Dah! Kutoka mbeba maboksi mpaka wakili msomi! Umenipendelea sana. Usomi huo mi mbeba maboksi niutoe wapi? [emoji3]
Hata hivyo, ahadi ni deni. Nimechoka kama mbwa, lakini naamini katika kutimiza ahadi.
Haya, twende kazi;
Kama nilivyosema hapo awali, maneno yote mawili, ‘onesha’ na ‘onyesha’, ni sahihi.
Neno sahihi katika kuelezea utumikaji wa hayo maneno ni ‘kibadala’ au ‘vibadala’. Kwa kimombo nadhani ni ‘alternate’.
Kama picha ya sehemu ya ukurasa inavyoonyesha hapo chini, kibadala ni moja kati ya maneno mawili au zaidi yanayotofautiana kidogo kwenye maandishi au matamashi, lakini yanakuwa na maana sawa; onyesha/ onesha. Na unakumbuka niliongelea mambo ya lahaja? Hata wao watu wa TATAKI wamelizungumzia hilo [2009 walibadili jina kutoka TUKI]. TATAKI ni Taasisi ya Taaluma za Kiswahili.
View attachment 2967852
Uzuri wa hizi kamusi za siku hizi, huwa zina maelezo mazuri sana kuhusu masuala ya lugha.
Kwa mfano, moja ya hizi kamusi nilizonazo ina orodha kabisa ya vibadala vya maneno na mojawapo ya hayo maneno ni ‘onyesha’ na ‘onesha’.
View attachment 2967856
Huu hapa ukurasa yaliyopo hayo maneno.
View attachment 2967857
Hapa chini ni kipande cha ukurasa wa kamusi ya Kiswahili sanifu tu. Yaani Kiswahili peke yake.
Angalia hayo maneno ‘onesho’ na ‘onesha’ utaona yakifuatiwa na neno ‘pia’ “onyesho “ na “onyesha”.
View attachment 2967860
Hiyo’pia’ maana yake ni kwamba hicho kibadala cha hilo neno, nacho ni sahihi pia!
Tukienda kwenye kamusi ya Kiingereza.- Kiswahili, neno ‘show’ wao wamelitafsiri kama ‘onyesho’.
View attachment 2967870
Hii hapa orodha ya watu waliohusika kuzitengeneza hizi kamusi. Wachache kati yao nafahamiana nao. Ni watu wanaoaminika kwa uwezo wao kwenye fani yao.
View attachment 2967871
Haya bana, baadaye. Nimechoka kama mbwa koko leo.
[emoji3577]