Kiswahili fasaha ni kipi?

Kiswahili fasaha ni kipi?

Center na centre, ipi ni sahihi?

Color na colour, ipi ni sahihi?

Najua ni misamiati ya lugha tofauti. Ila, kuna sehemu nataka kuelekea na hayo maelezo ya utofauti wake….
Kulinganisha centre vs center, color vs colour au hata salon vs saloon, kamwe hakushabihi uhusiano wa ndiyo vs ndiyo.

Hizo ni tahajia (spelling) tofauti za neno lenye maana moja. Ni kama ambavyo mtu angesema maalum vs maalum au mahususi vs makhususi, hasa vs haswa, nk.

Lakini ndiyo na ndio ni maneno mawili yenye maana tofauti.
 
  • Thanks
Reactions: ywf
Ndiyo nakuja.
Ndiyo, nakuja.
Usipoweka mkato utalazimika kutumia ndipo (ndipo nakuja). Hii ni kwa sababu ndiyo na nakuja ni sentensi mbili kamili ambazo kila moja hujitosheleza.

Aidha, unaweza kusema:
Ndiyo. Nakuja.

Ndiyo, nakuja - yes, I'm coming. (Dhana ya uyakinifu/kukubali)
Ndipo nakuja - I'm on my way coming. (Dhana ya wakati).
 
Kulinganisha centre vs center, color vs colour au hata salon vs saloon, kamwe hakushabihi uhusiano wa ndiyo vs ndiyo.

Hizo ni tahajia (spelling) tofauti za neno lenye maana moja. Ni kama ambavyo mtu angesema maalum vs maalum au mahususi vs makhususi, hasa vs haswa, nk.

Lakini ndiyo na ndio ni maneno mawili yenye maana tofauti.
Lugha nyingi zina lahaja, ikiwemo Kiswahili.

Utofauti wa lahaja huwa upo kwenye tahajiia, matamshi, uanuai wa misamiati, na kadhalika.

Ndio na ndiyo, yote ni maneno sahihi ambayo hutumika kwa kubadilishana.

Pia, ndio huwa lina maana nyingine kutegemea na muktadha unaotumika.

Neno ndio, katika muktadha mwingine na lahaja tofauti, hutamkwa kama ‘ndo’.

Maelezo yote haya ni kwa mujibu wa kamusi zangu za Kiswahili sanifu.

Wewe una kamusi yoyote ya Kiswahili hapo ulipo?
 
  • Thanks
Reactions: ywf
Ungekuwa unaweka na sentensi kabisa, ungeona jinsi unavyoenda kinyume nyume.

Ndiyo na ndio vyote vinakubali (vinaonesha uyakinifu), isipokuwa muktadha wa matumizi yao ni tofauti.

1. Huwezi kusema ndio nimekubali. Tunasema ndiyo, nimekubali.

2. Ndio hawa walijiunga na chama hivi karibuni. (sahihi)

3. Unaipenda JF - ndiyo au siyo? (Ni makosa kusema ndio au sio!)

NB: Kwa namna gani ndiyo hutumika kama kiunganishi?
Hujanielewa.

Ova
 
Kwa mbaali kama naelewa tofauti kati ya 'ndio' na 'ndiyo'.
1. Hawa ndio vijana wenye nguvu.
2. Ndiyo nakuja.
Kwa mifano hii, wataalam mtasema kama nimeelewa au bado
"ndio" inaweza kunyambulika zaidi.
Arusha ndiko.........
gazeti hili ndilo.....
humu ndimo....
vitabu hivi ndivyo....
 
Lugha nyingi zina lahaja, ikiwemo Kiswahili.

Utofauti wa lahaja huwa upo kwenye tahajiia, matamshi, uanuai wa misamiati, na kadhalika.

Ndio na ndiyo, yote ni maneno sahihi ambayo hutumika kwa kubadilishana.
kwenye concept ya lahaja upo sahihi kila lugha huwa na lahaja kama ulivyoeleza.

ila katika haya maneno mimi naona dhana yake hubadilika kulingana na jinsi yanavyotumika katika sentensi tu.

kwamba linaweza kuwekwa mbele ya nomino na likawa kama kivumishi.

au likasimama lenyewe mwanzo wa tungo kama kiwakilishi cha kukubali.
 
Mko poa bila shaka

Kiswahili fasaha ni kipi au neno sahihi ni lipi

1. Ndiyo
Au
2. Ndio

Lipi neno sahihi
Najaribu;
*Ndio inatumika kulezea jambo, watu, n.k. Mfano: Hawa ndio vijana wa CCM.
*Ndiyo maana yake ni kubali, itikia au kiri.
Mfano: Tanzania inapatikana Afrika mashariki?...Ndiyo
 
Mko poa bila shaka

Kiswahili fasaha ni kipi au neno sahihi ni lipino

1. Ndiyo
Au
2. Ndio

Lipi neno sahihi
Yote ni sahihi.
NDIVYO = matamshi
NDIO = maandishi

Kama ilivyo kwa
INZI = maandishi
NZI = matamshi
MWEMBE
MUEMBE.
and so on and so forth na kadhalika na n.k
 
Lugha nyingi zina lahaja, ikiwemo Kiswahili.

