Kiswahili fasaha kinatoweka

Kiswahili fasaha kinatoweka

Dah! Kutoka mbeba maboksi mpaka wakili msomi! Umenipendelea sana. Usomi huo mi mbeba maboksi niutoe wapi? [emoji3]

Hata hivyo, ahadi ni deni. Nimechoka kama mbwa, lakini naamini katika kutimiza ahadi.

Haya, twende kazi;

Kama nilivyosema hapo awali, maneno yote mawili, ‘onesha’ na ‘onyesha’, ni sahihi.

Neno sahihi katika kuelezea utumikaji wa hayo maneno ni ‘kibadala’ au ‘vibadala’. Kwa kimombo nadhani ni ‘alternate’.

Kama picha ya sehemu ya ukurasa inavyoonyesha hapo chini, kibadala ni moja kati ya maneno mawili au zaidi yanayotofautiana kidogo kwenye maandishi au matamashi, lakini yanakuwa na maana sawa; onyesha/ onesha. Na unakumbuka niliongelea mambo ya lahaja? Hata wao watu wa TATAKI wamelizungumzia hilo [2009 walibadili jina kutoka TUKI]. TATAKI ni Taasisi ya Taaluma za Kiswahili.

View attachment 2967852

Uzuri wa hizi kamusi za siku hizi, huwa zina maelezo mazuri sana kuhusu masuala ya lugha.

Kwa mfano, moja ya hizi kamusi nilizonazo ina orodha kabisa ya vibadala vya maneno na mojawapo ya hayo maneno ni ‘onyesha’ na ‘onesha’.

View attachment 2967856

Huu hapa ukurasa yaliyopo hayo maneno.

View attachment 2967857

Hapa chini ni kipande cha ukurasa wa kamusi ya Kiswahili sanifu tu. Yaani Kiswahili peke yake.

Angalia hayo maneno ‘onesho’ na ‘onesha’ utaona yakifuatiwa na neno ‘pia’ “onyesho “ na “onyesha”.

View attachment 2967860

Hiyo’pia’ maana yake ni kwamba hicho kibadala cha hilo neno, nacho ni sahihi pia!

Tukienda kwenye kamusi ya Kiingereza.- Kiswahili, neno ‘show’ wao wamelitafsiri kama ‘onyesho’.

View attachment 2967870

Hii hapa orodha ya watu waliohusika kuzitengeneza hizi kamusi. Wachache kati yao nafahamiana nao. Ni watu wanaoaminika kwa uwezo wao kwenye fani yao.

View attachment 2967871

Haya bana, baadaye. Nimechoka kama mbwa koko leo.

[emoji3577]
asante kiongozi kwa hizi spana matata
 
Yaani ni ghafla sana watu hawajui kuandika wala kusema Kiswahili sahihi siku hizi. Matumizi ya uyu/uyo (badala ya huyu/huyo) , aya ( badala ya haya), zarau (badala ya dharau), zalilisha (badala ya dhalilisha), maali( badala ya mahali) n.k yamekuwa mengi sana siku hizi.
 
Yaani ni ghafla sana watu hawajui kuandika wala kusema Kiswahili sahihi siku hizi. Matumizi ya uyu/uyo (badala ya huyu/huyo) , aya ( badala ya haya), zarau (badala ya dharau), zalilisha (badala ya dhalilisha), maali( badala ya mahali) n.k yamekuwa mengi sana siku hizi.
umesema vizuri mkuu
 
Nafikiri alitaka kufupisha, badala yake angetakiwa kuandika hivi:

Mjombayo = Mjomba yako
Mjomba -ye= Mjomba yake
Mama - ye=Mama yake
sheeda = shida
kudadavua = kufafanua
mi = mimi
ndo = ndio
sa = sasa
itakwaje = itakuwaje
dingi/dingilai/faza = baba
maza/mazeli = mama
 
Wenyewe Sifa zaidi ndio watawala,hivyo basi wenyewe uwezo wanakimbilia mafungu makubwa na ualimu unabaki ....
Elimu yetu inasikitisha sqna.

Uwezo wa kuipaisha tunao lakini naona hakuna mwenye nia hiyo.
 
Ukitaka kujua thamani halisi ya elimu yetu anangalia malipo ya watumishi huko

Watumishi wenyewe mapoyoyo. Kama malipo madogi kwanini hawaendi kufanya kazi zingine kama ukulima au ufugaji?

Kuku wank7enyej7 hatanuwe kijiji cha mbali vipi, wateja wanawafata hukohuko.

Wawache kazi, ndiyo dawa pekee ya kuongezewa mishahara.
 
Back
Top Bottom