ya ka kolona na wala hatuwezi kukambia ka Kolona kwasababu kwetu ka Kolona sii lolote, sii chochote, hatukaogopi na hakawezi kutufanya lolote wala chochote, tuendelee tuu kuchapa kazi of course huku tukizingatia tahadhari!.
Watanzania tupunguzeni ujinga kulalamika hivyo kwa kulalamikia vitu vingine vidogo vidogo vya kijinga jinga tuu!. Tuache ujinga!. Chato ni kijijini kwa rais Magufuli na ni nyumbani kwa rais Magufuli, akiwa likizo au mapumzikoni 'jijini' Chato rais Magufuli anakuwa amepumzika kwake kama Mwalimu Nyerere alivyokuwa ana pumzika Butiama, Mwinyi anapumzika pale kwake Mikocheni, Mkapa pale Masaki, kule Lushoto na Masasi, na Kikwete pale Regent na Msoga na sasa Magufuli Chato!.
Lakini rais akifanya majukumu yake yoyote ya kiraisi akiwa eneo fulani, ikiwemo kuteua, kuapisha, kulihutubia taifa, kukutana na wakuu wa ulinzi na usalama au kuendesha cabinet, then eneo hilo linageuka ni Ikulu!. Hivyo japo Chato ni kijijini kwa rais, lakini wakati akiwa Chato akafanya jukumu lolote la ki rais eneo hilo inabadilika na kugeuka ni Ikulu. Hii ni Ikulu ya Chato!.
Paskali
Rejea
Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike - JamiiForums
Tusilalamike tuu, kulaumu na kulaani kila kitu, kwenye mazuri tupongeze! Rais Magufuli is changing for the better!. - JamiiForums
Tusikalie kumlaumu tu Rais Magufuli na Serikali yake wanapofanya mabaya, kwenye mazuri, pia tupongeze!. - JamiiForums
Paschal Mayalla: Acheni kulalamika, kubalini mafanikio ya Serikali - JamiiForums