Utofauti wa lahaja huwa upo kwenye tahajiia, matamshi, uanuai wa misamiati, na kadhalika.

Ndio na ndiyo, yote ni maneno sahihi ambayo hutumika kwa kubadilishana.

Pia, ndio huwa lina maana nyingine kutegemea na muktadha unaotumika.

Neno ndio, katika muktadha mwingine na lahaja tofauti, hutamkwa kama ‘ndo’.

Maelezo yote haya ni kwa mujibu wa kamusi zangu za Kiswahili sanifu.

Wewe una kamusi yoyote ya Kiswahili hapo ulipo?
Ngeli ya A/WA (mtu, mnyama, nk)
Hutumia urejeshi wa ndiye (katika umoja) na ndio (katika wingi).

1. Mnyama huyu ndiye mwenye kasi zaidi.
2. Wanachama hai ndio sehemu ya ufanisi wa kila shirika.

Ngeli ya KI/VI (mfano kiatu, kiti, nk)
Hutumia urejeshi wa ndicho (katika umoja) na ndivyo (katika wingi).
1. Kiatu chake cha uongozi ndicho kinampatia umaarufu mkubwa.
2. Viti kadhaa vya ubunge ndivyo vitapotezwa na chama tawala.

Ngeli ya I/ZI (mfano harakati, karatasi, kalamu, nk)
Hutumia urejeshi wa ndiyo (katika umoja) na ndizo (katika wingi).
1. Kalamu mkononi mwa mtu mweledi ndiyo silaha madhubuti kuliko mtutu wa bunduki.
2. Harakati za uchaguzi mkuu ndizo zimeshika kasi nchini kuliko chochote kingine.

Ngeli ya U/ZI (mfano uzi, ubao, ubongo, nk)
Hutumia urejeshi wa ndio (katika umoja) na ndizo (katika wingi).
1. Ubongo ndio ogani pekee mwilini ambayo seli zake hazina uwezo wa urajilishaji; zikifa zimekufa.
2. Mbao za mninga ndizo mashuhuri sana, japo si imara kama za mtiki.

Ngeli ya LI/YA (mfano shamba, gari, yai, nk)
Hutumia urejeshi wa ndilo (katika umoja) na ndiyo (katika wingi).
1. Yai ndilo lilianza kuwepo ndipo kuku akafuata.
2. Magari yatumiayo mfumo wa gesi ndiyo mkombozi wa uchumi na mazingira.

Ngeli ya U/I (mfano muziki, mfumuko, mwanga, nk)
Hutumia urejeshi wa ndio (katika umoja) na ndiyo (katika wingi).
1. Mfumuko wa bei ndio unawarudisha nyuma kiuchumi wafanyabiashara wengi.
2. Kwa sasa, miziki duni ndiyo chanzo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili duniani.

Ngeli ya I (mfano sukari, simanzi, ari, oksijeni, surua, Dodoma, nk)
Hutumia urejeshi wa ndiyo. Haina wingi.
1. Oksijeni ndiyo gesi ya pili kwa ujazo hewani baada ya Naitrojeni.
2. Dodoma ndiyo imetashifika kufuatia uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo.

Ngeli ya U (mfano mchana, unadhifu, nk)
Hutumia urejeshi wa ndio. Haina wingi.
Unadhifu ndio unambeba katika suala zima la ajira.

Ngeli ya KI (mfano Kipemba, Kiswahili, Kichina, nk)
Hutumia urejeshi wa ndiyo (aidha, hutumika ndicho). Haina wingi.
Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya taifa letu.
Kichina ndicho kitakapiku Kiingereza hivi karibuni.

Ngeli ya PAMUKU (mfano pangu, mwetu, kusini, nk)
Hutumia urejeshi wa ndipo, ndimo, na ndiko mtawalia. Haina wingi.
Pangu ndipo panavuja tangu masika iliyopita.
Mwetu ndimo alianzia kufanya utafiti wake.
Kusini ndiko kutulivu zaidi.
 
Najaribu;
*Ndio inatumika kulezea jambo, watu, n.k. Mfano: Hawa ndio vijana wa CCM.
*Ndiyo maana yake ni kubali, itikia au kiri.
Mfano: Tanzania inapatikana Afrika mashariki?...Ndiyo
Tanzania ndiyo nchi pekee inayojivunia na kuimarisha Kiswahili.
 
Ndiyo - Yes
Ndio - ni conjuction
Nilikuwa naumwa ndio maana sikuja shule.
Je, wewe ni kijana? Ndiyo.
Huu ni mtazamo wangu kwa sababu mimi si mwana kiswahili. Ila katika hata dictionary ya TUKI neno linalowakilisha yes ni ndiyo
Kuna ili na hili ,kuna ilo na hilo.
 
Back
Top Bottom