Kiswahili cha Kisiasa Kwa Watanzania: Ikulu sio Eneo Specific, ni Makazi ya Rais, Tuna Ikulu ya Magogoni, Chamwino, Sasa Hadi Ikulu ya Chato!

Katiba inasemaje rais anapoenda likizo isiyoisha, je gharama za kuendesha nchi akiwa chato umezizingatia?;
 
Timiza majukumu popote,lakini ikulu inaendelea kubaki ni eneo specific.

Rais anapokuwa ziarani kila anaposimama inamaana panageuka kuwa ikulu?

Hahaha kumbe kwetu kilanjelanje napo palishakuwa ikulu.


Kuna watu leo wanafanyia kazi nyumbani, utasema nipo TBL hapa ilala,huku unajua umejifungia chumbani kwako?

Yeye achape kazi popote pale,hata asiporudi ikulu hadi amalize muda wake. Sisi wananchi tunataka kazi ziende.

Ila tunajua hayupo ikulu,anafanyia kazi sehemu nyingine.

Kuna RC mmoja nae eti vikao vinafanyikia nyumban kwake. Asubirie apate anachokitaka.

Sent using iphone pro max
 
Pia msoga na butiama
 
Pia msoga na butiama
Msoga na Butiama ni makazi tuu ya rais, hazikuwahi kuwa Ikulu, kwasababu marais wale walikuwa wanakwenda kupumzika na wana pumzika kweli.

Chato ni Ikulu ya Chato kwasababu sasa sio kupumzika bali ni eneo la kazi, hivyo panageuka kutoka makazi binafsi na kugeuka ofisi with staff and amenities.
P
 
Samwel Sitta Mungu akutehemu maana uliona mbali. Ofisi ya Spika Urambo ilijengwa sehemu sahihi maana Spika wa Bunge ni wa Tanzania nzima hivyo anaweza kuwa na ofisi popote. Baada ya uchaguzi wa mwaka huu tunatarajia Rais ateue wakuu wa mikoa wanaotoka mikoa wanayoongoza iwe rahisi kuongoza kutokea nyumbani. Mfano, Mwakasege akiteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa MBEYA atakuwa na ofisi Mbeya mjini kama makao makuu ya mkoa, Tukuyu mjini, na Mwakaleli ambako ni nyumbani kwake. Kwa hiyo kazi zitafanyika muda wote hata akiwa nyumbani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi za Nyerere aliamua yeye hakai Ikulu bali aliishi Msasani, kama angeamua kufanyia kazi zozote za urais hapo Msasani, then pangekuwa ni ikulu ya Msasani. Mwalimu Nyerere alikuwa anakwenda likizo Butiama, wakati akiwa Butiama, akiamua kufanya majukumu yoyote ya kirais, then hapo Butiama panakuwa ni Ikulu ya Butiama.

Hapo umedanya watu kumbe na wewe Pascal ni mburura tu kama mamburura wengine

Ikulu ni Ofisi ya raisi na ipo kikatiba ndani ya hiyo ikulu kama kuna nyumba raisi akiamua kuishi hapo sio kosa

Msasani yalikuwa ni makazi ya Mwl Nyerere na ndio maana alikuwa asubuhi anaenda ofisini ambako ni ikulu magogoni na jioni anarudi nyumbani kwake msasani kupumzika na familia yake

Naona humu watu wengi wanasema huwa unamtetea sana raisi ili upate uongozi kama kweli utapata uongozo utakuwa sio kiongozi nzuri maana wewe ni NDUMELAKUILI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thanks Dkt.P# CHATTLE PALACE# Stay Home
 
Duh! Kwa hiyo Rais ajae naye atakuwa na uwezo wa kufanyia kazi Chato? Au huyu akistaafu na hiyo Ikulu itaishia hapo hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uteuzi ukija jina la mayala likakosa nitajua kweli jina linamaanisha ile.maana nyingine
 
Ahsante kwa taarifa ilyojaa ujanja ujanja... Hivi Msoga napo tulikua na ikulu?



