mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
"kwa sisi ambao ka Kolona ni kaugonjwa kadogo ambacho hakatishi na tusitishane, hatuwezi kukuambia ka Kolona!"Wanabodi,
Kiukweli baadhi ya Watanzania ni walalamishi mpaka basi, baada ya rais Magufuli kushinda urais wa Tanzania katika uchaguzi huru, wa haki na wa kidemokrasia, na serikali ikaamua kujenga uwanja wa ndege Chato, kuna watu humu walipinga sana ujenzi wa uwanja huo, mimi ni miongoni mwa wachache tuliounga mkono ujenzi wa uwanja huo
Naunga Mkono Uwanja wa Ndege wa Chato, Una Justification, Utakuwa kama Ggabolite, au Yamoussoukro, Watalii Watamiminika! - JamiiForums
Sasa rais Magufuli yuko Chato, watu humu wanaanza tena kupiga kelele, kwanini rais yuko Chato muda mrefu?.
Japo Kiswahili ndio lugha yetu ya taifa, lakini kiukweli Kiswahili ni kigumu hata kwa baadhi ya Waswahili wenyewe, hivyo kwa vile ni mmoja wa Watanzania tuliobahatika kuzaliwa mjini, kukulia mjini, kusomea mjini na sasa tunaishi mjini, Kiswahili ndio lugha yetu kuu, tunakimanya vilivyo.
Wengi wasiojua Kiswahili barabara, wanadhani Ikulu ni eneo rasmi specific la makazi ya rais kuishi na kufanyia shughuli zake kama ilivyo Ikulu ya Magogoni au Ikulu ya Chamwino, kumaanisha rais asipokuwa Ikulu ya Magogoni au Chamwino, akiwa pengine popote, anakuwa hayuko kazini, hivyo huku kwenye mitandao ya kijamii sasa kuna kelele za watu kutaka kulazimisha lazima wamuone rais Magufuli na kumsikia akitokea ama Ikulu ya Magogoni, au Ikulu ya Chamwino.
Ikulu sio eneo lolote specific, bali eneo lolote la makazi rasmi ya rais ambapo anaweza kutimiza majukumu yake ya urais, hivyo kwa Tanzania tuna ikulu ya Magogoni, Ikulu ya Chamwino, Ikulu ndogo ya Lushoto na karibu kila mkoa kuna Ikulu ndogo kama ya Arusha, Tanga, Morogoro, Mishi, Iringa, etc.
Enzi za Nyerere aliamua yeye hakai Ikulu bali aliishi Msasani, kama angeamua kufanyia kazi zozote za urais hapo Msasani, then pangekuwa ni ikulu ya Msasani. Mwalimu Nyerere alikuwa anakwenda likizo Butiama, wakati akiwa Butiama, akiamua kufanya majukumu yoyote ya kirais, then hapo Butiama panakuwa ni Ikulu ya Butiama.
Kwa muda sasa rais Magufuli yuko kijijini kwake Chato, kwa vile huko Chato anatimiza majukumu yake yote ya urais, then hapo Chato ni ikulu ya Chato, as long as mambo yote yanakwenda, hizi kelele za watu kutaka kumuona rais Magufuli akiwa ikulu ya Magogoni au ikulu ya Chamwino za nini?.
Hii ni press release ya leo
View attachment 1426440
Hitimisho.
Watanzania wazalendo watapenda kumuona rais wao akitimiza majukumu yake ya urais akiwa popote na tungependa rais wetu awe free kukaa mahali popote anapopenda as long as it takes.
Kuna watu wenye akili fupi wanadhani uwepo wa rais Magufuli Chato ni kuikimbia Corona, it's not!, kwa sisi ambao ka Kolona ni kaugonjwa kadogo ambacho hakatishi na tusitishane, hatuwezi kukuambia ka Kolona!.
Tupunguzeni kulalamika!
Paskali
Rejea
Hongera Rais Magufuli kuipendezesha Ikulu yetu kuliko enzi za Nyerere, Ikulu iwe kivutio cha utalii, restrictions ziondolewe watalii wafurike - JamiiForums
Tusilalamike tuu, kulaumu na kulaani kila kitu, kwenye mazuri tupongeze! Rais Magufuli is changing for the better!. - JamiiForums
Tusikalie kumlaumu tu Rais Magufuli na Serikali yake wanapofanya mabaya, kwenye mazuri, pia tupongeze!. - JamiiForums
Paschal Mayalla: Acheni kulalamika, kubalini mafanikio ya Serikali - JamiiForums
Mkuu Paskali, kwa mtu ambaye hukurupuka tu kusoma maandishi yako bila ya kutuliza akili yake, hataweza kamwe kukuelewa na kuishia kukulaumu.
Sent using Jamii Forums mobile app