Cc: mahondaw
 
Ugawaji wa Tausi huu Ugawaji wa Tausi, kabla ya Raisi Hajagawa tausi kwa wastaafu, kuna hotel inaitwa JS imeshapatiwa hao Tausi kitambo,

Ni mmiliki nani na nani hasa aliruhusu wato Ikulu?

Britannica
Mkuu Britanicca, acha uchokozi na uchochezi, tausi ni ndege tuu kama ndege wengine wote na wanapatikana mahali pengi.

Kwa bandiko hili, ikiamuliwa kufunguliwa kesi ya uchochezi, jee utaweza kuthibitisha kuwa hao tausi wa JS Hotel pale Chato ni tausi kutoka Ikulu yetu?, unamaanisha kuna mwizi kaingia Ikulu yetu, akawaiba wale tausi wa Nyerere pale Ikulu ambao ni nyara za taifa, akawapeleka huko JS hotel?.
Au anamaanisha miongoni mwa watu wenye access na Ikulu yetu, kuna mtu ni mwizi kaiba tausi wetu ambao ni nyara za serikali, na kuwauza kwa JS hotel ya Chato?.

This is criminal liability, hivyo kama kuna tausi wa nyara za serikali pale JS Hotel, Chato, na police wetu wanasoma JF, waanzishe uchunguzi hapo JS kuchunguza yafuatayo
  1. Jee ni kweli JS hotel ya Chato kuna tausi?.
  2. Waliwapata wapi hao tausi?
  3. Wana vibali vya kumiliki nyara za serikali?
  4. Kama ni tausi kutoka Ikulu yetu, nani aliruhusu nyara hizo za serikali kuchukuliwa na kupelekwa hotel binafsi?.
  5. Kama ni kweli tausi hao wa JS hotel ni kutoka Ikulu yetu, then huu nao ni ufisadi tuu kama ufisadi mwingine wowote!.
NB. Angalizo: Kufuatia JS hotel kuwa karibu na Ikulu ya Chato, usikute tausi ambao Mkuu Britanicca amewaona ni tausi wa Ikulu ya Chato wakiranda randa mitaani kama wale Tausi wa Ikulu ya Magogoni wanavyo randa randa maeneo mengi, and this being the case, hakuna kesi wala hakuna issue!
P
 
Leo hii inaweza kuwa ndio the final and the last use of Ikulu ya Chato.

Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Mkuu jaap, your concern ni very genuine, na hii ni plus plus kwa Rais Samia as An African Woman, Tanzanian Woman na a Zanzibari lady, wanawake huwa hawajengi kwao, angekuwa ni mwingine, baada tuu ya yeye kuwa Rais wa JMT, tungeshuhudia ujenzi wa Ikulu ya Kizimkazi fasta!.

Kwa vile mimi ni miongoni wa waelimishaji umma humu, kwa kuwafunza kuhusu Ikulu ya Chato Kiswahili cha Kisiasa Kwa Watanzania: Ikulu sio Eneo Specific, ni Makazi ya Rais, Tuna Ikulu ya Magogoni, Chamwino, Sasa Hadi Ikulu ya Chato! na ili kurahisisha usafiri wa Chato, mimi Naunga mkono Uwanja wa Ndege wa Chato. Una justification, utakuwa kama Ggabolite au Yamoussoukro. Watalii watamiminika!, sasa maadam kijiji alichozaliwa rais wetu ni Kizimkazi, jee kuna ubaya wowote tuanze maandalizi ya uhamasishaji wa ujenzi wa Ikulu ndogo ya Kizimkazi?. Sio lazima ijengwe kwa fedha za serikali, bali hatua ya kwanza ni tubadili baadhi ya mila na desturi za kibaguzi za asili za mtoto wa kike akiolewa, atajenga kwa mumewe kule alikoolewa!. Sasa binti huyu wa Kizimkazi ndiye rais wa JMT, apewe nafasi Watanzania tumjengee ili eneo hilo liwe ni eneo muhimu la kihistoria kijiji alipozaliwa rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania. Rais wetu awe huru kwenda likizo ndefu Kizimkazi kama zile likizo za Chato.
Mnalionaje hili?.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…